Welcome to our online store Portal

Template Information

Wednesday, June 25, 2014

SISTA WA KANISA KATOLIKI APIGWA RISASI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Wananchi wakiangalia sehemu ambayo majambazi walimpiga risasi Sista Clencensia Kapuli Ubungo, Riverside, Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga 

Majambazi wamemuua kwa risasi Sista wa Kanisa Katoliki Clencensia Kapuli (50) na kupora kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakijajulikana.
Pia, katika tukio hilo lililotokea jana saa nane mchana eneo la Riverside, Ubungo, Dar es Salaam, dereva aliyekuwa akimwendesha Sista Kapuli, Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.
Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mwenyeheri Anwarite, Makoka Jijini Dar es Salaam alikuwa mhasibu wa parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura aliyefika katika Kituo cha Polisi Urafiki kufuatilia tukio hilo alisema Sista Kapuli na sista mwenzake wakiwa katika gari aina ya Toyota Hilux, walikuwa wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha na walipita Riverside ndipo walipopatwa na mkasa huo.
“Bado hatujajua ni kiasi gani cha fedha kimechukuliwa kwa kuwa Sista Kapuli ndiye alikuwa mhasibu na ndiye aliyekwenda kuchukua fedha hizo, subirini tutakapokwenda benki kuuliza ni kiasi gani cha fedha alichukua na tutawajuza,” alisema Wambura.
Kamanda huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ukisubiri taratibu za mazishi.
Shuhuda wa tukio hilo, Gadi Kinyamagolo alisema masista hao walikwenda Riverside kununua mchele katika moja ya maduka ya jumla.
“Mara baada ya kumaliza kununua mchele kama kilo 10 hivi walipanda katika gari wakiwa wawili na kabla ya kuondoka zilifika pikipiki mbili zikiwa na watu wanne, zikasimamisha gari hilo huku mmoja akiwa amevalia kininja na mwingine aliyevaa kawaida, wote wakiwa na silaha. Wengine wawili walibaki kwenye pikipiki.
“Kisha nikaona wanapasua kioo cha nyuma ambapo kulikuwa na sista mmoja na mwingine alikuwa mbele, wote wakiwa na mikoba ambayo majambazi hao waliiomba,” alisema Kinyamagoro na kuongeza:
“Walianza kuwaambia tupe mikoba huku majambazi hao mmoja akiwa amesimama upande wa dereva na mwingine upande wa pili wa gari alipokuwa sista aliyeuawa lakini masista wale hawakutoa mikoba hiyo.”
Kinyamagoro alisema: “Baada ya mabishano, sista aliyekuwa nyuma alifungua mlango na kukimbilia katika duka walilonunua mchele na yule aliyekuwa mbele alipofungua mlango akitaka kukimbia alipigwa risasi shingoni na kutokea upande wa pili na kuanguka nje ya gari.
“Baada ya tukio hilo majambazi hayo yalichukua mikoba miwili na kuondoka nayo. Kwa kuwa mimi nilikuwa karibu nililala chini na eneo hili lilikuwa kimya, watu walikimbia na wengine tulilala tukaacha wafanye kazi yao.”

Shahidi mwingine, Saidi Juma alisema: “Wakati majambazi hao wakiondoka palikuwa na watu wawili waliovalia sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakipita eneo hilo, waliulizwa na majambazi wanafanya nini huku wakiwa wameonyeshwa bunduki. Walinyoosha mikono juu na kuachwa, kisha majambazi wakapanda pikipiki zao na kutokomea.
“Wakati majambazi wakiondoka watu hao waliruka na kulala mtaroni kukwepa kupigwa risasi. Majambazi walipofika hapo mbele (mbele kidogo ya eneo la tukio), walimpiga risasi muuza machungwa na kumjeruhi begani.”
View detail

Tuesday, June 24, 2014

POLISI WATANGAZA HALI YA HATARI KUHUSU NGOMA YA KIGODORO

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, jana. Picha na Venance Nestory 

Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuanzishwa kwa operesheni maalumu ya kuwasaka wasanii wa ngoma wanaocheza wakiwa uchi maarufu kama kigodoro na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Pia, litafanya operesheni ya kuwasaka madereva wa bodaboda, bajaji na baiskeli za matairi matatu wasiofuata sheria za usalama barabarani.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senso alisema “Tunalaani vikali vikundi vya ngoma ambavyo hivi karibuni vimeibuka kwa wingi na huwa vinafunga mitaa na barabara huku wanawake wakicheza wakiwa uchi.’’
Hivi karibuni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipiga marufuku ngoma za aina hiyo.
Alisema kuwepo kwa vikundi hivyo ni uvunjaji wa sheria na maadili ya nchi, jeshi hilo litawasaka popote walipo ili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Alisema vikundi vya ngoma vinatakiwa kufuata utaratibu unaowekwa na halmashauri za maeneo husika ili kuzuia mianya ya kukiuka maadili.
Akizungumzia tukio la juzi la wachezaji wa kigodoro kudai kupigwa risasi eneo la Mwananyamala, alisema hakuna msanii aliyepigwa risasi, waliumia wakati wa purukushani zilizotokea polisi walipokuwa wakiwatawanya watazamaji wa ngoma hiyo.
“Hata ripoti ya daktari kutoka Hospitali ya Mwananyamala inaonyesha wacheza ngoma hao hawakupigwa risasi kama wanavyodai wao,” alisema Senso.
Akizungumzia operesheni ya bodaboda alisema, “Imekuwa  kawaida kwa madereva wa vyombo hivyo kupita barabarani wakati taa nyekundu zikiwa zinawaka hali ambayo husababisha ajali nyingi. kutokea.”
Alisema kuanzia Januari mpaka Juni, mwaka huu, ajali 1,449 zilizosababishwa na vyombo hivyo zilitokea na kusababisha vifo 218 huku watu 1,304 wakijeruhiwa.
View detail

MAKAMU WA RAIS WA CHINA APOKELEWA TANZANIA NA DKT BILAL

 

1
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo juni 23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita. (Picha na OMR).
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.  Wa pili (Kulia) ni Balozi wa Tanzania, nchini China, Luteni General Abraham Shimbo.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo June 23, 2014. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
4.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia) na baadhi ya Mawaziri wake, akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, aliyeongozana na ujumbe wake  wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
5
Baadhi ya Mawaziri waliofika katika mazungumzo hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, na baadhi kusaini mikataba na watu wa China.
6
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisainiana mkataba na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, wa Makabidhiano ya gari la matangazo la Shirika la Utangazaji la TBC, yaliyofanyika mapema mwaka huu. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao.
7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, (kulia) akisainiana mikataba miwili na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, ya makubaliano ya ushirikiano wa Kitaalamu utakaoiwezesha China kuwapa mafunzo Wanariadha wa Tanzania nchini China na wa makubaliano ya awamu ya tatu ya Ushirikiano wa kiufundi baada ya China kusaidia na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Taifa. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao. View detail

SUMATRA YAKAMATA MABASI 25 YA UDA JIJINI DAR

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Mabasi mengine 25 ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), yamekamatwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Baharini (Sumatra), kutokana na kuendelea kukaidi amri ya kuwataka wafuate sheria za usafirishaji wa abiria jijini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mfawidhi wa Sumatra, Conrad Shio alisema mpaka sasa wameshayakamata mabasi 40, kati ya hayo, 15 yalikamatwa wiki iliyopita.
Madereva wa mabasi hayo wanadaiwa kufanya makosa tofauti ikiwa ni pamoja na kutokuwa na leseni ya uchukuzi wa abiria jijini Dar es Salaam, inayotolewa na mamlaka hiyo, stika na vibao vya kuonyesha njia wanazokwenda.
Shio alisema walipoyakamata awali na kuyaachia, uongozi uliahidi kutekeleza maagizo waliyopewa na Sumatra lakini hawajayatekeleza mpaka sasa.
Alisema pia wamesitisha kwa muda kazi ya kuyakamata na sasa wanaendelea na mazungumzo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema baada ya mazungumzo hayo, atakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kuzungumzia hatua zaidi ambazo watachukua au kile ambacho watakuwa wameafikiana kwa vyombo vya habari.
“Tumeona tusitishe operesheni hii ya kuyakamata mabasi haya ili kutoa nafasi ya mazungumzo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa na iwapo mwafaka usipofikiwa tutajua cha kufanya” alisema Shio.
Kulingana na makosa ambayo yamekutwa katika mabasi hayo, kila basi litalazimika kulipiwa Sh250,000 na kwa mabasi 40, Uda watalazimika kulipia Sh10 milioni. Wiki iliyopita, Sumatra ilianzisha operesheni ya kuyakamata mabasi ya Uda kutokana na  malalamiko ya wananchi kuwa yamekuwa yakivunja sheria na hayana stika wala vibao vinavyoonyesha njia wanazopita.
View detail

