Welcome to our online store Portal

Template Information

Thursday, April 10, 2014

TIMU YA MPIRA YA WATOTO WA MITAANI YAPOKELEWA KWA SHANGWE

WTT1
Mwenyekiti wa Timu ya watoto wa mitaani ya jijini Mwanza Alfat Mansoor (Dogo) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jijini Dar es Salaam.
WTT2
Mchezaji aliyesabibisha timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania kuibuka mabingwa wa Dunia kw kufunga magoli matatu kwa mojadhidi ya Burundi Frank William(mwenye kofia nyekundu) akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake mara baada ya juwasili airport,kushoto ni Hassan Jaffar,Emmanuel Amos, na Hassan Seleman.
WTT3
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda akiwa amebeba kombe la ubingwa dunia mara baada ya kupokea timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania iliyochukua ubingwa huo kwa kuifunga timu kutoka Burundi jumla ya magoli 3-0. Timu hiyo imewasili nchini jana majira ya saa 9:35 mchana na kulakiwa na uongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa soka.
WTT4
Wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania ilyo nyakuwa ubingwa wa dunia katika mashindano yaliyofanyika nchini Brazil kwa kushirikisha timu za watoto wa mitaani, wakiwa wamebeba makombe waliyoyapa katika mashindano hayo.
 WTT5
Afisa Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Frank Shija akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani(Picha zote na Frank Shija, Afisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM).
 
View detail

Monday, April 7, 2014

NAFASI ZA KAZI KWA WATANZANIA WENYE SIFA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

On behalf ofTanzania Food and Nutrition Centre (TFNC), Tea Board of Tanzania (TBT),
Occupational Safety and Health Authority (OSHA), College of Business Education
(CBE), Tanzania Institute of Education (TIE) and The Institute of Rural Development
Planning (IRDP), Public Service Recruitment Secretariat invites qualified Tanzanians
to fill 8 vacant posts in the above Public Institutions. Follow the link for more information View detail

WATOTO WA MITAANI WA TANZANIA WATWAA KOMBE LA DUNIA BRAZIL

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Timu ya taifa ya Tanzania ya watoto wa mitaani wakishikilia Kombe la Dunia walilonyakua Brazil
Timu ya taifa ya Tanzania kwa watoto wa mitaani imenyakua Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani, katika mashindano yaliyozishirikisha timu za mataifa mbalimbali duniani huko Rio de Janeiro, Brazil hapo jana.
Ikiwa imetinga fainali za Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani kwa mara ya pili mfululizo, timu hiyo ya Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro.
Katika mechi ya fainali Tanzania iliibanjua Burundi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kulinyakua kombe hili kwa Kuinyuka magoli 3-1 huku mchezaji kiungo mshambuliaji wa Tanzania Frank William akipiga magoli matatu na kuwa nyota wa mchezo. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Tanzania ilikuwa ikiongoza kwa magoli 2-0. Kipindi cha pili iliongeza bao la tatu. Burundi iliweza kupata bao la kufutia machozi zikiwa zimebakia dakika nne mpira kumalizika.
Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuonyesha kiwango cha juu hata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino na Argentina.
Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano hii ya kombe la dunia.
Hii ilikuwa mara ya Pili kwa timu ya Tanzania kutinga fainali za michuano hiyo ya dunia kwa watoto wa mitaani inayofanyika siku chache kabla ya fainali za Kombe la Dunia kuanza mwezi Juni. Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za michuano hii kule Durban Afrika Kusini mwaka 2010 Tanzania ilifungwa na India katika fainali.
Mashindano haya hutambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA.
View detail

WANANCHI WA RWANDA WAKUMBUKA MAUAJI YA KIMBARI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Rwanda imekuwa ikilaumu Ufaransa kwa kilichotokea nchini humo
Rwanda inaadhimisha miaka 20 tangu kutokea mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Watu laki nane waliuawa wengi wakiwa wa kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri. Wote waliuawa na watutsi wenye msimamo mkali.
Hii leo Rais Paul Kagame anatarajiwa kuwasha mwenge ambao utasalia hivyo kwa siku 100 , kipindi ambacho mauaji ya kimbare yalifanyika.
Mgogoro wa kidiplomasia umesababisha Waziri wa sheria wa Ufaransa, kujiondoa katika shughuli za kumbukumbu ingawa Ufaransa inasema kuwa balozi wake ataiwakilisha nchi hiyo.
Wengi wa waathiriwa wa mauaji ya Rwanda, walishambuliwa kwa mapanga kwa siku 100. Mauaji hayo yalianza Aprili mwaka 1994, punde baada ya kufariki kwa hayati Rais Juvenal Habyarimana.
  • 6 Aprili: 1994: Rais Habyarimana afariki katika ajali ya ndege
  • 7 Aprili: Wanajeshi wa Rwanda pamoja na waasi wawaua wananchi
  • 8 Aprili:Kundi la waasi la (RPF) laanza kupambana
  • 11 Aprili: Maelfu wauawa
  • 17 Mei: Baraza la usalama la umoja wa mataifa lasema mauaji ya kimbari yametokea
  • 22 Mei: RPF yadhibiti uwanja wa ndege wa Rwanda
  • 22 Juni: Mauaji ya watutsi yaendelea licha ya kuwepo wanajeshi wa Ufaransa nchini humo
  • 4 Julai: RPF yadhibiti Kigali
Alifariki wakati ndege yake iliposhambuliwa katika anga ya Kigali na kudunguliwa.
Baadhi ya viongozi wa kidini walihusishwa na ghasia zilizofuata kifo cha Habyarmana.
Mauaji ya kimbari yaliisha mwezi Julai 1994 wakati chama cha RPF, kilichokuwa cha waasi wa Tutsi wakati huo, kilipoingia nchini humo kutoka Uganda na kuchukua uongozi wa nchi hiyo.
Kumbukumbu zinaanza kwa kuwekwa mauwa katika eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo na kufuatiwa na kuwashwa kwa mwenge katika uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali.
Mwenge huo umekuwa ukitembezwa katika nchi hiyo kwa miezi mitatu iliyopita
Viongozi wa kimataifa akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair,aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Mnamo Jumapili mamia ya watu walihudhuria maombi kuwakumbuka maelfu waliouawa View detail

SAHIHI ZA HATI YA MUUNGANO ZAZUA UTATA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta kukiri kuchezewa kwa saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Msekwa amesema, ‘mzungumzaji huyo ana lake jambo’.

Sitta akizungumza na mwandishi wetu  juzi mjini Dodoma alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.
Alifafanua kuwa saini ya Nyerere imeongezwa herufi ‘us’ kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno ‘Msekwa’ kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.
Msekwa akizungumza na mwandishi weu jana alisema: “Saini iliyo katika hati original (halisi) ni ya kwangu mimi, lakini huyo anayesema zimechezewa muulizeni atakuwa na lake jambo. Kama kompyuta imekosea ni leo kwa kuwa kipindi hicho kompyuta hazikuwapo.”
Aliongeza: “Ana lengo gani la kutilia shaka, ana lengo gani la kusema imechakachuliwa, kinachotakiwa ni hati original ambayo iko ofisi ya Katibu wa Bunge itolewe, kwanini tuendelee kuandikia mate wakati wino upo?”

Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Taarifa kwa Wananchi Umma (TCIB), Hebron Mwakagenda alisema yote hayo yanatokea ni kuvuruga hoja iliyopo mezani.
Alisema kitendo cha kupoteza muda kuzungumzia suala la kuchezewa kwa saini halitakiwi kwani kama maudhui yake hayakuchezewa basi hoja ya muundo wa Muungano uamuliwe na wananchi wenyewe.
“Tusianze kupoteza muda kwa mambo ambayo hayapo cha msingi wananchi wenyewe waulizwe wanaupenda Muungano au la lakini tusianze kumtafuta mchawi kuwa saini zimechezewa wananchi waamue wenyewe kuhusu Muungano,” alisema Mwakagenda.

Utata huo ulianza wiki hii baada ya kamati za Bunge Maalumu la Katiba kuanza vikao vyake vya kujadili sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba, zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wake.
Hali hiyo ilitokana na kutopatikana kwa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ile ya Sheria ya Baraza la Mapinduzi ya kuridhia Mkataba wa Muungano.
Aprili 2 mwaka huu, Kamati namba 2 ilimwalika, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Pius Msekwa kutoa ufafanuzi kuhusu hati hizo, lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali. Msekwa aliitwa kutokana na kwamba ndiye aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Shamsi Vuai Nahodha, alithibitisha kutokea utata huo na kwamba walilazimika kumuita Msekwa ili kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa na Msekwa alisema saini zilizopo katika hati hiyo ni ya kwake.
Nahodha alisema kwa maelezo ya Msekwa, inaonekana hati ya Muungano ipo Umoja wa Mataifa (UN), kwani kabla ya Muungano, Tanganyika ilikuwa na kiti chake UN na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hali kadhalika.
Aliongeza kuwa baada ya UN kuomba uthibitisho wa Muungano, ndipo walipelekewa hati hiyo na kwamba haijawahi kurejeshwa.
Kwa upande wake Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Hamis Hamad alisema hati hiyo ipo Dar es Salaam na ni moja tu, hivyo siyo rahisi kuipeleka bungeni Dodoma.
View detail

CCM YASHINDA KWA ASILIMIA 85 JIMBO LA CHALINZE


Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Chalinze yametangazwa Chama cha Mapinduzi CCM kimepata jumla ya kura 20,812,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kimepata idadi ya jumla kura 2,828 na chama cha Wananchi CUF kimepata kura 474, AFP kura 78, NRA kura 59
 
Hivyo chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda Kiti cha Ubunge Jimbo la Chalinze na Mh Ridhiwan Kikwete kutangazwa kua mbuge wa jimbo la Chalinze na kuungana na wabunge wenzie baada ya kuapishwa.

View detail

Thursday, April 3, 2014

VYETI VYA MATOKEO FEKI YA HIV VYAUZWA


http://azizicompdoc.blogspot.com/

Idhaa ya BBC kitengo cha Afrika kimebaini kuna watu wanaonunua matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya HIV yakionyesha hawana virusi hivyo nchini Uganda.
Picha za Filamu zilizonaswa kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa hongo kwa wahudumu wa afya ili kupata vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya watu wanaonunua vyeti hivyo visivyokubalika kisheria wanasema wamefanya hivyo ili kupata kazi, kusafiri kwenda ng'ambo ama kwa ajili ya kupata wapenzi wa ngono.
Mwandishi wa BBC wa Kampala Catherine Byaruhanga alilitembelea kliniki 15 bila ya kujitambulisha.
Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo zilikuwa tayari kumpa vyeti bandia vya kuthibitisha kuwa hawana virusi vinavyosababisha ukimwi vya HIV.
Wanaosimamia kliniki hizo walitaka hongo kati ya Dola 10 na 20 kwa kila cheti.
Picha za video tulizopiga kisiri katika maduka ya kupiga chapa katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Uganda, Kampala zinathibitisha kuwa mtu anaweza kuigiza cheti pia kwa urahisi sana.
BBC ilipomkabdihi Waziri wa Afya, Ruhakana Rugunda, ushahidi huo, alikubali kuwa hiyo ni changamoto kubwa lakini akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi kuwakamata na kuwashitaki wanaohusika katika ufisadi huo.
Serikali ya Marekani hutoa kiwango kikubwa cha peza za miradi inayotumiwa kupambana na ukimwi nchini Uganda.
Balozi wa Marekani alitoa wito kwa viongozi wa taifa hilo kufanya bidii zaidi kupambana na kashfa hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa hana uhakika kuwa Dola za Marekani hazijatumiwa katika kliniki hizo zinazotoa vyeti bandia. View detail

MAMA SALMA APEWA CHETI CHA HESHIMA

IMG_0091
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea cheti maalum cha ulezi wa heshima wa Chama cha wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika walioko nchini Ubelgiji (Honory Patronese of the Association of the Spouses of African Ambassadors in Belgium) kutoka kwa Mke wa Balozi wa Cameroon nchini Ubelgiji Mama Christiane Eloundov de Evina wakati wa chakula cha mchana walichowaandalia wake wa Marais wa Afrika jijini Brussels tarehe 2.4.2014.
IMG_0100
Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mama Adelaida Kamala akimkabidhi Cheti Maalum cha ulezi wa heshima cha wenza wa mabalozi wa Afrika walioko Ubelgiji, Mke wa Rais wa Cameroon Mama Chantal Biya wakati wa chakula cha mchana walichowaandalia wageni hao kwenye hoteli ya Sheraton tarehe 2.4.2014.
IMG_0123
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika pamoja wa wenza wa Mabalozi wa nchi hizo mara baada ya kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenza hao tarehe 2.4.2014.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amepewa cheti na Umoja wa wake wa Mabalozi  wa Afrika waishio katika  nchi za Jumuia ya  Ulaya kwa kutambua na kuthamini mchango wake na kazi anazozifanya za kuwasaidia wanawake, wasichana  na watoto wa Tanzania.
Cheti hicho amekabidhiwa jana katika hafla fupi  ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na wake hao wa mabalozi katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya Sheraton mjini Brussels.
Mama Kikwete ni mmoja kati ya wake wa Marais wa tano wa  Afrika waliokabidhiwa vyeti hivyo vya heshima kutokana na kazi zao wanazozifanya za kuisaidia jamii na kuhakikisha kuwa inapata mahitaji ya muhimu kama huduma ya afya na elimu.
Akiongea kabla ya kuwakabidhi wake hao wa marais vyeti hivyo Mke wa Balozi wa Equatorial  Guinea  ambaye pia ni rais wa umoja huo Mama Mangue de Nvono Nca alisema nia ya kuanzishwa kwa umoja wao ni kulitambulisha bara la Afrika ambalo linajulikana  kuwa na  changamoto za njaa, magonjwa, kutokuwa na haki na  usalama wa kutosha katika nchi za Ulaya.
“Siyo kama Bara letu la Afrika linakabiliwa na changamoto peke yake bali pia limejaliwa kuwa na  umoja, mshikamano na  ukarimu na haya yote yamejidhihirisha  kwetu leo hii kutokana na kitendo cha wake wa marais wetu kushiriki pamoja nasi katika hafla hii  na kubadilishana mawazo”, alisema Mangue de Nvono Nca.
Alisema umoja huo  unatambua kazi kubwa inayofanywa na wake wa Marais wa Afrika kwa jinsi wanavyowaunga mkono wenza wao kwa  kufanya kazi   ambazo malengo yake makubwa ni  kuwasaidia wanawake, wasichana , watoto na watu ambao wako katika makundi  hatarishi ndani ya jamii.
Akiongea  kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutunukiwa vyeti hivyo Mke wa Rais wa Congo Brazzavile Mama Antoinette N’Guesso  aliwashukuru wake hao wa mabalozi kwa kazi wanayoifanya ya kulitangaza bara la Afrika kuwa ni nchi ya umoja, mshikamano na ukarimu jambo ambalo litaondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kuwa kitu pekee kilichopo barani Afrika ni matatizo.
Wengine waliokabidhiwa vyeti hivyo ni pamoja na  Malkia wa  Swaziland Inkhosikati Zena Seraya Mahlangu , Mke wa Rais wa Madagascar Mama Lalao Rajaonarimampianina, Congo Brazzaville  Mama Antoinette N’Guesso  na  Cameroon  Mama Chantal Biy.
Wake hao wa Marais wameambatana na wenza wao ambao ni Marais wa Afrika wanaohudhuria mkutano wa nne  wa wakuu wa nchi za Afrika na Jumuia ya Ulaya unaofanyika nchini humo.
 
View detail

Tuesday, April 1, 2014

TANZANIA YASAIDIWA BILIONI 6 NA JAPAN

 
01
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akitia saini hati ya makubaliano ya msaada wenye thamani ya ziadi ya bilioni 6 unaolenga kukuza sekta ya kilimo uliotolewa   na Serikali ya Japan  kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda.
02
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akikabidilishana nakala ya makubaliano waliosainina na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) ambayo yanahusu msaada uliotolewa na Serikali ya Japan  kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam. 
03
Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi akikabidilishana nakala za mkataba uliosainiwa na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) leo jijini Dar es salaam. 
04
Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) baada ya Serikali ya Tanzania kusaini mkataba na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam.

Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za Kitanzania ambazo ni sawa na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Misaada (JAICA) .
Kauli hiyo ilitolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea msaada huo  ambao utatumika kukuza sekta ya kilimo na kupunguza umasikini nchini.
Katibu Mkuu Dkt. Likwelile alisema kuwa msaasa huo utatumika kununulia mbolea (UREA) ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia wakulima wadogo wadogo nchini ili kuwaongezea kipato chao.

Katibu Mkuu huyo alisema kuwa msaada huo umekuja muda muafaka ambapo serikali inachukua hutua za makusudi kuinua sekta ya kilimo ambayo inawaajiri watanzania takribani asilimia 74 nchini.
 Aidha, Katibu Mkuu aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaaada huo na kumhakikishia Balozi wa Japan nchini Mh. Masaki Okanda kuwa msaada uliotolewa na Japan kupitia JAICA utatumika kulinganana malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake  Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda alisema kuwa msaada uliotolewa na Serikali yake kupitia JAICA unalenga zaidi sekta ya kilimo na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara na masoko ambayo ndiyo kiini cha ufanisi katika sekta hiyo.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi alisema kuwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Japan ni wa kihistoria ulianzishwa tangu mwakqa 1974 ambapo mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa unanufaika na misaada hiyo katika kuboresha kilimo.
Akimshukuru Katibu Mkuu Likwalile na Balozi wa Japan nchini  Okanda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kayandabila alisema kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na ameahidi kuwa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo chenye tija nchini.
Serikali ya Japan nchini kwa kushikiana na Tanzania katika kusimamaia kilimo inaongozwa na nguzo kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na utawala bora, hali ambayo itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao bora na hivyo kupunguza umasikini nchini.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop