Ghasia zimekuwa jambo la kila mara Misri tangu Morsi kuondolewa mamlakani
Watu saba wameuawa mjini Cairo
usiku wa kuamkia leo kufuatia makabiliano makali kati ta wanajeshi wa
serikali na wafuasi wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani, Mohamed
Morsi.
Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya na
kuwasukuma nyuma waandamanaji hao ambao walikuwa wakiwarushia mawe huku
wakiwa wamefunga barabara kuu inayoelekea kati kati mwa mji mkuu.
Ghasia hizo zimetokea huku naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, William Burns akiwa ziarani nchini humo.
Waziri huyo amesema taifa hilo limepewa nafasi ya pili kurejesha utawala wa kidemokrasia.
Bwana Burn alifanya mashauriano na viongozi wa
serikali ya mpito ya nchi hiyo, lakini viongozi wa chama cha Muslim
Brotherhood, walisusia mkutano huo.
Awali mamia ya wafuasi wa kiongozi
aliyepinduliwa Misri Mohamed Morsi wamepambana na vikosi vya usalama
katikati mwa mji wa Cairo na kuwafyatulia waandamanaji hao gesi ya kutoa
machozi.
Mapigano hayo yanajiri muda mfupi baada ya
mjumbe mkuu wa Marekani William Burns kutoa wito kwa vikosi vya usalama
kujizuia kwa kiwango kikubwa katika kukabiliana na maandamano hayo.
Makabiliano yalifanyika baada ya naibu waziri wa
mambo ya nje wa Marekani anayezuru Misri, kuwataka maafisa wa usalama
kuhakikisha kuwa wanajitahidi kutuliza ghasia wakati wakijizuia kufanya
mauaji yoyote.
Burns alikutana na maafisa wa serikali inayoungwa mkono na majeshi.
Lakini chama cha Muslim Brotherhood kimesema haikina nia ya kukutana na waziri huyo.
Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa
serikali mpya inayoungwa mkono na jeshi nchini, mjumbe huyo, William
Burns, amesema Misri imepewa nafasi ya pili kufuatia kupinduliwa na
jeshi Mohammed Morsi.
Alikutana na serikali inayoungwa mkono na jeshi
nchini lakini Muslim Brotherhood, inasema haina mpango wa kukutana naye.
Naibu rais wa tawi la kisiasa la chama cha Morsi, Muslim
Brotherhood,Essam el-Erian, ametoa wito wa utulivu.