Saturday, June 21, 2014

SAMSUNG, BIDHAA MAALUM KWA MAZINGIRA YA AFRIKA


Print
Ukuaji endelevu wa uchumi wa Tanzania umeona ongezeko la kampuni za nje zikiingia nchini zikiwa na nia ya kuzindua bidhaa au huduma zao kwa Watanzania walio wengi. Mafanikio kwa bidhaa na huduma hizi yanategemea mambo mengi kuanzia mazingira hadi uhitaji, kuonyesha kwamba zinakubalika katika soko.

Kampuni moja ambayo imeona mafanikio yaliotulia na kua mtoa huduma tegemezi kwa Watanzania, ni kampuni ya vifaa vya umeme ya Samsung. Kupitia bidhaa zao mbalimbali wameshuhudia mauzo ya zaidi ya bidhaa zao 50,000 ndani ya mwaka mmoja. Katika mwaka ambao unatarajiwa kua wa mafanikio kwa kampuni hii Wanatazamia kudaka asilimia 30 ya soko la vifaa vya kielektroniki.
Takwimu hii inaweza kuja kama mshangao lakini ikiwekwa kwenye mtazamo halisi inajenga picha yenye uwazi. Mafanikio haya yanatokana na utafiti katika soko la Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla.  Ukichanganya mambo kama vile uhitaji wa vifaa vinavyo okoa gharama na zenye uwezo wa kuhimili mazingira ya Kiafrika. Kampuni ya Samsung imeendelea kua mbele kutokana na ubunifu wa bidhaa ambazo kwa pamoja zajulikana kama “Built for Africa”. Sehemu ya friji ndio inazidi kupendwa na wateja wengi katika miaka michache iliopita kutokana na kuaminika na uwezo wa kuhimili mazingira ya Kiafrika. Katika kujengea mafanikio hayo, Samsung inaangalia kulenga soko kupitia aina mpya za friza zinazofaa kwa matumizi ya nyumbani na biashara. Uhitaji wa kuwa tofauti na asili ya uongozi ndio inaweka jina sokoni mpaka sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Bw. Dongha Jang aliunga mkono kauli zilizotajwa alipohojiwa na kusema “Samsung daima inatafuta kuunganisha wateja wake na bidhaa zake kwa kutoa bidhaa zinazosaidia kustawisha maisha ya mtumiaji. Sisi lengo letu ni kuleta teknolojia ya kisasa katika mfumo ambao ni muhimu zaidi kwa soko la Tanzania.” Mr. Jang alifafanua zaidi kuhusu uzinduzi wa bidhaa kadha moja kwa moja kwenye soko la Tanzania “katika hiki kipindi cha miaka michache iliopita tumeona umuhimu wa kuleta bidhaa mpya moja kwa moja kwa watumiaji wetu wa Tanzania kuliko kutegemea uzinduzi kwenye soko la kimataifa”. Miongoni mwa bidhaa Bw. Jang alizokuwa anaongelea katika msemo wake ni uzinduzi sambamba wa bidhaa mbili muhimu za nyumbani ambazo ni Samsung Duracool freezer na Triangle AC.

Uzinduzi huo ulikuwa sehemu ya mkakati wa kudumisha nafasi ya Samsung kama kiongozi wa vifaa vya umeme katika majumba ya Watanzania. Samsung Duracool freezer na Triangle AC zina sifa zinazoruhusu ufanyaji kazi kwa kiwango cha juu ukizingatia mazingira magumu ya Tanzania ikiwemo usambazaji wa umeme usioaminika na gharama zinazo panda. Samsung wanakuja na ahadi ya kurahisisha maisha kwa kuwa na bidha zenye gharama nafuu kwa mtumiaji.
Katika soko ambalo halitabiriki kama la Tanzania, kampuni hii ya vifaa vya umeme imeweza kutambua maeneo yaliokuwa ya maslahi kwa wateja wake kimahesabu. Hii ni dhahiri leo kupitia uwepo wake katika mitaa mbalimbali nchini. Katika mazingira ambayo hayana uhakika wa mafanikio kwa wote, Samsung inaendelea kushinikiza mipaka ya ubunifuu wa bidhaa  ambazo “zimetengenezwa kwa ajili ya Africa”.
View detail

RAIS KIKWETE KURUDIA KAZI YA UALIMU BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE

Jakaya-Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anakusudia kurejea darasani kushika tena chaki kwa kuwa mhadhiri kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi – National Defence College (NDC) cha Dar Es Salaam.
Rais Kikwete amelieleza hilo mchana wa jana, Ijumaa, Juni 20, 2014, wakati alipotoa Mhadhara (Lecture) kuhusu Usalama wa Taifa (The Security of the Nation) mbele ya wanafunzi wa Chuo hicho kilichoko Kunduchi, Dar Es salaam.
Rais Kikwete amewaambia wanafunzi wa kozi ya pili ya Chuo hicho kutoka nchini na nchi za jirani za Uganda, Kenya na Rwanda: “Najisikia mwenye raha sana kuweza kurudi darasani kutoa mhadhara huu. Tukio hili linanikumbusha enzi zangu katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli (TMA). Ni matarajio yangu pia kuwa nitaweza kurudi kuwa mhadhiri katika Chuo hiki baada ya kukamilisha kazi yangu ya sasa.”
Rais Kikwete ambaye alizungumza kwa kiasi cha saa mbili, alianza mhadhara wake baada ya kupata maelezo kuhusu maendeleo ya Chuo hicho na baadaye akajibu maswali ya wanafunzi ambao walimwuuliza kuhusu mambo mbali mbali yanayohusiana na usalama wa nchi.
NDC kilianzishwa rasmi Septemba 2, mwaka 2012 na Chuo hicho kilizinduliwa Rais na Rais Kikwete Septemba 10, mwaka huo huo, 2012 wakati alipotembelea Chuo hicho kwa mara ya kwanza kufuatia juhudi kubwa za uongozi wake kuhakikisha kuwa chuo cha namna hiyo na cha aina yake kinaanzishwa nchini. Rais pia alifungua kozi ya kwanza ya Chuo hicho.
Kundi la wanafunzi wa kwanza kwenye Chuo hicho lilimaliza mafunzo yake Julai 23, mwaka 2013 na sasa chuo hicho kinaendesha kozi ya pili yenye wanafunzi 30. Chuo hicho tayari kimepata usajili kamili wa NECTA ambako kina uwezo wa kutoa shahada ya uzamili katika masomo ya Strategic Studies.
View detail

Wednesday, June 18, 2014

New Fund Launched for African Tech Hubs

Kutokana na mahitaji makubwa ya kuhitaji misaada ya kifedha ili kufikia malengo yakiufundi na ujuzi, basi mkombozi ameingia na kwa kukujali mdau wetu tumekuletea huduma hii karibu,
 Bofya hapa kwa maelezo zaidi View detail

Friday, June 6, 2014

NANI ATAFAIDIKA NA GESI YA MTWARA? MAJIBU HAYA HAPA


mabomba ya gesi
Mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Wananchi wanne kati ya watano wanaamini kuwa mafuta na gesi yatawanufaisha wao, watoto wao na nchi yao kwa ujumla. Wakati huo huo, wananchi wanne kati ya kumi (37%) wanaamini kuwa viongozi wa Serikali na matajiri ndio wataofaidika zaidi. Pia, zaidi ya nusu (55%)  wangependa baadhi ya mapato ya mafuta na gesi wapewe wananchi moja kwa moja kama fedha taslimu.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la Kusimamia Maliasili: Wananchi wanasemaje? Utafiti huu ulifanywa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika kwa njia ya simu ya mkononi wenye uwakilishi wa kitaifa.
Utafiti unaonesha kwamba matakwa ya wananchi ni kuwa, angalau kiasi cha mapato ya mafuta na gesi kipelekwe moja kwa moja kwa wananchi. Mwananchi mmoja kati ya watano (20%) angependelea kiasi kikubwa cha fedha kipelekwa moja kwa moja kwa wananchi; wakati wananchi asilimia 18 wangependelea kuwe na mgawo sawa wa mapato kati ya serikali na wananchi. Asilimia 17 wangependelea Serikali ipate asilimia kubwa zaidi ya mapato kwa ajili ya kuendeleza miundombinu na huduma za kijamii na wananchi wapewe kiasi kinachobaki.

Hata hivyo, Watanzania walio wengi (43%)  wangependa mapato yote yaende Serikalini kwa ajili ya kugharamia huduma muhimu. Isitoshe, wananchi walipoulizwa namna wanavyoamini mapato ya rasilimali yanaweza kuleta manufaa kwa Watanzania, nusu yao (46%) walisema mapato yatumike katika kutoa huduma za afya na elimu, na wananchi wanne kati ya kumi (20%) walipendekeza yatumike kwenye miundombinu au kwenye mipango ya kupambana na umaskini (17%).
Linapokuja suala la usimamizi wa maliasili, jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa Tanzania haiangukii kwenye uhanga wa laana ya utajiri wa maliasili. Uzoefu kutoka nchi nyingine unaonyesha kuwepo kwa uwazi kuhusu mapato na mchakato kama kitu muhimu sana katika kuepuka laana hii, pamoja na ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi yanayohusu namna mapato yanavyosimamiwa.

Hivi sasa, ingawa Watanzania wengi (64%) wanafahamu ugunduzi wa mafuta na gesi, Utafiti wa Sauti za Wananchi ulibaini kuwa Watanzania wawili kati ya watatu (65%)  wangependa kupata taarifa zaidi. Pindi taarifa zinapokosekana, tetesi na uvumi mara nyingi huziba pengo hilo. Ingawa makadirio ya sasa yanasema kuwa uchimbaji mkubwa wa mafuta na gesi hautaleta faida katika kipindi cha miaka saba hadi kumi ijayo, mwananchi mmoja kati ya watatu (36%) anaamini kuwa makampuni ya mafuta na gesi tayari yameshaanza kupata fedha kutokana na ugunduzi huu. Isitoshe wananchi watatu kati ya kumi (28%) hawana uhakika kama tayari kuna mapato kutoka kwenye mafuta na gesi au la. Aina hii ya mapengo kati ya mitazamo na uhalisia, kama haitaangaliwa vizuri, inaweza kusababisha wananchi kutoridhishwa na usimamizi wa maliasili.

Mjadala mwingine mkali umekuwa juu ya nafasi ya makampuni ya ndani na ya nje ya nchi katika kuchimba mafuta na gesi. Wafabiashara wengi wamedai kwa msisitizo upendeleo utolewe kwa makampuni ya Tanzania. Nusu ya Watanzania (52%) wangependa kunufaika na utaalamu wa makampuni ya kigeni katika sekta hii, lakini kwa kushirikiana na makampuni ya ndani ambayo yanapaswa kumiliki hisa kubwa zaidi katika ushirikiano wa kibiashara hio. Mwananchi mmoja kati ya watatu (35%) anaamini kuwa makampuni ya ndani yapewe kipaumbele kwenye zabuni za makubaliano. Aidha, Watanzania sita kati ya kumi (61%) wako tayari kuona mafuta na gesi yakiuzwa kimataifa kwenye nchi zote. Hata hivyo, wananchi watatu kati ya kumi (28%) wanafikiri gesi inapaswa kutumika nchini tu, na mwananchi mmoja tu kati ya ishirini (5%) anafikiri mauzo ya gesi yafanyike nchi za Afrika Mashariki pekee.

Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema “Kama tunataka watu wa Tanzania wanufaike na ugunduzi wa gesi, tunahitaji uongozi wa serikali ulio imara, wenye uwazi na ubunifu. Kuwepo kwa mfuko huru wa utajiri wa taifa ni sehemu moja muhimu ya ufumbuzi. Hata hivyo, tunahitaji kufikiria juu ya njia mbadala, kama vile kupeleka fedha moja kwa moja kwa watu. Jambo la msingi zaidi ni kuweka wazi taarifa, kusikiliza maoni ya wananchi na kuwasiliana ili kujenga imani ya wananchi kufahamu namna fedha za gesi inavyotumika.”
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop