Welcome to our online store Portal

Template Information

Friday, November 30, 2012

Ushahidi mpya wa mauaji ya Mau Mau

 Baadhi ya wapiganaji wa Mau Mau waliodhulumiwa na wakoloni wa Uingereza
Stakabadhi za Serikali zilizotolewa huko Uingereza zinaonyesha kwa ukamilifu namna wafungwa wengi waliuawa wakati wa uasi wa kundi la Mau Mau nchini Kenya.
Wakenya kumi na mmoja walipigwa na walinzi hadi kufa katika kambi walikozuiliwa ya Hola huku wengine wakijeruhiwa mwaka 1959.
Mzee moja manusura wa mauaji hayo kwa sasa ameshtaki serikali ya Uingereza akidai aliteswa.
Stakabadhi hizo zinaonyesha mkutano uliongozwa na aliyekuwa gavana wa Kenya na maafisa wakuu wa magereza kumbukumbu zinazoonyesha kuwa maafisa hao walikiuka haki za binadamu lakini hawakufunguliwa mashtaka. View detail

Rasimu ya katiba Misri yaidhinishwa

 Generali Mamdou Shahin (Kulia) akishauriana na maafisa wa kamati ya katiba kabla ya kupigiwa kura
Kamati inayoandika katiba nchini Misri imeidhinisha rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Hayo yaliafikiwa katika shughuli iliyochukua saa kumi na sita, na kamati hiyo ilikubaliana kwa kauli moja kupitisha vifungu viwili thelathini na nne.
Rasimu hiyo sasa sharti iidhinishwe na rais Morsi kabla ya kupigiwa kura ya maoni.
Wanasiasa waliberali pamoja na wakristu walisusia shughuli za kamati wakisema walihisi kutengwa.
Akizungumza kwa runinga awali Rais Mohamed Morsi amesema kuwa atajiondolea mamlaka mapya aliyojikabidhi pindi tu watu watakapokubaliana kuhusu katiba. View detail

Palestina yapandishwa hadhi na UN

 Wapalestina walisherehekea sana kufuatia tangazo hilo
Baraza la umoja wa mataifa limepitisha kwa kauli moja kwa wingi wa kura kupandisha hadhi ya eneo la Palestina.
Nchi mia moja thelathini na nane ziliunga mkono hatua ya kuitambua Palestina kuwa nchi ambayo si mwanachama wa Umoja wa mataifa lakini itaruhusiwa kushiriki katika shughuli za umoja wa mataifa.
Mataifa tisa yakijumuisha Isarael na Marekani yalipiga kura ya kupinga mpango huo huku mataifa arobaini na moja yakisusia shughuli hiyo.
Kura hiyo yenye umuhimu mkubwa sasa inaiwezesha Palestina kuwa na ushirika na umoja wa mataifa na mashirika mengine kama vile mahakama ya ICC.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa wapelestina wanaweza kutumia nafasi hayo kuishataki Israel kwa kusababisha visa vya dhulma dhidi ya ubinadamu katika ngome yake. View detail

Thursday, November 29, 2012

UN yasaidia Mali ingawa kwa tahadhari

 Waasi wa Tuareg nchini Mali
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon ameunga mkono mapendekezo ya Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuidhinisha vikosi vya usalama vya kulinda amani vya AU vipelekwe Mali kukabiliana na wapiganaji wa kiisalamu Kaskazini ya Mali.
Hata hivyo ilikataa kutoa ufadhili wa Umoja wa Matifa katika shughuli hiyo.
Alionya kuwa kuingiliwa kijeshi katika eneo hilo kutasababisha hatari kubwa za kibinadamu na akataka kuwe na mipango ya kutuliza hali hiyo.
Wanadiplomasia wanasema kuwa vikosi hivyo vitatumia nguvu kupita kiasi ilihali vinatakiwa tu kutoa huduma za kusitisha vita kwa njia ya amani.
Hata hivyo bwana Bana hakutoa msaada wa kifedha na ksuema kuwa mataifa ya Afrika yanahitaji maswali kuhusu jeshi hilo litakavyoendesha kazi zake.
Viongozi wa Afrika wamekuwa wakitaka kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kuunda jeshi la pamoja na nchi za Afrika Magharibi litakalosaidia jeshi la Mali kupambana na waasi.
Jeshi la Mali lilipoteza udhibiti wa Kaskazini mwa nchi ambalo linashikiliwa tena.
Kuhusu mapendekezo yake kwa baraza la usalama la umoja huo, bwana Ban alisema ataidhinisha wanachama wa muungano wa Afrika kuunda kikosi cha wanajeshi 3,300 ambao watajulikana kaa AFISMA kuweza kushika doria nchini humo kwa mwaka mmoja.
Alisema wataisaidia jeshi la Mali kurejesha hali ya utulivu kaskazini mwa nchi na kupunguza tisho la makundi ya kigaidi kuvamia eneo hilo View detail

200 wajeruhiwa wakitafuta kazi Tunisia


Mmoja wa waliojeruhiwa wakitafuta ajira huko Tunisia

Zaidi ya watu mia mbili walijeruhiwa huko Tunisia Jumatano katika siku ya pili ya maandamano jijini Siliana kilomita mia moja Ishirini kutoka katika jiji kuu la Tunis.
Waandamanaji hao walikuwa wakimtaka gavana wa eneo hilo kujiuzulu, kutaka msaada wa kiuchumi na vile vile kushinikiza watu kumi na wanne waliokamatwa katika ghasia za Aprili kuachiliwa.
Maafisa wa usalama walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kuwatwanya watu waliokuwa wanataka ajira. Pia kulikuwa na ripoti za watu kutibiwa baada ya kupata majeraha ya risasi.
Vyama vya wafanyakazi vimeitisha maandamano zaidi baadaye leo.
Tunisia ndiyo ilikuwa kitovu cha mapinduzi ya kiraia katika nchi za Kiarabu ambapo wananchi walimng'oa mamlakani rais wao wa muda mrefu Januari mwaka 2011.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Hamadi Jebali amekataa wito wa waandamanaji kuwa aondoke mamlakani akisema kupitia televisheni kuwa Gavana hang'atuki
Mwandishi wa BBC Sihem Hassaini ambaye yuko mjini Tunis, anasema kuwa maandamano hayo ni ya hivi karibuni katika msururu wa maandamano mengine ya watu wanaeolezea kukerwa na ukosefu wa mageuzi ya kuridhisha tangu mapinduzi ya kiraia kufanyika. View detail

Wednesday, November 28, 2012

INTER UNIVERSITIES BASH PART

CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA, KINAPENDA KUWAALIKA WATU WOTE KTK INTER UNIVERSITIES BASH PART. KWA MAELEZO ZAIDI ANGALIA KTK HILO TANGAZO. View detail

7 kunyongwa Misri kwa kutengeza filamu

 Maandamano yalifanyika kote duniani kupinga Marekani
Mahakama nchini Misri imewapa hukumu ya kunyongwa watu saba walioshukiwa kuitengeza filamu iliyosababisha kero na ghadhabu katika ulimwengu wa kiisilamu mapema mwaka huu.
Hasira dhidi ya filamu hiyo iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed, ilisababisha maandamano dhidi ya Marekani kiasi cha kuteketezwa ubalozi wake nchini Libya.
Washukiwa hao saba walihukumiwa wakiwa hawapo mahakamani.
Hukumu hizo ziliidhinishwa na Mufti mkuu nchini Misri ambaye pia ni msomi wa dini ya kiisilamu.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa ni nadra kwa Mufti kupinga hukumu kama hizi.
Filamu hiyo iliyokuwa ya hali ya chini mno, ilitengezwa mjini Carlifonia, Marekani na kutolewa kwenye internet mwezi Septemba.
Miongoni mwa wale walioshtakiwa ni mtengezaji wa filamu yenyewe Morris Sadek ambaye ni raia wa Misri.
Mahakama itatoa hukumu ya mwisho mwezi Januari kufuatia itikio la Mufti
KWA YEYOTE MWENYE KUPENDA TECHNOLOJIA YA COMPUTER View detail

Tuesday, November 27, 2012

Washukiwa wa ICC Kenya kuunda Muungano

 Uhuru Kenyatta ni mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007

Washukiwa wawili wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya, Uhuru Kenyatta na William Ruto wanajadiliana kwa lengo la kuunda muungano wa kisiasa watakaotumia kugombea uongozi wa nchi.
Taarifa za awali zilisema kuwa wawili hao tayari wameunda muungano huo ingawa baadaye afisa wa mawasiliano wa vigogo hao alikana kuwepo makubaliano yoyote.
Wawili hao ambao ni mahasimu wa jadi kisiasa,wanaanda mkutano wa pamoja siku ya Jumamosi mjini Nakuru mojawapo ya maeneo yaliyokumbwa na ghasia mbaya zaidi za kikabila baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007.
Na hataua ya wawili hawa inakuja wakati mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu ikiwa wanaweza kugombea uongozi wakati wanakbiliwa na tuhuma za kuhusikana ghasia za baada ya uchaguzi ambapo mamia ya watu waliuawa.
Wanasema wameamua kuunda muungano watakaoutumia kuwania nafasi ya rais na makamu wake katika uchaguzi mkuu mwaka ujao kama ishara ya kuwapatanisha wakenya.
Wanatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya ICC baada ya uchaguzi mwaka ujao kujibu mashtaka ya kuhusika na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008
Kenyatta ambaye ni naibu waziri mkuu na Ruto ambaye ni mbunge , wanasema kuwa muungano wao utakuwa wenye kauli mbiu ya kupigia debe umoja wa kitaifa, ustawi na kupatanisha wakenya .
Katika uchaguzi uliopita, wawili hao walikuwa pande pinzani. Na ulikuwa uchaguzi ulioshuhudia upinzani mkali zaidi katika historia ya Kenya.
Ulifuatiwa na ghasia za kikabila ambapo mamia ya watu waliuawa na maelfu wengine kuachwa bila makao mwaka 2007.
Wawili hao wamekanusha madai ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi hasa kupanga makundi ya watu walioshambulia makundi hasimu. View detail

TAARIFA YA KIFO CHA MSANII SHARO MILIONEA KUTOKA KWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA

Sharo Milionea enzi za uhai wake
Namkariri Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Constantine Massawe akizungumza na East Africa Radio jana usiku akisema, “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”

Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.
Kwenye gari alikuwa mwenyewe hivyo hakuna taarifa kamili ya nini kilichotokea maana inaweza kuwa alisinzia.

R.I.P Sharo tulikupenda lakini mungu kakupenda zaidi, kazi zako tulizipenda na tutakukumbuka kwa mengi.
View detail

Rais Zuma awachinjia Ng'ombe wahenga


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewataka wazee wa jadi au wahenga kumsaidia katika kushikilia uongozi wa chama tawala (ANC).
Bwana Zuma alihudhuria sherehe moja kijijini siku ya Jumapili, ambako ng'ombe 12 walichinjwa na huku ubani ukichomwa watu wakimuombea achaguliwe tena.
Wapinzani wake wanataka ang'olewe kutoka katika uongozi wa chama, huku kongamano la chama likitarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Bwana Zuma, ambaye ana wake zaidi ya mmoja na watoto 21, anasifika sana kama mwenye kufuata itikadi za utamaduni wa Zulu.
Alimshinda mtangulizi wake Thabo Mbeki katika kinyang'anyiro kikali kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka
2007 ili kuongoza chama cha ANC.

Mkuki na Ngao

Ushindi wake ulimaanisha kuondoka mamlakani kwa bwana Mbeki na kumweka Kgalema Motlanthe kama rais wa mpito, hadi mwaka 2009 ambapo uchaguzi mkuu ulifanyika na kumuingiza madarakani.
Tawi la vijana wa chama tawala pamoja na maafisa wengine wa serikali sasa wanamfanyia kampeini bwana
Motlanthe, ambaye ni makamu wa rais, kumenyana na bwana Zuma katika kongamano litakalofanyika mwezi ujao, mjini Mangaung.
Wawili hao watakuwa wakigombania uongozi wa chama.
Familia ya Zuma ilichinja ng'ombe 12 na kuchoma ubani katika kijiji chao cha Nkandla mkoani KwaZulu-Natal siku ya Jumapili kuwataka wahenga kumpa mwongozo kabla ya uchaguzi.
"tuko hapa kumtakia kila keri baba yetu. Baada ya sherehe hii tuna imani kuwa ana ulinzi wa kutosha na tuna uhakika atarejea kusherehekea nasi.'' alinukuliwa akisema mwanawe Zuma , Nomthandazo Zuma
Kiongozi wa kijamii alimpa Zuma mshale na ngao akiwa amevalia nguo yenye madoa doa na kumtaka atumie silaha hiyo kujikinga kutokana na wapinzani wake katika chama cha ANC.
Bwana Zuma amekumbwa na kashfa za ufisadi tangu alipochukua mamlaka lakini kulingana na duru za kisiasa huenda akachaguliwa tena. View detail

Monday, November 26, 2012

Waasi wa DRCongo wagoma kuondoka Goma



Waasi wa M23 wamekataa pendekezo la viongozi wa mataifa ya eneo la Maziwa Makuu la kuwataka wakomeshe mapigano na kuondoka mjini Goma.
Waasi hao wanaipinga serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupigana nalo katika eneo la mashariki mwa taifa hilo.
Viongozi hao walitoa pendekezo hilo kutoa fursa mazungumzo ya amani yafanyike ili kutafuta suluhu kwa mgogoro huo.
Hatua ya waasi hao kuuteka mji wa Goma yapata wiki moja iliyopita imezua wasiwasi kwamba huenda yakatokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Awali, serikali ilisema haiwezi kufanya mazungumzo na waasi hao hadi pale watakapoondoka mjini Goma.
Kupitia taarifa, marais wa Rwanda, Kenya, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliiambia M23 "ikomeshe mapigano mara moja na iondoke Goma", na hali kadhalika "ikome kusema kwamba inakusudia kuipindua serikali."
Marais hao pia walipendekeza kawmba:-
  • Serikali hiyo iyaangalie "matakwa halali ya M23"
  • M23 ijiondoe katika maeneo iliyoteka na kusogea takriban 20 km kutoka Goma katika kipindi cha siku mbili
  • Kuundwa kwa kikosi cha pamoja cha wanajeshi kutoka nchi za eneo, serikali, na waasi watakaokuwa katika kiwanja cha ndege cha Goma
  • polisi wa Goma warudishiwe silaha na kurudi kazini
  • walinda amani wa Monusco wawekwe katika eneo huru, kati ya Goma and waasi M23
View detail

Sunday, November 25, 2012

Shilingi Bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini



Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.
Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).
Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.
Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi. Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo (installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.
Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1.      Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.
2.      Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.
3.      Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.

Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha
Dar es Salaam. Novemba 25, 2012 View detail

ETHIOPIA YAIFUNGA KWA TABU SUDAN KUSINI TUSKER CHALLENGE

Mshambuliaji wa Sudan Kusini, Hamisi Leon akipanga mbinu za kumtoka beki wa Ethiopia katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Mamboole, Kampala, Uganda. Ethiopia imeshinda 1-0, bao pekee la Yonatal Kebede Teklemariam kipindi cha pili.
View detail

Saturday, November 24, 2012

KILIMANJARO STARS YAWASILI UGANDA SALAMA



Timu ya kandanda Tanzania bara, Kilimanjaro Stars, ikiwasili ktk uwanja wa ndege wa Entebe nchini Uganda tayari kwa mashindano ya CECAFA Senior Challenge yanatarajiwa kutimua kivumbi kuanzia leo ktk uwanja wa Mandela jijini Kampala

View detail

Friday, November 23, 2012

ANTIVIRUS BORA DUNIANI

Mkuu wa Majeshi DRC afutwa kazi

 
                                                                    Generali Amis


Mkuu wa majeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo.
Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali ya Rais Kabila imemfuta kazi mkuu huyo wa majeshi, siku chache baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao mpia wameutekja mji wa Sake, lakini msemaji wa serikali Lambert Mende, amesema wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuumboa tena mji huo mdogo.
Waasi hao ambao wanaaminika kuungwa mkono na serikali za Rwanda na Uganda, wametishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa Kinshasa, ikiwa rais Joseph Kabila hatabuli kuanzisha mazungumzo ya amani. View detail

Mkuu wa polisi auawa Benghazi

Afisa mmoja mkuu wa usalama nchini Libya amepigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake mjini Benghazi.
Wizara ya usalama wa ndani nchini humo imeelezea kuwa Bwana Farraj al-Dursi , ambaye alikuwa mkuu wa polisi mjini humo, amefariki kutokana na majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Kumekuwa na visa vingi vya mauji mjini Benghazi katika siku za hivi punde.
Mnamo mwezi Septemba, balozi wa marekani mjini Benghazi aliuawa pamoja na wamarekani watatu katika ubalozi huo.
Col Dursia aliteuliwa kuwa mku wa polisi mjini humo muda mfupi baada ya shambulio lililotekelezwa kwenye ubalozi wa Marekani, ambalo balozi wa Marekani na maafisa watatu waliuawa.
Maafisa kadhaa wa Ulinzi wameuawa na watu wasiojulikana mjini Benghazi, mji ambao maandamano na machafuko yaliyomuondoa madarakani Muamarr Gaddafi yalianza.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli, anasema wengi wa maafisa hao wanalengwa kwa sababu wanakisiwa kuwa na uhusiano na serikali ya ya zamani ya nchi hiyo.
Kabla ya serikali, ya Gadaffi kuondolewa madarakani, Kanali, Dursi alifahamika kuwa afisa aliyehusika na kitengo cha kupambana na dawa za kulevya. View detail

DK MWAKYEMBE ATIMUA BODI YA TPA NA KUUNDA MPYA

Tuesday, November 20, 2012

MTOTO ALIYECHOMWA MOTO NA KULISHWA KINYESI NA MAMA YAKE MDOGO SASA AKATWA MKONO



Mtoto anethy johanes akiwa katika hospitali ya rufaa mbeya wodi namba 8 anakopatiwa matibabu mtoto huyo alifikishwa hapo baada ya mama yake mdogo kumchoma moto huku akimlisha kinyesi ambapo baadaye wasamaria wema walijitokeza kumuokoa mtoto
huyo na baadaye kumpeleka katika hospitali ya rufaa mbeya .hata hivyo mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo madaktari walilazimika kumkata mkono wake baada ya kile kinachodaiwa kuwa angeweza kupata madhara zaidi kwa kuwa mkono wake ulianza kuoza.kwa mujibu wa muuguzi wa wodi hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa si msemaji, alisema kuwa hivi sasa mtoto huyo yuko chini ya uangalizi wa hositali hiyo anahudumiwa matibabu na kupewa chakula ambapo anapatiwa yai moja na karanga maalumu nyakati za asubuhi pamoja na chakula.
View detail

Thursday, November 8, 2012

WATU WAGANDANA WAKIFANYA TENDO LA NDOA LISILO HALALI. (TEMEKE HOSPITALI HALI SI SHWARI, POLISI WAINGILIA KATI)

Shiliningi milioni 5 za kitanzania zinahitajika ili kuwanusuru watu wawili walionasiana wakivunja amri sita. Watu wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam wanadaiwa kukutwa wakiwa wamenasana wakati wakifanya tendo maalum la watu walio katika mahusiano (mke na mume) na kwakua wao sio mke na mume halali wamenasiana. Mume wa mwanake ambae amefikwa na maswaibu hayo ya mwaka jijini Dar es Salaam anahitaji kiasi hicho cha fedha ili atoe PASSWORD ya pin hiyo kali aliuyoiweka katika eneo takatifu la unyumba wao. Taarifa za awali kutoka Temeke zinapasha kuwa wawili hao wapo katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa unasuaji ambao wadadisi wa mambo hasa ya kijamii wanadai Hospitali hawataweza kuwanasua isipokuwa kwa wataalm wa jadi hasa Mume wa Mwenye mke ambaye aliwekewa tego. Blog hii itatujuza zaidi juu ya tukio hilo ambalo hadi sasa limekuwa ni gumzo jijini na kujaza umati mkubwa wa watu na kusababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu eneo la tukio.

WATU WAWILI WAGANDANA TEMEKE
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop