Tuesday, January 7, 2014

ZITTO KABWE AIBUKA KIDEDEA DHIDI YA CHADEMA, WANASHERIA WA CHADEMA WAMESHINDWA KUTOA HOJA ZA MSINGI


http://azizicompdoc.blogspot.com/ 
Taarifa kutoka hapa mahakama kuu Dar ni kwamba Zitto Kabwe ameshinda kesi dhidi ya Chadema, wafuasi wa Zitto wamejawa na furaha kupita kiasi


Kwa mantiki hiyo Zitto amepewa kinga na mahakama hiyo, hivyo Chadema haitamjadili kwa namna yoyote ile


Ikumbukwe kuwa leo macho na maskio ya watanzania   hasa  wafuasi  na  wapenzi  wa  CHADEMA yalielekezwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John Utumwa   alikuwa  akitoa  hukumu  dhidi  ya  Zitto Kabwe  na CHADEMA....

 


Zitto ambaye alikuwa   ni  Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho  iliyokutana  tarehe  3  na  4  mwezi  huu  kujadili  hatima  ya  uanachama wake  wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake... Akisoma  hukumu  ya  kesi  hiyo  baada  ya  kuiahirisha  jana, Jaji  wa mahakama  hiyo,Jaji Utamwa  ameridhia  pingamizi  lililotolewa  na  mh. Zitto Kabwe la  kutojadili  uanachama  wake na  kuitaka  kamati  kuu  ya  CHADEMA  au  chombo  kingine  chochote  kisijadili  uanachama  wake   hadi  kesi  yake  ya  msingi ( rufaa )  itakaposikilizwa  na  baraza  kuu  la  chama  hicho.
 Mh Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kutojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia kufanyika kesho, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote.
                     Zitto Kabwe akiingia mahakama Kuu Dar es Salaam leo
 Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
 Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto ana wakili wake Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa wakisubiri uamuzi wa mahakama, ambapo Zitto aliibuka kidedea kwa pingamizi lake kukubaliwa hivyo kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika kesho kukatazwa kumjadili kwa namna yoyote Zitto.
Quantity : Add to Cart

1 comment:

  1. hapa umeweka kiporo kwenye friji na kitaliwa tu kama sio nawewe kitaliwa na watoto

    ReplyDelete

Labels

Blogroll

Labels

About