Welcome to our online store Portal

Template Information

Thursday, October 31, 2013

JUA KUPATWA JUMA PILI HII TAREHE 03 NOVEMBA 2013




Tarehe 3 novemba mwaka huu, siku ya Juma pili saa 8:05 mchana mpaka Jua kuchwa, tutakuwa miongoni mwa wachache watakao bahatika kushudia tukio la angani ambalo limewastaajabisha watu tangu zama za kale. Katika nchi chache za Afrika ya kati, katika eneo mwembamba linaloanzia Bahari ya Pasifiki, kukatisha Gaboni, Zaire, kaskazini ya  Uganda, kaskazini ya Kenya karibu na Ziwa la Turkana, Ethiopia na kuishia Somalia, watu wa maeneo hayo watabahatika zaidi kushuhudia Jua likifunikwa kabisa, na kwao mchana utageuka usiku. Kwa upande wetu, nchini Tanzania, tutaona takribani asilimia 70 % ya Jua kufunikwa na kuonyesha Jua likiwa na umbo la hilali kama vile Mwezi mwandamo, linapoangaliwa kwa miwani maaalum ya kuangalizia Jua.


Kupatwa kwa Jua kwa tarehe 3 novemba ni aina maalumu ya kupatwa huko, kunakojulikana kama kupatwa mchanganyiko (Hybrid Eclipse) kwa sababu huanza kama kupatwa kwa pete (Annular Eclipse), ambapo ukingo wa Jua unakuwa haujafunikwa na hivyo kuonekana kama pete. Baada ya muda pete hiyo nayo inafunikwa na kubadilika kuwa kupatwa kamili. Kupatwa kwingine kwa mchanganyiko kuma ule wa Novembar 3 kutatokea tarehe 20 Aprili 2023, katika maeneo ya Asia ya kusini mashariki.


Sisi nchini Tanzania, na takriban bara lote la Afrika (Angalia mchoro wa Afrika), watu wataona kupatwa kwa Jua kwa sehemu asilimia mbali mbali kutegemeana na umbali kutoka mkanda wa kupatwa kamilifu. Hili tukio kubwa kwa vile watu wa bara lote la Afrika watashuhudia tukio hlili kwa pamoja, muda ule  ule.  Kwa hiyo wananchi barani kote Africa wanahamasishwa wangalie tukio hili la maumbili ya kustajabisha na ni maajabu kwa watoto na vijana kuwachocheza wapende sayansi.
Je kupatwa kunatokeaje? Wakati wa  kupatwa kwa Jua, uso wa Jua tunaouona sisi hufunikwaa na Mwezi.  Wakati  huo, Mwezi unakuwa kati ya Dunia na na Jua, kwa hiyo kivuli cha Mwezi huangukia Duniani.  Kutoka angani ungeona kivuli cha Mwezi kinaangukia Dunini (Angalia mchoro wa jiometri unaononesha mistari  ya mionzi inayosababisha kivuli.)
Wakati  wa kupatwa kwa Mwezi (ambalo lilitokea wiki mbili zilizopita, tarehe 19 Oktoba), pia kuna kufunikwa kwa Jua. Lakini wakati huo Dunia inakua kati ya  Jua na Mwazi.  Hivyo kivuli cha Dunia kinaangukia Mwezini na kusababisha kiza katika sura ya Mwezi.
Mwezi huzunguka Dunia kila mwezi.  Kwa hiyo Mwezi waweza kujipanga mstari mmoja na Dunia na Jua kwa namna ambayo Mwezi uko kati ya Jua na Dunia, na kusababishwa kupatwa kwa Jua. Nyakati nyingine Mwezi unaweza kujipanga mstari kwa namna ambayo Dunia ipo kati ya Jua na Mwezi na kusababisha kupatwa kwa Mwezi. 
Kwa vile Mwezi unazunguka Dunia kila mwezi, tungetarajia kutokee kupatwa kwa Mwezi mara moja kwa mwezi, na kupatwa kwa Jua pia mara moja kwa mwezi, yaani tungeshuhudia matukio ya kupatwa mara mbili kila mwezi.  Lakini tunaelewa kuwa katika mwaka mmoja, hali ya kupatwa hutokea tatu au nne tu kila mwaka.  Kuna tatizo gani? 
Dunia inazunguka Jua, na Mwezi unaizunguka Dunia.  Na mizunguko hiyo ni ya uso bapa ambayo imeinamia kiasi kidogo.  Hivyo, mstari wa Jua, Mwezi na Dunia hauwi wa kunyooka, kupatwa hakuwezi kutokea. Kupatwa kunatokea tu wakati Mwezi unapokuwa pale ambapo mizunguko ya Dunia na Mwezi inakatisha. Hii hutokea mara tatu au nne tu kila mwaka na matokeo ni kwamba tunapata matukio mawili hadi manne tu ya kupatwa kila mwaka.
Sababu nyingine ya Jua kuweza kupatwa na Mwezi ni kwamba unapangalia kutoka Duniani, ukubwa wa Jua na Mwezi zinaukubwa uliolingana kabisa. Ukiangalia Jua kwa kutumia miwani maalumu ya kujikinga, utatambua kuwa Jua linaonekana ukubwa sawa kabisa na Mwezi mpevu. Ingawa kipenyo cha Mwezi ni  ndogo, (km3,500), na kile cha Jua ni kikubwa kwa mara mia nne (km. milioni 1.4), vinaonekana ukubwa sawa, kwetu kwa sababu Jua liko umbali wa mara 400 kutoka kwetu. Kwa hiyo ukubwa wao dhahiri ni sawa kabisa.  Jambo hili la ulingano kamili wa Jua na Mwezi kutoka hapa Duniani kwetu, ni  wa kustaajabisha sana na kinavutia wananchi wote.
Ni rahisi kuonyesha kwa vitendo, kwamba kitu kidogo sana kinaweza kufunika kuona kwako kitu kikubwa sana. Kata mduara mdogo kwenye kadibodi na shika mbali kidogo na macho yako. Utaona kwamba mduara mdgogo unaweza kuficha hata jengo zima au mti wote, jinsi ilivyooneshwa kwenye mchoro.

Pia inavutia kuelewa kwa nini kupatwa kwa Jua hutokea wakati wa Mwezi mwandamo tu. Wakati huo, Jua linakuwa nyuma ya Mwezi, ambao upande wake wa giza unatuelekea sisi. Wakati wa kupatwa kwa Jua, upande mweusi wa Mwezi (upande wenye  giza) unakuja mbele ya Jua na kulificha Jua tusilione. Kwa upande mwingine, kupatwa kwa Mwezi, hutokea wakati wa Mwezi mpevu kama ilivyotokea wakati wa kupatwa kwa Mwezi kwa giza jepesi (Penumbral Lunar Eclipse), usiku wa tarehe 19 oktoba 2013. Wakati wa Mwezi mpevu, uso wa Mwezi unaangazwa na Jua kwa ukamilifu na pia linalotuangaza, Duniani upande wa mchana. Fikiria Dunia (yaani sisi) kuwa kati ya Jua na Mwezi.  Utaona kuwa kivuli cha Dunia kinaweza kuangukia kwenye Mwezi na kusababisha kupatwa kwa Mwezi. Aina mbili hizo za kupatwa, mara nyingi, hufuatana moja baada ya nyingine, jinsi ilivyotokea safari hii.  Mwezi ulipatwa tarehe Oktoba 19 na Jua litapatwa wiki mbili baadaye, yaani  tarehe 3, Novemba.
Tumetaja aina mbalimbali za kupatwa kwa Jua: kupatwa kabisa, kupatwa sehemu, kupatwa kwa petu na kupatwa mchanganyiko wa Jua. Kupatwa huku, kunatokea kutegemea na aina ya kivuli cha Mwezi kinachofikia Dunia. 

Kama ni kivuli cha giza zito (lijulikanalo kama umbra), hutokea kupatwa kabisa na mwanga wote wa Jua huzibwa.  Kusema kweli huu ni miongoni mwa mwonekano wa kustaajabisha katika maumbile kwa sababu mchana ghafla hugeuka kuwa usiku, angalau kwa mda mfupi. Huu ni wakati pekee ambapo mtu anaweza kuona anga la juu la Jua, linalojulikana kama Corona, ambalo ni muonekano unaofaa kuona mwenyewe. Wanasanyansi wengi wanatumia fursa ya kupatwa kabisa kwa Jua, kufanya utafiti wa Jua na Corona yake na jinis inavyosababisha mabadiliko katika hali ya  hewa ya Dunia.
Kupatwa kwa Pete, hutokea wakati kivuli mchanganyiko cha Mwezi kinafikia uso wa Dunia. Kinachotokea hasa ni kwamba Mwezi unakuwa mbali zaidi kutoka Duniani, kwa kipenyo chake dhahiri, ni kidogo kuliko kile cha kipenyo dhahiri cha Jua kwa hiyo ukingo wa Jua unaachwa wazi na pete ya mwanga wa Jua inaonekana.
Tarehe 1 Septemba 2016, Tanzania itakuwa kitovu cha tukio la  Dunia wakati kupatwa kwa Jua kwa pete kutapitia Afrika ya kati na kitovu chake kitakuwa kusini mwa Tanzania.  Litakuwa ni tukio kubwa kwa Watanzania  wote, na kila mtu nchini tujiandae kuwapokea watalii Watanzania pamoja na kutoka nchi za nje kuja kushuhudia tukio hili.
Kupatwa tutakaoona siku ya Jumapili Novemba 3, itakuwa ni kupatwa sehemu tu ya Jua. Sehemu ya Jua itafunikwa na Mwezi.  Hakikisha kuwa una miwani maalum ya kuangalizia kupatwa.  Aidha, unaweza kutumia kioo Namba 14 kinachotumiwa na  wanaochomea chuma.  Kwa usalama kamilifu, njia bora zaidi ni kutoliangalia Jua moja kwa moja kwa muda  mrefu.  Jua ni  gimba linalotoa mwanga mkali mno kupita kiasi.
 TAFADHALI USIANGALIE JUA MOJA KWA MOJA, AU KWA DARUBINI - UTAPOFUKA PAPO HAPO.
Kuanzia saa 8:05 mchana, kwa kutumia njia salama ya kuangalia kupatwa kwa Jua, utaona uKingo wa Jua ukianza kufunikwa na Mwezi.  Hali hii itadumu pole pole mpaka saa 9:50 alhasiri wakati kiasi kikubwa cha Jua kitafunikwa. Kwa sehemu za kaskazini ya Tanzania, zaidi ya asilimia 80% ya Jua itafunikwa na mnamo saa 10 jioni wakati watu wa kusini mwa Tanzania wataona asilimia 60% la Jua litakuwa limefunikwa. Jijini Dar es salaam, tunatarajia zaidi ya theluthi mbili za Jua litafunikwa mnamo saa 10 alasiri.   Wakati huo, kwa kutumia miwani maalumu, Jua litaonekana kama vile ni Mwezi mwandamo.

Baada ya kupatwa kwa kiwango cha juu, mnamo saa 10, ukubwa wa  Jua kama Mwezi mwandamo utaongezeka hadi ukingo wa mwisho wa giza utakapotanzuka saa 11:25 jioni. Mabadiliko ya Jua yatatokea pole pole kwa kipindi cha zaidi ya saa 3 kwa hiyo hakuna haja ya kuangalia kupatwa huko mfululizo na waweza kushirikiana kwa urahisi miwani ya kupatwa kati ya watu wengi.
Licha ya kutumia miwani ya kupatwa na kioo cha giza namba 14, unaweza kuangalia jini kupata kunaendelea kupatwa kwa Jua kwa kutumia njia ya mwonekano. Utakuwa umegundua kuwa mwanga wa Jua unapo ingia kwenye kitundu kidogo chochote kwa mfano  katika kipande kikubwa cha kadibodi, utaona mduara wa mwanga ukiangazwa upande wa ndani katika kivuli cha kadibodi.  Mduara huo ni taswira ya Jua, na njia hii inaitwa njia ya tundu ya kuangalia kupatwa kwa Jua. Kwa hiyo wakati Jua linapopatwa sehemu tu, utaona umbo kama Mwezi mwandamo badala ya mduara. Utaweza kufatilia kwa urahisi maendeleo ya kupatwa kwa Jua kwa kutumia njia ya mwonekano. Hata mwanga unaopenya kwenye minyare ya kati ya majani ya miti utaonesha Miezi miandamo mingi sakafuni.
Jiandae kwa fursa hii ya kipekee ya kuona tukio la kusisimua Jumapili hii.  Kwa  maelezo zaidi na taarifa za hivi karibuni, tembelea tovuti: http://www.astronomyintanzania.or.tz
HAKIKISHA KWAMBA UNAKINGA MACHO YAKO KWA MIWANI MAALUM UNAPOANGALIA KUPATWA KWA JUA SIKU YA JUMAPILI 03/09/2013

Na Dkt. N. T. Jiwaji
ntjiwaji@yahoo.com


View detail

Wednesday, October 30, 2013

TANZANIA KUJITOA AFRIKA YA MASHARIKI

Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.
Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo.
Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.
Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya forodha.

Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.
Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.
Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.
View detail

NAFASI ZA KAZI KWA WATANZAIA WOTE WENYE SIFA

Kwa wananchi wote wa tanzania wenye kuona taarifa hii wanaombwa wao au watu wanaowafahamu kuwapa taarifa ya ajira za serikali zilizotolewa. kwa kuona nafasi za kazi fuata Link hii View detail

MAJINA YA WALIOITWA KAZINI (UTUMISHI WA UMA)

Kwa wale walioomba nafasi za kazi ktk taasisi na ofisi mbalimbali za uma na wakafanyiwa usaili majina yao yapo ktk blog hii, kuona majina ya waliochaguliwa fuata Link hii View detail

KAPT KOMBA AJILIPUA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kapteni Mstaafu, John Komba amevunja ukimya na kutamka wazi kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ndiye chaguo lake na atakuwa Rais ajaye uchaguzi wa 2015.
Komba anakuwa mtu wa pili kumtaja Lowassa hadharani kuwa anafaa kwa rais 2015.
Itakumbukwa Mbunge wa Viti Maalumu, Beatrice Shelukindo (CCM) naye alivunja ukimya baada ya kutangaza kumuunga mkono Lowassa kumrithi Rais Kikwete.
Shelukindo alitoa kauli hiyo wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT, kwenye sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa na kuhudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.
Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu jana, Komba ambaye ni Kiongozi wa Kundi la Uhamasishaji cha CCM Tanzania One Theatre (TOT Plus), alisema mtazamo wake kwa mtu anayefaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete ni Lowassa.
Komba aliyeingia kwenye siasa kutokana na msukumo wa mama yake aliyekuwa msaidizi wa Bibi Titi Mohamed, alisema anazo sababu kuu tano za kumkubali Lowassa kuwa Rais na atasimama popote kumtetea.
“Nakuambia Lowassa ndiye anafaa kuwa Rais... unafikiri kuna mwingine. Nina sababu zangu tatu,” alisema Komba na kuhoji:
“Wewe unakwenda kwenye harambee, nani leo hii anaweza kusaidia kuchangia kwa fedha nyingi na zote hizo ni kwa maendeleo yanayokusudiwa kama siyo Lowassa?”
alisema Komba ambaye ni mahiri katika kuinadi CCM, katika kampeni mbalimbali za udiwani, ubunge na urais.Juu ya kuwa atakuwa katika wakati mgumu endapo anayempigia debe hatokuwa, Komba alisema: “Mimi sikwambii ni nani, lakini wapo Mawaziri waliomkana, lakini leo hii wapo kwenye Serikali hii hii ya Rais Kikwete.
“Mimi nasema Lowassa, na kama akipita sawa nitaburudiiika kwelikweli, lakini kama akiteuliwa mwingine, mimi nitakuwa naye...nitamwimbia hadi mwisho. Kazi yangu si unaijua, nitampigia debe kwa kuwa si mtu wa mtu mmoja, ni uteuzi wa wanaCCM ule si wa Komba.” alisema.
Mbali na kumnadi Lowassa, Komba alisifu uimara wa chama chake kuwa kinaimarika siku hadi siku na ndicho kinachotoa viongozi wa kweli na hata wananchi wanakikubali.
Akizungumzia suala la rushwa ndani ya CCM, Komba ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga, alisema kama chama kuna watu wa aina nyingi, kuna wasafi, kuna wachafu lakini wote wako kwenye mstari mmoja.
Alisema kuwa vita ya rushwa ndani ya CCM itamalizika endapo kila kiongozi atasimamia kwenye haki na maadili ya uongozi na pia kutambua wajibu wake ndani ya chama.Komba alijipigia upatu kuwa ameleta maendeleo katika jimbo lake kwani jimbo linatazamika ikilinganisha na miaka ya nyuma kuwa wananchi walikuwa wakiishi maisha ya tabu na kimaskini ilhali wana raslimali za kutosha.
View detail

Monday, October 28, 2013

UKATILI MKUBWA WAFANYWA NA G4S

Kamuni ya ulinzi ya G4S imakanusha madai ya ukatili dhidi ya wafungwa
Wafanyakazi wa jela moja la Afrika Kusini la wahalifu sugu na ambalo linalindwa na kampuni ya ulinzi ya Uingereza G4S , wametuhumiwa kwa kufanya ukatili wa kiwango cha kushtua.
Serikali ya nchi hiyo sasa imeamua kudhibiti ulinzi wa jela hiyo ya Mangaung ya kuanzisha uchunguzi.
Hatua hii inajiri baada ya wafungwa kulalamiika kuwa kupigwa kwa nguvu za umeme na kulazimishwa kudungwa sindano hata hivyo G4S inakanusha madai hayo ikisema kuwa hakuna ushahidi kuwa wafanyikazi wake wanatekeleza vitendo hivyo.
BBC imepata video kutoka katika gereza hilo lenye ulinzi mkali ambapo milio ya nguvu za umeme inasikika .Inaonyesha pia mfungwa mmoja akikataa kupewa matibabu
Watafiti wa Wits Justice Project kutoka chuo kikuu cha Wits mjini Johannesburg wanasema kuwa wamekusanya ripoti za wafungwa karibu 30 kuhusiana na kupigwa kwa nguvu za umeme na kuchapwa katika utafiti wao wa mwaka mmoja
Mwandishi wa BBC Andrew Harding anasema kuwa serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa hali katika gereza hilo lenye ulinzi mkali ya Mangaung ni ya kushtua sana
“Wengine walisema kuwa walizirai waliposhindwa kustahimili uchungu wa nguvu za umeme,” alisema Ruth Hopkins ,mwanahabari wa mradi wa Wits Justice
Alisema kuwa wafungwa walilalamika kuhusu kuvunjika kwa mikono na miguu na majeraha mengine makuu.
Mmoja wa aliyekuwa mfungwa kwa gereza hilo aliambia BBC kuwa nguvu za umeme zilitumika kuwatesa ,vilevile askari aliyefutwa kazi aliongezea kuwa wafungwa walimwagiliwa maji ili kuongeza uzito wa nguvu za umeme.

“Madai yoyote ya yakiripotiwa kwetu ,ambayo ni ya kesi ya kipekee inatubidi kuyashughulikia vilivyo”
Kulingana na mwandishi wa BBC wa Afrika Andrew Harding ,wakili wa baadhi ya wafungwa hao alishutumu tabia ya wafanyikazi katika gereza hilo kufanya ukatili bila kujali.
G4S hata hivyo imedai kuwa kuwepo na purukushani katika gereza hilo ni kwa sababu ya mzozo wa ajira. Zaidi ya askari 300 walifutwa kazi mwezi huu baada ya kushiriki mgomo
Nontsikelelo Jolingana,ambaye ni kamishna wa vitengo vya marekebisho aliambia BBC kuwa kitengo chake kimeanza uchunguzi rasmi kuhisiana na madai hayo .

Shirika la magereza ya Afrika Kusini mwezi jana lilitangaza kuwa wanachukua wanadhibiti ulinzi katika gereza hilo lililo katika mkoa wa Central Free State kwa muda baada ya shirika la kibinafsi la usalama kushindwa kulisimamia vyema gereza hilo.
Andy Baker, ambaye ni mkuu wa G4S Afrika alisema kuwa kuwadunga wafungwa sindano si jukumu la G4S bali ni la wafanyikazi wa afya.
Alipoulizwa kuhusu madai ya kutumia nguvu za umeme na kupigwa didhi ya wafungwa alisema kuwa “hakujawahi kutokea jambo hilo”.
Habari kwa hisani ya BBC
View detail

Friday, October 25, 2013

SAKATA LA GESI MENGI AVUNJA UKIMYA

Dar es Salaam. Suala la gesi lilizua balaa jana wakati wa mkutano wa wadau wa sekta hiyo baada ya malumbano makali kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Mwenyekiti wa Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF), Dk Reginald Mengi.
Maswi na Mengi walitofautiana juu ya suala la nafasi ya wawekezaji wazawa kwenye sekta hiyo ya gesi katika kongamano la pili la wadau wa mafuta na gesi jana jijini Dar es Salaam.
Malumbano hayo yalichochewa zaidi na kauli iliyotolewa juzi na Waziri wa Nishani na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye alisema kuwa wazawa wana uwezo mdogo wa kuwekeza katika sekta hiyo.
Mengi arusha kombora
Mengi ndiye aliyeanza mashambulizi pale alipotaka wazawa wapewe kipaumbele kwenye uvunaji wa mafuta na gesi.
“Tunaambiwa sisi hatuna fedha. Eti hela zetu ni kwa ajili ya kufanyia biashara ya matunda. Lakini tunayo ardhi, Tanzania siyo nchi maskini, gesi ni mtaji wetu, tuweke mkakati wa kugawana hii rasilimali,” alisema Mengi na kuongeza;
“Huku ni kuwa maskini wa fikra na tutakuja kuulizwa na Mwenyezi Mungu. Kama Serikali haina sera itauzaje rasilimali zetu kwa wageni? Tusingependa kuyazungumza haya hadharani, lakini tunasema tu. Mtu mwenye hekima pale wizarani wa kutusikiliza ni Maswi peke yake.” Mengi alisema anataka kuona Serikali ikitumia mfumo wa taifa la Nigeria kwa kutoa kipaumbele kwa wazawa.
“Mimi katika masuala ya uwekezaji kwa kweli `role model’ (kivutio) ni nchi ya Nigeria,” alisema Mengi.
Mwakilishi wa taasisi
za dini ashindilia
Baada ya Mengi kukaa, alisimama Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Jamii, Mchungaji William Mwamalanga alisema Serikali inatakiwa kukubaliana na hoja za Watanzania katika uwekezaji wa sekta hiyo.
Mchungaji Mwamalanga aliongeza kuwa huu siyo wakati wa kuendelea kuwaachia wawekezaji hatua zote katika rasilimali ya Tanzania.
“Lazima tujifunze kwa mataifa kama Nigeria, serikali yao imetoa nafasi ya mwananchi kusimamia, yaani mwekezaji akiingia lazima apitie kwa mwekezaji wa ndani kabla ya kufanya mazungumzo na serikali. Kwa nini tusifanye hivyo pia? “alihoji Mchungaji Mwamalanga.
Mbali na hilo Mchungaji Mwamalanga alisema Serikali inatakiwa kukiri dhambi ya kuingia mikataba bila kuwapo kwa sera ya gesi.
Maswi ajibu mapigo
Baada ya Mengi na wajumbe wengine kutoa maoni ya kuilaumu Serikali, Maswi alitakiwa kutoa maelezo ya Serikali kuhusiana na suala hilo.
Maswi alionyesha wazi alikuwa amepandwa na jazba kufuatia maoni ya kuiponda Serikali na hakuchelewa kuanza kuwakosoa Mengi na wadau wengine.
“Katika andiko letu tumeandika, nawahimiza mkalinunue, tumewagusia wazawa ambao watahusishwa katika ununuzi wa vitalu. Hakuna aliyesema kuwa sekta binafsi haitashirikishwa,” alisema Maswi huku akifoka.
Maswi alisema kuna mambo mengi ambayo Watanzania wanayo fursa ya kushiriki katika uwekezaji wa sekta hiyo na siyo kukaa majukwaani na kuzungumza kwa unafiki.
Aidha, aliongeza kuwa mpaka sasa hajaona kampuni yenye uwezo mkubwa hapa nchini katika ushiriki wa moja kwa moja katika uwekezaji wa sekta hiyo.
“Tusijidanganye kwa vikampuni vidogovidogo tulivyonavyo, tukadhani kama vinaweza kuingia kwenye ushindani wa moja kwa moja. Vikampuni vyenyewe vimejaa rushwa tu za kuhonga, hakuna lolote tuache ubabaishaji, “ alisema Maswi. Aliukosoa pia mtindo wa uwekezaji wa Nigeria ambao Mengi ameupendekeza:
“Mengi kaka yangu, hakuna suala la mjomba katika masuala ya uwekezaji. Huo mtindo wa Nigeria siyo mzuri, huwezi kuwapa watu wachache rasilimali wakati wengi wakiwa kwenye umaskini. Nigeria imejaa vurugu na hatuwezi kuichukulia kama mfano mzuri,” alisema Maswi na kuongeza:
“Jukumu letu kama wizara na kila ninapokutana na ninyi, nakutana kama Katibu Mkuu, siyo Maswi. Lengo letu ni kuwaeleza kinachoendelea na jinsi ya kuwawezesha wazawa.”
Akijibu hoja ya Mchungaji Mwamalanga, Maswi aliwataka viongozi hao kushirikiana na Serikali badala ya kuinyooshea kidole.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iko tayari kukutana na kundi lolote. Mkitaka tuonane, leteni barua tu. Tuko tayari na hatufichi kitu,” alisema na kuongeza: “Tatizo la nchi yetu watu ni kulalamika tu, fanyeni kazi... Mkitusaidia maaskofu, tutatoka hapa tulipo, siyo kutunyooshea tu vidole.
Maaskofu wenyewe wanakula rushwa, wanafanya vitu vya ajabu, mbona sisi hatuwanyooshei? Au tuwataje? Kwa sababu msione tu Serikali ni watu wabaya, `no, let’s work as a team’,” alisema Maswi.
Aliendelea kusisitiza kuwa fursa ya uwekezaji ipo kwa watu wote bila kujali wa ndani au wa nje.
“Hakuna mtu anayekuja hapa ambaye ni mjomba wenu. Sasa kama nyie mnakaa nyuma nyuma, hebu muwekeze basi.
Hivyo vitalu tumetoa, nani ametaka `document’ tumemkatalia? Watu wanakuja wanaleta hela, sasa tuzikatae?” Kuhusu sera na sheria ya gesi na mafuta, Maswi alisema sheria ipo ila sera itakamilika ifikapo Mei mwakani.
“Nawaahidi hadi mwisho wa mwaka huu tutakuwa na sera ya wazawa, hivyo nawaomba mshiriki kutoa maoni. Kama tunayo sheria tangu mwaka 1970 na 1980 tunataka nini tena? Tunataka sera au sheria? Nadhani sheria ni kubwa zaidi, huwezi kwenda kinyume na sheria. Hata hivyo, sera tunayo tangu Oktoba mwaka huu, lakini bado iko kwenye mchakato. Itakamilika ifikapo Mei, 2014,” alisema Maswi.
View detail

Wananchi Madagascar wajitokeza kumchagua Rais


Harakati za kampeni kabla ya uchaguzi wa Rais Madagascar
Wananchi wa Madagascar wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini humo tangu yalipofanyika mapinduzi yaliyoungwa mkono na jeshi miaka minne iliyopita.
Wagombea 33 wanawania urais wa nchi hiyo katika uchaguzi huo, ambao umeahirishwa mara tatu mwaka huu.
Wagombea wawili wanaopewa nafasi ya kushinda, wanaahidi kujenga upya uchumi wa Madagascar baada ya miaka ya mgogoro wa kisiasa na kiuchumi.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, zaidi ya asilimia 92% ya wananchi milioni 21 wa Madagascar wanaishi chini ya dola mbili kwa siku.
Rais Andry Rajoelina alimng'oa madarakani Marc Ravalomanana mwaka 2009, na kulitumbukiza taifa hilo katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kusababisha nchi hiyo kutengwa na jumuiya ya kimataifa na kunyimwa misaada kutoka nje. View detail

Thursday, October 24, 2013

ASKARI WAUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA


Wanajeshi wa UN walichukua usukani kutoka kwa wanajeshi wa Ufaransa waliopambana na wapiganaji wa kiiisilamu kaskazini mwa Mali
Wanajeshi wawili wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, wameuawa na wengine sita kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la kujitoa mhanga Kaskazini mwa Mali.
Raia wa kawaida pia walifariki kwenye shambulizi lengine la bomu wakati mshambuliaji alipoingiza gari lake lenye mabomu katika eneo la kukagua magari kabla ya kujilipua mwenyewe.
Mtoto mmoja aliuawa na mwengine kujeruhiwa kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la Reuters likinukuu maafisa wa serikali.
Umoja wa Mataifa una takriban wanajeshi 6,000 nchini Mali, walioko huko kupambana na wapiganaji wa kiisilamu.
Katibu mkuu wa umoja huo Ban Ki-moon alisema kuwa mashambulizi hayo hayataathiri kabisa lengo la UN kuunga mkono kurejeshwa kwa utulivu na usalama pamoja na amani nchini Mali.
Baraza la usalama la UN limelaani mashambulizi hayo kwa kauli nzito sana.
Ilielezea kusikitishwa pamoja na kuwatakia pole jamaa na marafiki za wanajeshi waliouawa pamoja na serikali ya Mali na Chad.
Baraza huilo limesema kuwa waliohusika lazima watachukuliwa hatua kali na imeitaka Mali kuchunguza mauaji hayo na kuwaadhibu waliohusika nayo.
Wizara ya ulinzi ilisema kuwa washambuliaji wanne walihusika na mashambulizi hayo na wote walifariki.
Mwakilishi wa UN nchini Mali, Bert Koenders, mapema mwezi huu alitoa wito wa kupelekwa kwa wanajeshi zaidi baada ya kuongezeka kwa visa vya mashambulizi ya mabomu na makombora.
Wanajeshi wa Ufaransa, walikomboa eneo la Kaskazini mwa Mali pamoja na miji mingine kutoka kwa wanamgambo baada ya kuanzisha operesheni dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Jukumu la usalama hata hivyo walilikabidhi kwa Umoja wa Mataifa mwezi Julai.
View detail

Tuesday, October 22, 2013

WAHITAJI KUSOMESHWA BURE DEGREE YAKO?

Fursa muhimu kwa kila msichana wa kiafrika anaehitaji kusoma elimu ya juu kwa fani mbalimbali, Nafasi ni nyingi na kila mwenye sifa anastahili kuomba, kwa kujua namna ya kuomba udhamini Bofya hapa View detail

Monday, October 21, 2013

UKWELI KUHUSU TUKIO LA UFOO SARO

Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye hivi karibuni alikumbwa na madhila ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na mzazi mwenzie, ameanza kufunguka kidogo kidogo na kueleza kwa kina jinsi tukio zima lilivyotokea.

Akizungumza kwa sauti ndogo na taratibu na gazeti hili kando ya kitanda alicholazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mwanahabari huyo alieleza kushangazwa na ujasiri na nguvu za aina yake ambazo zilimwezesha kutambaa na kujiburuza hadi eneo la karibu ya barabara ili kuomba msaada wa kukimbizwa hospitali.

Ufoo ambaye alionyesha dhahiri kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazozingira tukio lake, alisema tayari alikuwa amewahakikishia polisi waliofika kumjulia hali hospitalini hapo kwamba alikuwa akisubiri afya yake iimarike kabla hajaeleza kwa kina kila anachokijua kuhusiana na tukio hilo.

“Alifika hapa kunijulia hali na kuangalia maendeleo yangu afande Msangi na nikasema nitakuwa tayari kueleza kila ninachokijua baada ya afya yangu kuimarika. Nasikitika kuna watu wanasema mambo wakifikia hatua ya kutaka kuonekana wananifahamu vizuri kuliko hata ninavyojifahamu mwenyewe,” alisema akionyesha kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazoripotiwa kuhusu sakata lake.


Ufoo ambaye alifikishwa hospitalini hapo Jumapili ya wiki iliyopita kutokana na kujeruhiwa kwa risasi na mwanaume aliyezaa naye mtoto mmoja alisema anamshukuru sana Mungu kwa uzima alionao sambamba na kuelezwa kupata faraja kubwa na kutiwa moyo na mwajiri wake, ndugu, jamaa na marafiki.   

Mwanahabari huyo ambaye bado yuko chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi mwilini mwake siku chache zilizopita, amelazwa katika chumba cha peke yake ambacho ingawa kina seti ya televisheni alisema alikuwa haruhusiwi kuiangalia kwa ushauri na maelekezo ya madaktari.

Huku akionekana wa chini ya uangalizi mwingine wa karibu na wa kudumu wa muuguzi ambaye muda wote wa mazungumzo haya alionekana kuwapo katika chumba hicho, Ufoo alisema alikuwa ana mapenzi makubwa kwa mzazi mwenzake huyo ambaye alipoteza maisha katika tukio hilo.

“Nilimpenda sana Antheri. Alikuwa kijana mtaratibu na mpole sana. Najua kile kilichotokea ni shetani tu na binafsi nilishasamehe alfajiri ile ile baada ya tukio lile,” alieleza Ufoo ambaye pia alimpoteza mama yake mzazi katika mkasa huo.


Ufoo ambaye mara kadhaa katika mazungumzo na gazeti hili alionekana kukunja uso akiashiria kupata maumivu, alionyesha eneo la chini ya bega katika mkono wake wa kulia lililofungwa na bandeji ambalo alisema ndipo alipopigwa risasi ya kwanza wakati akigeuka na kujaribu kuepuka mauti muda mfupi baada ya Antheri kumfyatulia risasi zilizomkuta mama yake mzazi.

Akijaribu kuvuta kumbukumbu ya tukio lilivyoanza, Ufoo alisema mzazi mwenzake huyo alifika nyumbani kwake akitokea Sudan alikokuwa akifanya kazi usiku huo huo wa tukio na akamtaka kwenda kwa mama yake (Ufoo) eneo la Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Kabla ya kufika Kibamba na kwa sababu ambazo Ufoo hakuzieleza, alimkariri mzazi mwenzake huyo akisema alikuwa amefikia uamuzi wa kujiua yeye na mtoto wao.

“Hata sijui ni nini kilitokea. Wakati tukitoka nyumbani Antheri alianza kwa kuniambia kwamba alikuwa amepanga kujiua yeye na mtoto wetu,” alisema Ufoo kabla ya kukaa kimya kwa sekunde kadhaa na kuendelea na simulizi yake ya kusikitisha.

Akiwa na sura ya ujasiri, Ufoo anasema pamoja na kumwambia maneno hayo bado Mushi alimsisitiza kwamba waende kwa mama yake (Ufoo) baadae warudi kumchukua mtoto wao japo Ufoo hakusema walitaka kwenda wapi baada ya hapo.

Alisema walipofika nyumbani kwa mama yake walikwenda moja kwa moja sebuleni na wakiwa wamekaa kwenye makochi baada ya salamu za hapa na pale ghafla Mushi akasimama akamwambia mama yake Ufoo kwamba; “Mama nimeishafanya maamuzi” 

Kwa mujibu wa maelezo ya Ufoo, baada ya Mushi kutamka maneno hayo ghafla akaingiza mkono nyuma ya suruali  alikokuwa ameweka bastola  yake na kisha akaichomoa.

Katika maelezo yake Ufoo alisema baada ya kuichomoa bastola hiyo mama yake naye alisimama na kwenda kujaribu kumpokonya, kitendo hicho kilimfanya amiminiwe risasi mfululizo.

Alisema kuona hivyo aliamua kukimbia kuelekea jikoni ambapo Mushi alimuona na kuanza kumiminia risasi ambayo moja ilimpata eneo la mkono wa kulia ambayo ilitokezea mbele na kuchana titi la kulia.

Kwa mujibu wa Ufoo jeraha hilo halikumfanya akate tamaa ya kunusuru maisha yake kwani alijaribu kukimbia ingawa Antheri alifyatua risasi nyingine kadhaa ambazo zilimpata juu kidogo ya mgongo na kutokea tumboni ambazo zilisababisha aanguke chini

Akiendelea kusimulia, anasema ingawa alikuwa akivuja damu nyingi, na huku akijiburuza ardhini, Ufoo alisema wakati akitambaa aligeuka nyuma na akamuona Antheri akijielekeza bastola eneo la kidevu na alipofyatua risasi alianguka chini.

“Nikiwa chini nilimuona Antheri akijipiga risasi kidevuni na akaanguka chini, sikujua kilichofuata baada ya hapo kwani niliendelea kujiburuza ili kuokoa maisha yangu,” alisema Ufoo 


“Nyumbani kwetu, pale Kibamba si mbali sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”.

Anasema dada yule alimpa khanga akajifunga na aliposogea barabarani alikutana na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja.

“Nilipoona kuna gari linapita nikainuka kuomba msaada. Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha nikamweleza kwamba nilikuwa nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake anikimbize hadi katika hospitali ya Tumbi na kwamba akifika pale tu aniache mlangoni.

“Si rahisi kuamini, yule mama alikataa kunisaidia akisema alikuwa akiwahi sehemu kumchukua mzazi. Sina la kusema niliamua kumsamehe tu yule mama ingawa niliumia sana,” alisema Ufoo.

Alisema muda mfupi tu baadaye alitokea kijana aliyekuwa na pikipiki, maarufu kwa jina la bodaboda ambaye alimuomba msaada wa kumkimbiza hospitali ya Tumbi na akakubali.

“Yule kijana aliniuliza iwapo nilikuwa ninao uwezo wa kujishikilia vizuri na niliposema nitaweza akanisaidia kupanda katika bodaboda.

“Wakati huo nilikuwa naona kama tumbo linazidi kujaa. Nikiwa kwenye pikipiki kuna wakati nilikuwa nikihisi kwamba naweza nikaishiwa nguvu na kuanguka katika barabara na kisha kupitiwa na gari na kupoteza maisha. Lakini nilipata ujasiri na kujishikilia,” alieleza kwa sauti ya chini.

Alisema anakumbuka wakati walipofika eneo la Kibaha ilipo mizani ya kupima uzito wa magari makubwa walikuta barabara ikiwa imejaa magari na yeye alimuomba dereva huyo wa bodaboda kupita hata nje ya barabara eneo la nyasi ili kumwahisha hospitalini jambo ambalo kijana yule alilifanya. 

“Nilipofika eneo la mapokezi pale Tumbi nilimueleza muuguzi niliyemkuta kwamba nilikuwa nimejeruhiwa kwa risasi na nikamuomba asaidie kuokoa maisha yangu. Yule nesi alisita akitaka kwanza kupata kibali cha polisi (PF3) lakini nikaumuomba apigiwe simu, Kaimu Mganga Mkuu wa Tumbi, Dk. Dattan ambaye tunafahamiana”

“Baada ya muda mfupi Dk. Dattan alifika na nikamweleza yaliyonipata na mara moja nikaanza kuhudumiwa kwa kuniwekea dripu, na nikamsikia akiwaeleza wauguzi kwamba isingekuwa busara kwa hali niliyonayo kama wangeanza kuchukua picha za X-ray kwani hatua hizo zingeweza kusababisha kupoteza maisha,” alieleza akikumbuka yaliyojiri hapo Tumbi.

Kwa mujibu wa Ufoo, akiwa bado ana fahamu alimsikia daktari aliyekuwa akimhudumia akiomba msaada wa gari la kubeba wagonjwa ili limchukue na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wito ambao ulijibiwa kwa maelezo kwamba lilikuwa halina mafuta.

Majibu hayo kwa mujibu wa Ufoo, yalisababisha daktari huyo aombe kuletewa gari la wagonjwa la wagonjwa maarufu (VIP) ambalo lililitwa na muda mfupi baadaye akapakizwa tayari kwa safari ya kukimbizwa Muhimbili.

Alisema wakati akikimbizwa Muhimbili anakumbuka namna alivyokuwa akipatwa na maumivu makali wakati wote gari ile ya wagonjwa ilipokuwa ikipanda matuta ya barabarani na kuna nyakati alikuwa akihisi kupoteza pumzi na kuishiwa nguvu.

View detail

MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA AFUKUZWA KAZI

  
Ni mwanamama Gladys Shollei ambaye alikuwa  Msajili Mkuu wa Mahakama ya Kenya.
Nairobi. Msajili Mkuu wa Mahakama ya Kenya, Gladys Shollei amefukuzwa kazi kwa madai ya utovu wa nidhamu na kuwadharau makamishna wa Tume inayosimamia idara hiyo (JSC).
Shollei ndiye aliyemwapisha Rais Uhuru Kenyatta alipoingia madarakani mwaka huu.
Kwenye taarifa ya uamuzi huo iliyosomwa na Jaji Mkuu Willy Mutunga mwishoni mwa wiki, JSC ilitoa sababu tano za kumsimamisha kazi Shollei, ambapo msajili huyo alishutumiwa kwa kukosa maadili.
“Baada ya kusoma madai yote yaliyomkabili msajili mkuu wa mahakama na baada ya kusoma majibu yake, ikizingatiwa kwamba aliamua kujitokeza mbele ya tume, tumeamua kwa pamoja kumsimamisha kazi mara moja,” alisema Jaji Mutunga.
Kwa hatua hiyo, Shollei anakuwa msajili mkuu wa Mahakama wa kwanza kufutwa kazi tangu Idara ya Mahakama ifanyiwe marekebisho ili kuafiki matakwa ya Katiba ya sasa.
Aidha, ni ofisa wa pili wa ngazi ya juu kwenye idara hiyo kupigwa kalamu, baada ya aliyekuwa Naibu Jaji Mkuu, Nancy Baraza kufutwa mwaka jana.
Akielezea uamuzi huo, Jaji Mutunga alitaja ukosefu wa nidhamu, ukiukaji wa kanuni za kazi za maofisa wa mahakama, ukiukaji wa sura ya sita ya Katiba inayohusu maadili na kukaidi maagizo ya wakubwa wake, kama sababu zilizosababisha JSC kumsimamisha kazi Shollei.
“Kutokana na uzito wa masuala yaliyosababisha kusimishwa kazi kwa Shollei, JSC inaialika Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) ifanye uchunguzi wa kina kuhusu masuala haya,” alisema Jaji Mutunga.
“Madai yaliyotolewa kumhusu Shollei ni mazito sana. Pesa zinazohusishwa katika madai hayo ni Sh2.207 bilioni. Amekubali madai 33 ambapo Sh1.7 bilioni pesa za walipa ushuru ziko katika hatari ya kupotea. Amekataa madai 38 ambayo yanafikia Sh250 milioni ilhali majibu yake kuhusu Sh361 milioni yanakanganya,” alisema.
Jaji Mutunga alisema kuwa JSC imeweka madai yote yanayomkabili Shollei, majibu yake na matokeo ya uchunguzi uliofanywa na JSC katika tovuti yake.
Mwezi uliopita, Shollei aliiandikia barua JSC akiifahamisha kwamba yuko tayari kufika mbele yake kuanzia Oktoba 15, kujibu madai dhidi yake.
View detail

Friday, October 18, 2013

MENO YA TEMBO TANI MBILI YAKAMATWA

Shehena ya meno ya tembo yanaswa Uganda

Maafisa nchini Uganda wamekamata shehena meno ya tembo yenye uzito wa tani mbili, ambacho ni kiwango kikubwa kukamatwa kwa miaka mingi iliyopita.
Chama cha Wanyama Pori nchini Uganda kimesema meno yapatayo 832 yenye thamani ya dola milioni 6.7 yamekamatwa.
Wataalamu wanasema baadhi ya meno hayo yanaaminika yametokana na tembo waliouawa na majangili nje ya nchi ya Uganda.
Kuna mahitaji ya meno ya tembo kutoka barani Afrika kwenda nchi Asia kwa ajili ya kutengeneza mapambo.
Meno hayo ya tembo yalikuwa yakielekea kwenda kusafirishwa katika bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Baadhi ya meno hayo yalikuwa yamekatwa vipande vipande na kufunikwa na chupa za plastiki kwenye makreti na kubandikwa maandishi kuonyesha kwamba ni bidhaa zinazokwenda kuchakatwa (recycling).
Chama hicho cha Wanyama pori kimemwambia mwandishi wa habari wa azizicompdoc.blogspot.com kuwa Uganda imeanza kutumiwa na majangili kama njia ya kupitisha bidhaa za wanyamapori kutoka nchi za Sudan Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
View detail

SAUDIA YAITUNISHIA MISULI UN


Nchi ya Saudi Arabia imekataa nafasi iliyopewa na baraza la usalama la umoja wa mataifa kuwa mwanachama asiye wa kudumu, huku ikituhumu baraza hilo kwa mapendeleo.
Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo , alisema kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa kufanyiwa mageuzi mwanzo.
Aliongeza kusema kwamba baraza la usalama limefeli katika majukumu yake kuhusu Syria pamoja na katika mizozo mingine kote duniani.
Awali, Saudi Arabia iliwahi kuelezea uchungu wake kuhusu jamii ya kimataifa kukosa kutatua mzozo wa Syria, ambako inaunga mkono waasi dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Asaad.
Kwa kawaida huwa kuna ushindani mkali miongoni mwa nchi kutaka moja ya nafasi kumi zisizo za kudumu katika baraza hilo ambazo hushikiliwa na nchi tofauti kwa awamu kwa muda wa miaka miwili, katika baraza hili linalosimamia maswala ya usalama duniani.
Lakini Saudi Arabia imeamua kutumia nafasi hii kuelezea pingamizi zake kuhusu baraza hilo.
Hii ni mara ya pili kwa Saudi Arabia kuelezea hisia zake kuhusu swala kama hili.
Mapema mwezi huu, waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, aligoma kutoa hotuba yake katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuelezea ,malalamiko yake kama hayo tu.
Bila shaka hatua ya Saudia imewashangaza wengi lakini ikiwa itaishinikiza kufanya mageuzi, haijulikani kama yatafanyika mara moja.
Hatua hii imekuja saa chache baada ya Saudia kuteuliwa kwa mara ya kwanza kuchukua nafasi hiyo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.
View detail

Thursday, October 17, 2013

WANAJESHI WA UN MALI WAHITAJI MSAADA


Ndege ya UN nchini Mali
Umoja wamataifa umeomba usaidizi wa vifaa kuwawezesha wanajeshi wake wa amani nchini Mali kushika doria.
Kikosi hicho cha UN kilianza kulinda amani nchini Mali mwezi Julai , na kina chini ya nusu ya wanajeshi 12,000 wanaohitajika kushika doria
Mjumbe maalum wa UN nchini Mali, Bert Koenders, amesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni yamekuwa dalili ya changamoto zinazowakumba wanajeshi hao.
Aliongeza kuwa kikosi hicho kinachojulikana kama Minusma, kinahitaji rasilimali zaidi ili kuweze kudhibiti hali Kasakazini mwa nchi.
Wanajeshi wa Ufaransaka , waliongoza operesheni dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu na kuwaondosha kutoka katika eneo hilo.
Uchaguzi wa Urais ulifanyika mwezi Julai lakini wapiganaji hao wakaanza tena kufanya mashambulizi Kaskazini mwa nchi ambako kundi linalotaka kujitawala la Tuareg pamoja na wapiganaji wengine wamekitaka kambi.
Lakini Bert Koenders, anasema kuwa tisho la usalama linasalia kuwa changamoto kubwa.
Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alishambulia mji wa Timbuktu tarehe 28 Septemba huku wapiganaji wa kiisilamu nao wakilipiza mashambulizi hayo kwa kurusha makombora.
Kikosi cha kulinda amani cha UN kilipata pigo jengine mwezi Agosti baada ya idadi nyengine kubwa ya wanajeshi wa Nigeria kurejea nyumbani kupambana na wanamgambo wa Boko Haram.
Hatua hii iliwaacha wanajeshi wa UN na chini ya wanajeshi elfu sita. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi wanajeshi 12,640 ifikapo mwezi Disemba.
UN inatarajiwa kuwapeleka wanajeshi wengine huko kuchukua nafasi ya wanajeshi wa Ufaransa waliorejea nyumbani baada ya kuingilia kati mgogoro huo wapiganaji walipotishia kuvamia mji mkuu wa Mali Bamako mwezi Januari.
Wapiganaji hao wenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeeda walidhibiti Kaskazini mwa Mali, ikiwemo miji mingine mikubwa ya Gao, Kidal na Timbuktu, baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka 2012.
View detail

Tuesday, October 15, 2013

AU YAITUNISHIA MISULI ICC

 
Rais Kenyatta akiwa katika mahakama ya ICC.
Rais Kenyatta anakabiliwa na kesi inayoanza kusikilizwa mwezi Novemba.
Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika Ehiopia umetaka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC) huko The Hague icheleweshe kesi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, iliyopangwa kuanza kusikilizwa Novemba mwaka huu.
AU pia wamekubaliana azimio linaloeleza kuwa hakuna kiongozi mkuu wa taifa la Afrika aliyeko madarakani atakayefikishwa katika mahakama hiyo.
Wakati viongozi wa Kenya na Sudan wakikabiliwa na kesi huko ICC, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuwa mahakama hiyo inafanya upendeleo na kuwaonea kwa makusudi.
AU ilijadili uwezekano wa nchi wanachama kujitoa, lakini wazo hilo halikuungwa mkono kiasi cha kutosha.
Wanasiasa na wanadiplomasia waandamizi akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan wamekosoa mpango wa kujitoa kutoka ICC.

Viongozi hao wa AU, waliokutana Addis Ababa, walikubaliana kuwawekea kinga ya kutoshitakiwa kiongozi yoyote wa taifa la Afrika.
Pia wameitaka Kenya iandike barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiga kuomba ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama ya ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya jinai.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop