Welcome to our online store Portal

Template Information

Tuesday, April 30, 2013

Mwanajeshi wa Ufaransa auawa Mali


Ufaransa inatarajiwa kuanza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Mali

Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa nchini Mali ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa maafisa wa Ufaransa, mwanajeshi huyo kutoka kikosi maalum cha Ufaransa aliuawa Magharibi mwa nchi baada ya gari lake kulipukiwa na bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara.

Hadi kufikia sasa wanajeshi sita wa Ufaransa wameuawa tangu Ufaransa kuanza operesheni yake dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu waliokuwa wanadhibiti Kaskazini mwa nchi
Ufaransa ilitangaza kuanza kuondoa baadhi ya wanajeshi wake 4,000 walioko Mali.
Lakini wengine 1,000 watasalia nchini humo hadi mwakani kuweza kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu walio na uhusiano na kundi la Al-Qaeda

Baadhi ya miji, imeweza kudhibitiwa na wanajeshi hao, lakini wapiganaji hao wangali kwenye maficho yao ya mwisho Kaskazini mwa Mali ambako wanafanya mashambulizi ya kuvizia dhidi ya wanajeshi wa Mali na Ufaransa.
Hivi maajuzi Umoja wa Mataifa uliafikia kunda kikosi cha wanajeshi 12,000 kushika doria nchini Mali.
Watashirikiana na kikosi cha wanajeshi 6000 ambao tayari wako nchini humo.
Rais Francois Hollande ametoa rambi rambi zake kwa familia za waliouawa huku akiwasifu kwa ujasiri wao nchini Mali.
 Baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa

View detail

Monday, April 29, 2013

NAFASI ZA MAFUNZO NCHINI INDIA BUREEEEE!!!!


NAFASI ZA MAFUNZO YA FANI MBALI MBALI NCHINI INDIA KWA WATANZANIA WAFANYAKAZI WA SERIKALI, KILA KITU KIMELIPIWA, WE UNATAKIWA KUCHAGUA FANI INAYOENDANA NA UJUZI WAKO NA KUJAZA FORM TUU, BOFYA HAPO CHINI KWA KUCHANGAMKIA NAFASI HIZI.
View detail

Sunday, April 28, 2013

Zuma akutana na Tiangaye Pretoria


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nicolas Tiangaye, wamekutana mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, na wamekubaliana kuzidisha uhusiano baina ya nchi mbili hizo.
Uhusiano uliharibika baada ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa mwezi March wakati wapiganaji walipoiteka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliarifu kuwa wanajeshi hao walipelekwa huko ili kampuni za biashara za Afrika Kusini zipate kandarasi za madini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wakuu wa Afrika Kusini walikanusha hayo.
View detail

Wednesday, April 24, 2013

RAIS WA KENYA AANZA KUUNDA SERIKALI YAKE

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya ambapo ametangaza majina ya mawaziri wanne. Wanne hao ni pamoja na Dkt. Fred Okeng'o Matiangi ambaye ni waziri mteule wa Teknolojia na Mawasiliano, Henery Rotich ameteuliwa wizara ya Fedha, James Wanaina Macharia ndiye Waziri mteule wa Afya na Balozi Amina Mohammed ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.
Ilitarajiwa kwamba Rais Kenyatta angewataja mawaziri wote 18, lakini amesema wengine watatangazwa baadaye na kuomba taifa kuwa na subira. Huku haya yakiarifiwa Bunge la Kenya limeidhinisha kamati maalum ambayo itawachuja mawaziri watakaoteuliwa na Rais. kamati hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.
Chini ya katiba ya Kenya sharti bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo Mawaziri, mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba.
View detail

Friday, April 19, 2013

Police US wafanya Msako wa mshukiwa wa mashambulizi Boston


Mmoja wa washukiwa wa mashambulizi ya Boston
Polisi nchini Marekani wanamsaka mshukiwa mkuu wa mashambulizi yaliyotokea katika mbio za Boston Marathon katika mji mdogo karibu na Boston.
Operesheni kubwa ya polisi inayoendelea ilianza baada ya afisaa mmoja wa polisi kuuawa katika chuo ya mafunzo anuai cha Massachusetts .
Mshukiwa mmoja aliuawa baada ya polisi kumfukuza hali iliyosababisha ufyatulianaji wa risasi umbali wa kilomita kumi kutoka Boston.
Mshukiwa mwingine ambaye picha yake ilionyeshwa alikuwa amevalia kofia huku akikimbia kutoka eneo la Watertown.
Polisi walisema kuwa wanaume hao wawili walishukiwa kumuua polisi mmoja, katika chuo hicho cha Massachusetts Jumanne jioni. Thursday.
Baadaye waliiba gari mmiliki wake akiwemo ndani kwa kutumia nguvu lakini walimwachilia mmiliki bila kumjeruhi.

Shirika la FBI limetoa picha kadhaa za washukiwa hao.
Wawili hao waliwasrushia polisi mabomu na hata kwuafyatulia risasi kabla ya kusimamishwa katika eneo la Watertown.
Wakaazi wa mtaa huo wameshauriwa kusalia makwao.
View detail

Thursday, April 18, 2013

VURUGU ZAZIDI BUNGENI! KODI ZA WALALAHOI ZAPOTEA

RAIS KIKWETE, DK SHEIN WAONGOZA MAZISHI YA FATMA BINTI BARAKA "BI KIDUDE" VISIWANI ZANZIBAR LEO.


Jeneza lenye mwili wa Msanii Mkongwe wa Muziki wa Mwambao (taarab) hapa nchini,Marehemu Fatma Bint Baraka (Bi Kidude) likitolewa katika msikiti wa Mwembeshauri aliposaliwa mchana wa leo,tayari kwa kwenda kwenye Mazishi. 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said sadiq akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Nasibu Abdul Juma (Diamond) akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

View detail

MAZISHI YA BI KIDUDE YALIYOFANYIKA ZNZ LEO

Baadhi ya watanzania walioweza kuhudhuria ktk mazishi ya Bi kidude
View detail

Thursday, April 11, 2013

CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA TAWI LA LINDI WAPATA GARI MPYA

 Katika kuhakikisha Tunatoa huduma kwa kuwafikia wananchi wote kwa kiwango kinachotakiwa, tumefanikiwa kupata Gari mpya kwa kituo cha lindi, na tunajipanga zaidi kua na jengo la kwetu ktk mkoa huo ili tuwahudumie ipasavyo wananchi wa lindi na wao wafaidike zaidi na huduma zetu

 Mwonekano wa gari hiyo kwa mbele

 Mwonekano wa gari hiyo kwa ubavuni

 Mwonekano wa gari hiyo kwa mbele
Mwonekano wa gari hiyo kwa nyuma
View detail

Tuesday, April 9, 2013

NAFASI ZA MAFUNZO CHINA KWA WATUMISHI WOTE WA SERIKALI

TANGAZO KWA UMA

COMPUTER DOCTOR ANACHUKUA NAFASI HII KUWAFAHAMISHA WATUMISI WOTE WA SERIKALI KUA KUNA NAFASI NYINGI ZIMETOLEWA NA SERIKALI KWA WATUMISHI WA SERIKALI KWENDA KTK MAFUNZO YA FANI MBALIMBALI NCHINI CHINA. GHARAMA ZOTE ZIMELIPIWA. UNACHOTAKIWA NI KUCHAGUA FANI INAYOENDANA NA UJUZI WAKO NA KUJAZA FOMU MAALUMU INAYOPATIKANA KTK TANGAZO HILI.
KUMBUKA NAFASI HIZI NI KWA WATUMISHI WOTE WA SERIKALI NA UMA. MADIWANI PIA KUNA NAFASI ZENU. TUNAWATAKIA MAFANIKIO KTK KULITEKELEZA SUALA HILI MUHIMU KWA MANUFAA YA NCHI YETU.
 


View detail

Monday, April 8, 2013

Margaret Thatcher afariki dunia


Margaret Thatcher

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher ameaga dunia.
Thatcher alikuwa na umri wa miaka 87 na msemaji wake ameelezea kuwa alifariki kutokana na ugonjwa wa kiharusi
Thatcher alikuwa mwanamke wa kwanza waziri mkuu wa Uingereza na anasemekana kuleta mageuzi makubwa kisiasa Uingereza alipochukua mamlaka mwaka 1979.
Pia alisifika sana na kuwa mwanamke mwenye ushawishi mkubwa katika View detail

WALIOFARIKI MISRI WAONGEZEKA



Watu wawili wameripotiwa kufariki katika makabiliano nje ya kanisa la Kikopti nchini Misri.
Duiru zinasema kuwa hali ya utulivu ilirejea katika eneo la Abbassiya ambako polisi walikuwa kwa wingi kudhibiti hali ya usalam. Eneo hilo linapakana na kanisa ambako makabiliano yalitokea.
Waandamanaji kadhaa wa ambao ni waumini wa kanisa hilo, walikusanyika katika eneo hilo mapema asubuhi ya leo
Makabiliano makali yalitokea nje ya kanisa hilo kufuatia mazishi ya wakristo wanne wa kikopti waliouawa katika ghasia za kidini siku ya Alhamisi.

Waombolezaji waliokuwa wanatoka katika kanisa hilo walikabiliana na wenyeji wa eneo hilo nje ya kanisa.
Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi kujaribi kuwatawanya waandamanaji. Zaidi ya watu 80 walijeruhiwa kwa mujibu wa shirika la kitaifa la habari.
Wizara ya afya ilisema kuwa mtu mmoja aliuawa katika ghasia hizo.
Waombolezaji awali walikuwa wakiimba nyimbo za kupinga serikali ya rais Mohammed Morsi.
Walioshuhudia vurugu hizo waliambia wanahabri kuwa ghasia zilianza baada ya umati wa watu kuvamia kikundi cha waombolezaji walipokuwa wanaondoka kanisani kwa kuwarushia mawe na mabomu ya petroli. Wakati huo pilisi walikuwa wachache sana katika eneo hilo.

Wakristo nao walijibu mashambulizi dhidi yao kwa kuwarushia mawe watu hao hadi polisi walipowasili katika eneo hilo na kujaribu kusitisha vurugu kwa kuwarushia watu gesi ya kutoa machozi
Duru zilisema kuwa barabara zilizoko karibu na eneo hilo zilikuwa na ghasia kati ya wakristo na watu wasiojulikana

Aidha moto uilianzishwa katika jengo lililokuwa karibu na kanisa hilo lakini moto huo ukazimwa kwa wakati.
Pia inaarifiwa kuwa Rais Morsi alilaani ghasia hizo kupitia kwa njia ya simu kwa papa Tawadros wa pili ambaye ndiye kiongozi kwa kanisa la kikopti.
''Shambulizi lolote dhidi ya kanisa hilo ni kama shambulizi dhidi yangu,'' alisema Papa Towadros ambaye pia aliwataka watu kuwa watulivu.
View detail

Friday, April 5, 2013

TBC HABARI 05/04/2013

Kamati ya ardhi, maliasili na mazingira yaamuru kuvunjwa haraka ghorofa lingine pembeni ya lile lililobomoka jijini Dar


 Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli. akiongea leo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo lilikoporomoka ghorofa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo, akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka. 

Kamati hiyo imeziamuru halmashauri za Wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni kufanya tathmini ya majengo yote na kuchukua hatua mara moja zitapogundulika zimejengwa chini ya kiwango.
Tayari watu 11 wanaotuhumiwa kuhusika katika ujenzi wa ghorofa lililoporomoka wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kuua bila kukusudia 
 
 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka akiwa eneo la jengo lilioporomoka. Nyuma yake ni jengo ambalo linajengwa na mjenzi yule yule aliyejenga liliporomoka. Kamati hiyo imetoa siku nne kwa mjenzi kubomoa jengo hilo ambalo linasemekana nalo limejengwa chini ya kiwango. 
 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk TerezyaHuvisa wakimsikiliza   Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka  na  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
 
  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli akijadili jambo na Bw. Azim Dewji pamoja na mjumbe wa kamati Mhe Zakhia Meghji. View detail

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI MUSHI ZANZIBAR AFIKISHWA KIZIMBANI LEO


Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) akiongozwa na Askari polisi kuingia katika Mahakama Kuu ya Zanzibar  kusikiliza kesi inayomkabili.


 
 wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) kulia akizungumza na mawakili wake Abdalla Juma kushoto na Rajab Abdalla muda mfupi baada ya kutajwa kwa kesi yake Mahakamani hapo. 
 Mawakili wanaomtetea Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri , Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) wakili Abdalla Juma (kulia) na Rajab Abdalla wakiwa mezani pao  kabla ya kutajwa kwa kesi ya mteja wao katika mahakama Kuu Vuga mjini Zanzibar
Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) akiwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kesi yake kutajwa mahakamani hapo.
View detail

MATOKEO KWA WANAFUNZI WA OPEN YAKO HEWANI

Dear Students

The provisional results of the Jan/Feb 2013 examinations are now available
online and can be accessed by login into SARIS at http://des.out.ac.tz or
http://www.out.ac.tz)

In case you cannot see your results, please contact your DRC to access the
raw marks; all queries related to missing marks into SARIS should be
directed to des@out.ac.tz but only after failing to locate the marks at
your DRC’s office, the main cause of missing marks is the availability of
old marks in your SARIS which have prevented the entry of new marks.

Please note that, these are only 'Provisional Results', they will become
final only after approval of relevant authorities.


Regards
Lawi
View detail

KOREA YA KASKAZINI YAIPA WASIWASI MAREKANI

Jeshi la Marekani likiajiandaa kwa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini

Marekani imepeleka mitambo ya kukinga makombora katika kisiwa cha Guam katika bahari ya Pacific huku Korea Kaskazini ikitishia kurusha makombora ya nuklia nchini humo.
Idara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema kuwa mitambo hiyo itakuwa tayari katika kipindi cha wiki kadhaa , na kuongeza kwa zana za kivita ambazo zilipelekwa katika eneo hilo.
Korea Kaskazini ilitaja kisiwa cha Guam kuwa miongoni mwa maeneo yanayolengwa kwa mashambulizi ikiwemo Hawaii na Marekani.
Korea Kaskazini haidhaniwi kuwa na teknolojia ya kutosha kushambulia Marekani kwa zana za nuklia au makombora ya masafa marefu.
Korea Kaskazini inasema kwamba imewaweka wanajeshi wake, tayari kwa shambulio dhidi ya Marekani ikiwemo kutumia zana za nyukilia.
Taarifa hii imejiri wakati Marekani imeimarisha mitambo yake ya kukinga makombora katika kisiwa cha Guam kilichoko bahari ya Pacific.

Idara ya ulinzi ya Korea Kaskazini imesema inatoa taarifa kwa Marekani kwamba jeshi lipo tayari kushambulia bila huruma, kile imetaja kama vitisho vya Marekani dhidi yake.
Utawala wa Pyongyang ulionekana kukerwa na hatua ya Marekani ya hivi maajuzi ambapo wanajeshi wake walifanya mafunzo ya pamoja na ambayo yalihusisha utumizi wa zana za kivita.
Hata hivyo wachanganuzi wamesema Korea Kaskazini haina silaha ambazo zinaweza kushambulia ardhi ya Marekani, japo katika siku za karibuni imefanya majaribio ya makombora ua masafa marefu.
Hapo jana Jumatano, Korea Kaskazini iliwazuia wafanyikazi wa Korea Kusini kuvuka mpaka kuelekea katika viwanda vya pamoja vinavyomilikiwa na nchi mbili, na hivyo kukatiza uhusiano uliobaki kati yake na Kusini.
Baadhi wanaona malumbano ya sasa kama hatua ya Korea Kaskazini kushinikiza Marekani kuanzisha mazungumzo ya pamoja ambayo yataafikia mkataba wa amani.
View detail

Wednesday, April 3, 2013

Afrika ya Kati wasitishwa Msako dhidi ya Kony


Mtoro Joseph Kony


Serikali ya Uganda inasema kuwa imesitisha msako wake wa kiongozi mtoro wa waasi wa LRA Joseph Kony, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Uganda inasema imeamua kuchukua hatua hiyo kufuatia mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo baada ya rais Francois Bozize kung'olewa madarakani.
 
Pia imeelezea kuwa serikali ya mpito inayoongozwa na kiongozi wa waasi imetatiza shughuli zao.
Uganda inasema kuwa wanajeshi wake katika eneo hilo ambako waasi walichukua mamlaka siku kumi zilizopita, watasalia katika kambi zao hadi muungano wa Afrika utakapotoa mwongozo.
Joseph Kony anayeongoza kundi la waasi wa LRA, anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.
Anaaminika kujificha na wapiganaji wake katika misitu inayopakana na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
View detail

NAULI MPYA ZATANGAZWA RASMI NA SUMATRA

VIWANGO VIPYA VYA USAFIRI WA DALA DALA NA MABASI TOKA SUMATRA 

 Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.


SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji.  Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe.  Bofya Hapa Kuona viwango vya nauli View detail

Tuesday, April 2, 2013

Wafungwa wa Kisiasa waachiliwa huru na Rais Bashir


Rais Omar el Bashir

Rais wa Sudan Omar al Bashir, ameagiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa vikao vipya vya bunge, Rais Bashir alitoa wito wa kufanyika mashauriano na vyama vingine vya kisiasa.
Wiki jana makamu wa rais Ali Osman Taha aliwaalika waasi kutoka majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile,kushauriana kuhusu katiba mpya.
Hata hivyo walikataa mwaliko huo.
Waandishi wa habari wanasema kuwa hali ya wasiwasi imeanza kupungua kati ya Sudan na Sudan Kusini tangu nchi hizo mbili zikubaliane kurejelea shughuli ya kuchimba na kusafirisha mafuta.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop