Welcome to our online store Portal

Template Information

Sunday, December 29, 2013

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI


D92A7272
 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.Akiwa nachini Marekani Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.(picha na Freddy Maro).
D92A7296
Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Kikwete Mrisho mara baada ya kumlaki muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake nchini Marekani. Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini jana, Ijumaa, Desemba 27, 2013, akitokea New York, Marekani.
Rais Kikwete amekuwa New York kwa wiki moja kwa shughuli za kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam, Rais Kikwete amelakiwa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
View detail

MAWAZIRI MZIGO LAZIMA WAWAJIBISHWE, FILIKUNJOMBE

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Makamu Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge, Fedha na Uchumi, Deos Filikunjombe amesema mkakati ya kuwang’oa mawaziri wanaoshindwa kutekeleza mipango ya Serikali  ya kuwaletea maendeleo wananchi ni endelevu.
Filikunjombe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Njombe alitoa msimamo huo wakati wa Ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu William Pasvual Johson  lililopo Kijiji cha Ilela,  Kata ya Manda wilayani hapo.
Alisema mkakati wa wabunge kuwawajibisha mawaziri wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao hauna nia mbaya, bali unalenga kuhakikisha mawaziri na Serikali wanatekeleza  majukumu yao.
“Siyo kwamba wabunge tunakuwa wakali, kimsingi tunatimiza wajibu wetu tunachotaka sisi, mawaziri na Serikali watimize wajibu wao,” alisesma.
Filikunjombe alisema tukio la hivi karibuni la wabunge kushinikiza mawaziri waliozembea katika Operesheni Tokomeza Ujangili lilifanyika kwa nia ya kuwatetea wananchi.
Alisisitiza kuwa hata kesho ikitokea kuna waziri ambaye anazembea kutekeleza majukumu yake, wabunge hawatasita kushughulika naye.
“Tutaendelea kushughulika na mawaziri wazembe kwa niaba yenu,” alisisitiza.
Akitoa salamu za Krismasi na Mwaka Mpya, Padri wa kanisa hilo, Reuben Ngoye alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi wa busara wa kuwang’oa mawaziri ambao walililalamikiwa na wabunge kwa kushindwa kusimamia vizuri utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
 “Uamuzi wa Kikwete wa kuwaengua mawaziri hao umenifanya niamini kuwa kiongozi wetu ana msimamo,” alisema Padri Ngoye.
View detail

250 WAJIUNGA NA CCM NA KURUDISHA KADI ZA UPINZANI TEMEKE

Watu 250 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia  Tawi la Kigunga B, Kilakala wilayani Temeke jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya, Katibu wa Vijana wa CCM, wilayani Temeke Onesha Haruna amesema viongozi wa chama hicho wana jukumu kubwa la kuhakikisha idadi ya wanachama inaongezeka kila kukicha.
Hili litafanikiwa ikiwa kila mmoja wao atatekeleza ilani ya chama chao kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kufanya uhamasishaji kwa watu mbalimbali.
“Ilani ya CCM haina mapungufu hata chembe. Ikiwa itafuatwa na kutekelezwa kila kilichoandikwa ndani yake, ni wazi kuwa chama chetu kitakuwa chama cha mfano na chenye kuongoza kwa idadi ya wanachama kuliko hata ilivyo sasa”  alisema.
Licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo za ndani kama vile kuwepo kwa makundi ndani ya chama, bado kimeonyesha kuimarika zaidi kutokana na kuwa na viongozi wenye moyo madhubuti wa kukiongoza.
Katika hotuba yake, Haruna alitoa wito kwa wenyeviti wa vijana katika matawi ya wilaya hiyo kuhamasisha makundi ya vijana kujiunga na CCM.
“Vijana ni taifa la leo, hivyo kuwa na ushiriki mkubwa ndani ya chama, kuwezesha kupatikana kwa maendeleo kwani siku zote chama ni watu,” alisema Haruna.
View detail

WATU WANNE WAILUWA GEITA

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Watu wanne wakazi wa Kijiji cha Nyankumbu mkoani Geita, wameuawa kikatili kwa kuchomwa moto na mwingine akifia kwenye dimbwi la maji kijijini hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paul alisema kuwa  tukio hilo la kikatili lilitokea usiku  wa juzi.
Paul alisema saa sita usiku watu wanaokadiriwa  watano walikwenda nyumbani kwa Mzee Barabara Luhemeja kwa lengo la kupora fedha .
“Watu hao walikwenda kwenye nyumba ya Luhemeja na kumkuta mtoto wake waliyemtaka kuwaonyesha mahali alipo baba yake,” alisema Kamanda Paul.
Alisema kuwa wakati wakiendelea kumhoji mtoto huyo awaonyeshe baba yake, ghafla alitokea ambapo watu hao walimweka chini ya ulinzi kabla ya kupora Sh60,000 ambazo ni rambirambi ya kufiwa na mjukuu wake.
Paul alisema kuwa baada kupora fedha hizo, walikimbia, ambapo mzee huyo alitoa kwa sungusungu walioanza msako wa watu haona kubahatika kumkamata mmoja aliyewataja wenzake.
Baada ya watuhumiwa wote kukamatwa, wananchi waliwafunga kamba na kuwachoma moto.
Akizungumza kwa huzuni, mama mmoja ambaye jina lake halikupatikana, ambaye pia miongoni wa waliouawa ni watoto wake, alisema: “Ndiyo kwanza napata taarifa kwamba watoto wangu walikuwa wezi,” Nyambona Malwa alisema kuwa hana taarifa.
Aidha Kamanda alisema kuwa watu waliouawa katika tukio hilo majina yao hayajafahamika, kwani walikuwa wageni kwenye kijiji hicho.
Kamanda Paul ameonya tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi, kwani jeshi lake halitasita kuwachukulia hatua kali.
“Mpaka sasa tunawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya watu hayo na uchunguzi wa kuwabaini wengine unaendelea,” alisema Kamanda Paul.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Said Magalula naye ameonya tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi, akisema kamwe haivumiliki na kuwataka kuacha vitendo hivyo mara moja.
“Mwizi akikamatwa, asiuawe, wananchi watoe taarifa kituo cha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe kama kupekwa kortini.”
View detail

MTOTO WA MWAKA 1 AUAWA NA KUKATWA SEHEMU ZA SIRI

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Watu saba wamefariki dunia katika matukio tofauti wakati wa   Sikukuu ya Krismasi mkoani Morogoro, akiwemo mtoto wa mwaka mmoja kuuawa na watu wasiofahamika kisha kukatwa sehemu zake za siri na mwili wake kutupwa pembezoni mwa Mto Morogoro.
 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alimtaja mtoto aliyefariki  kuwa ni James Stephen (1), mkazi wa Nanenane Manispaa ya Morogoro na kwamba tukio hilo lilitokea Desemba 25 mwaka huu saa moja asubuhi.
 Katika tukio la pili, mtoto Veronica Chigunda (6) mkazi wa Mashambani Likwambe, Wilaya Ulanga alifariki dunia wakati akipelekwa Hospitali ya Lugala baada ya kuungua moto wakati amelala kwenye nyumba anayoishi.
 Kamanda Shilogile alisema kuwa tukio hilo lilisababisha majeraha kwa watu wawili, akiwemo mama wa marehemu Paula Fimbo (24) na Matiasi Mahumba (1) na wote wamelazwa katika hospitali hiyo.
 Shilogile alisema tukio la nne, mfugaji wa jamii ya kimasai Mela Kipara (25) mkazi wa Makole wilayani Mvomero, alifariki dunia baada ya kukatwa na mapanga na mfugaji mwenzie wakati wakitoka kunywa pombe za kienyeji.
Aidha, Mganga Machaku (35) mkazi wa Mdudu, Kilosa alikutwa ndani ya nyumba yake amekufa na mwili wake ukiwa umeharibika vibaya huku chanzo cha kifo hicho kikiwa ni kunywa pombe za kienyeji kupita kiasi.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi  Kanda Maalumu  Dar es Salaam, limejipanga kuongeza  ulinzi katika kuelekea mkesha wa Mwaka Mpya.
View detail

Saturday, December 28, 2013

MWAMUNYANGE, MWEMA HALI YAZIDI KUA TETE

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Mkuu wa Majeshi Nchini, Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema nao wametakiwa kujiuzulu kutokana na uozo uliobainika katika ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili, iliyosababisha Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wake wanne.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katibu wa madiwani wa jiji hilo, Julian Bujugo alisema wakuu hao wanapaswa kujiuzulu kwa kuwa wao ndio wanaotoa amri kwa askari wao na siyo mawaziri.
“Nao wanatakiwa kuchukua uamuzi wa kujiuzulu kama hatua ya kuonyesha uwajibikaji wao, askari wao wamefanya maovu makubwa,” alisema. Alisema kama wakuu hao wa watakaidi agizo la madiwani watalipeleka suala hilo kwa Rais Kikwete.
“Watendaji wa Serikali ndio chanzo cha uonevu, hata mawaziri ‘mizigo’, nao wanatakiwa kujiuzulu. Alimtolea mfano Waziri wa Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Bujugo alisema ameshindwa kuwasimamia wakulima na kusababisha mvutano na vurugu katika Sekta ya Kilimo.
Chiza alitajwa kama waziri ‘mzigo’ na Kamati Kuu ya CCM iliyokutana wiki mbili zilizopita chini ya uenyekiti wa rais Kikwete.
Bujugo ambaye ni diwani wa Kata ya Magomeni alisema mbali na wakuu hao wa ulinzi na usalama, pia wakuu wote wa wilaya waliohusika kusimamia operesheni hiyo nao wanapaswa kuwajibika kwa kuwa walijua na waliona wazi vitendo vichafu walivyofanyiwa wananchi lakini walikaa kimya.
Ripoti ya tume ya kuchunguza Operesheni Tokomeza Ujangili ilisomwa bungeni mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita na mwenyekiti wa Kamati hiyo, James Lembelii na kuwango’a mawaziri hao.
Waliong’olewa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, huku Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa njia panda kutokana na wabunge kuendesha mpango wa chini chini wa kupiga kura ya kutokuwa na Imani naye kwa maelezo kuwa ameshindwa kuwasimamia mawaziri wake.
View detail

PROF. LIPUMBA AIONYA SERIKALI

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa matatizo ya kiuchumi, kwa kuwa hali ilivyo sasa ni mbaya.
Profesa Lipumba ambaye pia ni profesa wa uchumi alisema hivi karibuni Dar es Salaam kuwa hali ya uchumi imezidi kudorora na kusababisha maisha ya wananchi wengi kuwa magumu.
“Vijana wa siku hizi wengi hawana simile kushughulika na mambo yanapokwenda sivyo, ajabu ni kwamba wanaofanya mambo hayo yawe magumu wamekuwa wepesi wa kutetea kwa hoja zisizo na msingi kwa masilahi yao binafsi,” alisema.
Akizungumzia maazimio yaliyofikiwa kwenye Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kilichofanyika Desemba 21-22 mwaka huu Dar es Salaam, alisema hatua ya kupandishwa kwa gharama za umeme iliyotangazwa hivi karibuni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mambo ambayo yanaendelea kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi, jambo ambalo lingeweza kuzuilika kwa shirika hilo kudhibiti wizi wa nishati hiyo.
Kuhusu hali ya kisiasa nchini, Profesa Lipumba alisema Baraza Kuu limetoa wito kwa vyombo vya Dola kuwa na weledi na uadilifu na kuacha kutekeleza amri za wanasiasa zisizojali utawala wa sheria na haki za binadamu ili vipunguze uhasama baina yao na raia.
“Serikali pia isitumie Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kushughulikia masuala ya uvunjifu wa sheria katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, badala yake kazi hiyo ifanywe na Jeshi la Polisi kwa mujibu wa taratibu za kisheria. Nao pia waongezewe uwezo wa kiutendaji,” alisema.
Alisema CUF inaona si vyema kutumia JWTZ kudhibiti vurugu kwa kuwa wanajeshi hao hawana mafunzo ya kukamata wananchi wenye tuhuma za uhalifu isipokuwa wamefundishwa jinsi ya kulinda usalama wa nchi katika mipaka.
View detail

MWILI WA KHALID KITARA WAKABIDHIWA KWA JAMAA BAADA YA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Picha na Mktaba
Mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara wa Kariakoo, Dar es Salaam, Khalid Kitara (47) uliokutwa na dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni heroini, umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya utaratibu wa mazishi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kwamba baada ya kufanyika kwa uchunguzi huo wameamua kukabidhi mwili huo huku wakiendelea na upelelezi kubaini mtandao unaohusika na tukio hilo.
 
Alisema jeshi hilo bado linaendelea kuwashikilia watuhumiwa watatu, ambao ni madereva wawili waliokuwa wakipokezana kuendesha gari hilo ambao aliwataja kuwa ni Teddy Sichilima (27), mkazi wa Tunduma Mbeya, Lucas Atubonekisye (32), mkazi wa Mtaa wa Songea, Tunduma na aliyekutwa na mwili wa Marehemu, Jumbe Mbano (36), mfanyabiashara na mkazi wa Kariakoo. Alisema watu hao watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.
Alitoa wito kwa jamii kuendelea kuwafichua wahalifu ili sheria ichukue mkondo wake huku akisisitiza azma ya polisi kupambana kuhakikisha linatokomeza biashara ya dawa ya kulevya ambazo kwa sasa uuzaji wa dawa hizo umeonekana kuzagaa nchini.
View detail

TUGHE HALI YAZIDI KUA TETE

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Hali si shwari katika Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (Tughe), baada ya Baraza lake Kuu la Taifa kuwasimamisha viongozi wakuu hadi mkutano mkuu wa chama hicho utakapoitishwa.
Viongozi hao wamesimamishwa kutokana na kukacha mkutano wa Baraza Kuu la Taifa baada ya kuhojiwa kwa tuhuma za ubadhirifu na kuvunja katiba.
Mwenyekiti wa Kamati Teule, Archie Mntambo alisema viongozi hao walikimbia baada ya kuhojiwa juu ya uvunjifu wa katiba kwa kutoitisha vikao vya baraza hilo na ubadhirifu wa fedha za chama hicho.
Akizungumza kabla ya kuahirisha mkutano huo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini hapa, Mntambo aliwataja waliosimamishwa kuwa ni Mwenyekiti wa Taifa, Dk Diwani Mrutu, Makamu Mwenyekiti, Maclean Chitete na Katibu Mkuu Ally Kiwenge.
Alisema kikao hicho hakina madaraka ya kuwavua uongozi na kwamba suala hilo litapelekwa kwenye mkutano mkuu wenye uamuzi wa mwisho kuhusiana na jambo hilo.
“Tangu wachaguliwe Septemba, 2011, hawajawahi kuitisha kikao cha Baraza Kuu la Taifa ambalo ndilo linalohusika na upangaji wa bajeti ya chama,” alisema.
Alisema viongozi hao baada ya kusomewa mashtaka yao waliitwa mmojammoja mbele ya wajumbe wa baraza hilo na kuhojiwa lakini kabla ya kupewa majibu ya tuhuma zao waliondoka.
Katiba ya chama hicho inautaka uongozi kuitisha vikao vya baraza kuu mara mbili kwa kila mwaka.

Hata hivyo, Chitete alikana kusimamishwa akisema mkutano huo ambao ulianza Desemba 19 mwaka huu, ulimalizika kwa mwenyekiti kuufunga... “Mwenyekiti wa Taifa alifunga kikao na mimi nikaondoka kwenda hotelini kwangu.”
Kwa upande wake, Dk Mrutu alisema jana kuwa kikao hicho kilichochagua kamati teule hakikuwa halali kwa sababu alifunga kikao bila uamuzi huo kufikiwa.
Kuhusu tuhuma za ubadhirifu na uvunjaji wa katiba, alikataa kulizungumzia suala hilo kwa undani na kusema anasubiri barua ya kumtuhumu kutoka katika kikao halali cha chama.
View detail

RAGE APASUA JIPU

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema amesikitishwa na madai kuwa hakuhusika na ushindi dhidi ya Yanga.
Madai hayo yalitolewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Sued Nkwabi kwamba hakuhusika kufanikisha ushindi dhidi ya wapinzani wao, Yanga katika mchezo wa Nani Mtani Jembe ambapo Simba ilishinda 3-1.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rage alisema anashangaa madai ya namna hiyo yanaelekezwa kwake Simba inapofanya vibaya licha ya kwamba yeye si kocha, lakini inapofanya vizuri huambiwa hahusiki.
“Nimewasikia hao wanaosema kwamba mimi sikuhusika na ushindi ilioupata Simba katika pambano dhidi ya Yanga. Huku ni kupotosha.
“Unawezaje kusema mimi sijahusika wakati hata mchezaji aliyefunga bao la tatu Awadh Juma nilimsajili mimi nyumbani kwangu? Na siyo bao la tatu tu, hata pasi ya bao la kwanza alilofunga Hamis Tambwe alitoa yeye,” alisema Rage na kuongeza:
“Kila mtu ana uhuru wa kuongea lakini tuwe wa kweli basi, ukisema Kamati ya Utendaji ya Simba ndiyo imefanikisha ushindi maana yake na mimi ni sehemu hiyo kamati inaonekana watu wengine hawaijui hata katiba ya Simba.”
Siku chache baada ya pambano hilo ambalo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, Nkwabi alisema Rage hakuchangia kwa namna yoyote kufanikisha timu yao kuibuka na ushindi.
Rage yuko kwenye mgogoro na Kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba baada ya wajumbe hao kumsimamisha uongozi wakati akiwa yeye hayupo kikaoni.
View detail

MDAU RIDHIWAN ISSAH ALAMBA NONDOZ!

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Ni mdau mkubwa wa blog yetu ambae yupo Iringa kikazi, amefanikiwa kumaliza elimu yake ya chuo kikuu baada ya kutaabikia elimu kwa miaka mitatu sasa. Mungu akujaalie mdau ufike mbali zaidi View detail

Friday, December 27, 2013

Tanzanian Woman arrested in Macao China for Drugs Smuggling

eca86bd9dddf141e387d29
A 28-year-old woman from Tanzania was arrested on a charge of drug possession in Macao, Dec 19, 2013. She hid 1.1 kilograms ofheroin valued at $137,720 in her body and took a flight from Thailand to Macao on Tuesday. She said her destination was Guangzhou, capital of South China’s Guangdong province.
eca86bd9dddf141e39412a
Drugs excreted from a 28-year-old woman’s body are shown. The woman, who is from Tanzania, was arrested on a charge of drug possession, Dec 19, 2013. She hid 1.1 kilograms of heroin valued at $137,720 in her body and took a flight from Thailand to Macao onTuesday
eca86bd9dddf141e3a492b

View detail

NAFASI ZA MAFUNZO YA MUDA MREFU NA MUDA MFUPI KWA WATANZANIA

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Kutokana na mabadiliko ya nyanja mbalimbali nchini, serikali kwa kushirikiana na nchi ya Australia imetoa nafasi kwa watanzania wenye sifa ktk fani mbalimbali kwenda Australia kwa mafunzo ya muda mrefu na mfupi. kuona nafasi zilizopo bofya hapa  View detail

NAFASI ZA KAZI KWA WATANZANIA WENYE SIFA ZINAZOSTAHILI

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Kutoka na mahitaji mkubwa wa watumishi serikalini na kupunguza wafanyakazi hewa, serikali imeamua kutangaza kazi zake kupitia mfumo wa pamoja wa utumishi wa umma. kuona nafasi zilizotangazwa bofya hapa View detail

Thursday, December 26, 2013

DR. BILALI AZURU FAMILIA YA MAREHEMU SHEKH SULEIMAN AMOUR JENDELE


IMG_7340
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) aliyefariki Dunia hivi karibuni wakati alipofika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja jana Disemba 25-2013.
IMG_7345
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo.
IMG_7347
IMG_7354
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) kwenye Makaburi alipozikwa kijijini kwake Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo jana Disemba 25-2013   (Picha na OMR).
View detail

PINDA ASHEHEREKEA X-MASS KIBAONI


IMG_0064
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wazee baada ya ibada ya  Krismasi iliyofanyika kijijini kwake, Kibaoni wilayani  Mlele, Katavi, Desemba 25, 2013.
 (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
IMG_0066
IMG_0043
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na watoto  baada ya ibada ya Krismasi iliyofanyika  kijijini kwa Waziri Mkuu, Kibaoni wilayani Mlele, Katavi Desemba 25,2013.
 (Pichana Ofisi ya Waziri  Mkuu)
View detail

Wednesday, December 25, 2013

WATAALAMU WA UCHUMI WAIPINGA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Baadhi ya wachumi na wadau mbalimbali wa nishati ya umeme wameikosoa hatua ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya kuongeza gharama za umeme kwa maelezo kuwa hatua hiyo itamkandamiza mwananchi wa kawaida.
Kauli hizo zimekuja siku moja baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei mpya za umeme huku kukiwa na ongezeko kubwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam jana, baadhi yao walisema hatua iliyochukuliwa siyo mwarobaini wa matatizo ya umeme, badala yake unahitajika mfumo mpya wa kiutendaji ili kuinusuru Tanesco.
Mjumbe wa Bodi ya Umoja wa Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Felix Mosha alisema kitendo cha kuongeza gharama ya umeme kitapunguza ushindani wa kibiashara.
“Wananchi walitarajia ongezeko la viwango vya gharama ambavyo vingeweza kuongeza ushindani wa bidhaa zetu dhidi ya zile zinazotoka nje. Tangazo hilo la Ewura linatakiwa kutazamwa upya,” alisema Mosha.
Pia alisema kuwa gharama za uzalishaji nchini zimekuwa kubwa kutokana na matumizi ya jenereta ambazo ni mara nne zaidi ya mitambo ya kawaida.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini (CEO’s Roundtable), Ali Mufuruki alitofautiana msimamo huo wa wenye viwanda akisema hatua hiyo ni sahihi endapo itakuwa suluhisho la kupunguza changamoto za kupatikana kwa umeme.
Mufuruki alisema Tanesco imekuwa na tatizo kubwa la kununua umeme kwa bei ya juu ukilinganisha na ankara inazotuma kwa wateja wake.
“Tusiangalie zaidi kumuathiri mwananchi na kupunguza ushindani wa kibiashara tu kwani mtu anaweza kujipanga. Ni heri bei ipande kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa kutosha kuliko kuwa na umeme wa kubabaisha,” alisema Mufuruki.
Wanaharakati
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo-Bisimba alisema mwananchi amebebeshwa mzigo huku baadhi ya watumishi wa Tanesco wakituhumiwa kufanya ubadhirifu.
“Leo hii mamalishe na wajasiriamali wadogo watafanyaje kazi zao? Kwa nini wadaiwa sugu wa kodi wasingebebeshwa mzigo huo... Mimi ningekuwa na uwezo ningetembea peke yangu kuandamana kwa sababu wananchi wanaona lakini wanaendelea kuvumilia maumivu yasiyostahili,” alisema Dk Bisimba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya alisema kwa ongezeko hilo la bei, Serikali haina mpango madhubuti wa kupunguza umaskini wa Mtanzania.
“Kuna kila sababu ya Serikali kukaa chini na kutafakari upya juu ya gharama hizo za umeme ili kumsaidia mwananchi kwa sababu hakuna uhusiano wa kupanda kwa gharama hizo na maisha anayoishi kwa sasa na badala yake itaendelea kumuumiza,” alisema Usu.
TUCTA yatoa tamko
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholas Mgaya alisema shirikisho hilo limetoa maazimio kadhaa ikiwamo kuitaka Serikali kuongeza mishahara kwa wafanyabiashara ili kutengeneza uhusiano wa ongezeko hilo na kipato cha mshahara uliopo.
“Kama imeona ni vyema kuongeza bei hizo, basi iongeze hata mishahara kwani ongezeko la Tanesco ni asilimia 40 kwa mtu wa chini wakati mshahara wake ulipanda kwa asilimia 25 tu. Kwa mazingira hayo ni lazima ataumia tu,” alisema Mgaya.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya kiuchumi alisema Tanesco itahitaji kuwa na menejimenti yenye uwezo wa kulisimamia shirika hilo ikiwa ni pamoja na kudhibiti upotevu mkubwa wa fedha.
“Hakuna menejimenti ya kusimamia shirika, tunataka uongozi wa watu wenye uwezo wa kulinusuru shirika ambao wataokoa upotevu wa fedha,” alisema Profesa Lipumba.
Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Constantine Akitanda alisema kupanda kwa gharama za umeme kunaathiri sekta nyingine zinazotegemea huduma kutoka Tanesco, hivyo wananchi wategemee mabadiliko ya bei za bidhaa.
“Ni bora wangeboresha miundombinu ya Tanesco na kuondoa mikataba mibovu ambayo inawafanya watumie sehemu kubwa ya mapato yao kulipa madeni,” alisema Akitanda.
View detail

NILIPOJIUNGA NA CHADEMA DR. SLAA ALIKUA CCM, ZITTO KABWE

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe, amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema alichukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.
“Wakati hao wenye midomo mikubwa wanaoongea sasa, walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa mnapigwa mabomu kutaka mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi na ndiyo maana hatuwezi kuwaachia.
Hatuwezi kukubali, hatutoki, demokrasia ni mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi yangu ya Chadema nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa nne mwaka 1993, nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu Mkuu wa chama changu alikuwa yuko CCM.
Akizungumza kile alichosema ni uongo unaosambazwa na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na Mwenyekiti wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na Dk Slaa Kanda ya Magharibi.
Alisema kwenye mikutano hiyo, Mbowe anasema kuwa endapo mbunge huyo atarudi yeye Mbowe atajiuzulu, suala alilosema linaonyesha kuwa tayari ameshafukuzwa bila hata utetezi wake kusikilizwa.
Alisema baada ya viongozi hao kuzungumza na kusema mambo hayo na yeye aliamua kurudi nyumbani Kigoma na baada ya kuona hilo Dk Slaa akahoji mbunge huyo anafanya vikao hivyo kama nani.
“Mimi nimekata rufaa, wajumbe wa baraza kuu wa Mtwara, Ruvuma wanaandika barua wanataka mkutano mkuu, Katibu Mkuu akiwa Igunga anasema hiyo ni haramu na hao wafuasi wa Zitto watafanya Zitto afukuzwe, si __wamwamesha nifukuza? takachokuja kunijadili, hivyo si wameshanifukuza ?
View detail

KISA CHA YANGA KUMFUKUZA KOCHA WAO HIKI HAPA


http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Timu ya Yanga  nchini Tanzania imeingia ktk hatua nyingine baada ya kufungwa na watani wao wa jadi (Simba SC (Mtani Jembe)) juma  lililopita na kufikia maamuzi mazito ya kumfukuza kocha wao ambae bado alikua anapanga kikosi chake. Kuona kisa kilichomtoa kocha huyo Bofya hapa View detail

Tuesday, December 24, 2013

MABASI YATEMBEAYO MAJINI NA NCHI KAVU KUINGIA TANZANIA

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/

Kampuni ya Transevents Marketing Ltd ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious Transport(DAT) linalotengeneza mabasi  kutoka Uholanzi  yenye uwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayoanzia Tanzania.

Mabasi hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha swala zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.
http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
 
Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu. Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu  kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.
Video hizi Mbili zinaelezea kwa kina na kuonesha jinsi Mabasi haya yatakavyokuwa yakifanya kazi hapa nchini Tanzania
http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
View detail

DR. MWAKYEMBE AKAGUA NAULI ZA MABASI MWENYEWE NA KUWATOZA FAINI WALIOZIDISHA NAULI

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Waziri wa Uchukuzi,Dr Harisoni Mwakembe afanya ukakuguzi wa tiketi ilikubaini mabasi yaliyotoza gharama kubwa za nauli za kusafiria katika kipindi cha Xmass na mwaka mpya,badhi ya mabasi yalikamatwa na kuamuliwa kuwarudisha nauli zilizozidi abiria wao. zoezi hilo limefanyika majira ya alfajiri katika eneo la Visiga mkoani pwani na kila basi lilozidisha nauli lilitozwa faini ya shilingi laki mbili na nusu.
http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
View detail

WATANZANIA WANNE WAKAMATWA NA HEROIN

GEDSC DIGITAL CAMERA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari bunduki aina ya SMG iliyokamatwa wilayani Ngorongoro hivi karibuni huku mkono wake wa kulia akiwa ameshika kifurushi chenye madawa ya kulevya aina ya Heroin yaliyokamatwa jana wilayani Arumeru. 
(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Kuelekea katika kusherehekea Sikukuu ya Krimas, Jeshi la Polisi Mkoani hapa limeendelea kupambana na wahalifu wa madawa ya kulevya ambapo safari hii limefanikiwa kuwakamata watu wanne wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin. Tukio hilo limetokea jana tarehe 23.12.2014 muda wa saa 12:30 jioni maeneo ya Elikyurei wilayani Arumeru.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas amesema kwamba tukio hilo limefanikiwa baada ya kupata taarifa toka kwa raia wema ambapo askari wa Jeshi hilo walikwenda katika eneo husika na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa ndani ya chumba cha mtuhumiwa mmojawapo huku wakiwa wanaendelea kufunga kete za madawa hayo na tayari walikuwa wamefunga kete 25.
Kamanda Sabas aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Seifu Bakari (28) na Hamid Makame wote ni wakazi wa Elikyurei wilayani Arumeru pamoja na wenzao ambao ni Evance Gidion (29) Mkazi wa Ngarenaro na Abraham Hamis (23) Mkazi wa Kaloleni jijini hapa.

Kamanda Sabas alisema kwamba madawa hayo yenye uzito wa gramu 100 yanakadiriwa kuwa na thamani ya Tsh 10 Mil. Mpaka hivi Jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili kufahamu undani zaidi na watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
Kufuatia tukio hilo na mengine ya nyuma Kamanda Sabas alizidi kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kwa jinsi wanavyoonyesha ushirikiano kwa jeshi hilo juu ya kufichua vitendo vya uhalifu na wahalifu na kuahidi kuendeleza falsafa ya Polisi Jamii ambayo inaleta mafanikio makubwa katika suala zima la kuimarisha amani na utulivu Mkoani hapa.
View detail

MWAKYEMBE AWATAMBULISHA RASMI KATIBU MKUU NA NAIBU WAKE KTK WIZARA YA UCHUKUZI

DSC_0847
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jioni katika mkutano maalum wa kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(kulia kwa Waziri Mwakyembe)na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(kushoto kwa Waziri Mwakyembe Katika ukumbi wa Karimjee,jijini Dar es Salaam.
DSC_0854
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs Monica Mwamunyange akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo. Mkutano huo umefanyika leo jioni katika ukumbi Karimjee jijjini Dar es Salaam. Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo amesisitiza ushirikiano na kujiwekea malengo katika utendaji kazi wa kila siku.
DSC_0842
Sehemu ya Watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Shaaban Mwinjaka(Hayupo pichani) wakati wa mkutano maalum wa kufunga mwaka na kuwatambulisha rasmi viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
DSC_0838
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Dk. Shaaban Mwinjaka (wa tano kutoka kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs Monica Mwamunyange (wa nne kutoka kushoto) na Watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi leo alipokutana nao ili kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na watumishi.
DSC_0861
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(wa kwanza kulia mstari wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa WIzara hiyo.
DSC_0873
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(wa tatu kutoka kulia mstario wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange (wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na baadhi ya watumishi wa  Wizara ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa Wizara hiyo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Uchukuzi).
View detail

BEI MPYA ZA UMEME ZATANGAZWA RASMI NA EWURA KUANZIA TAR 1/01/2014

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.

Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.

Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa 
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.

Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).

USHIRIKISHWAJI WA WADAU

Kulingana na Kifungu Na. 19(2) (h) cha Sheria ya EWURA, Mamlaka ilifanya Taftishi ili kupata maoni juu ya ombi la kurekebisha bei za umeme. Ukusanyaji wa maoni ulihusisha pia mikutano minne (4) iliyofanyika Iringa na Shinyanga tarehe 15 Novemba 2013, Bagamoyo tarehe 20 Novemba na kuhitimishwa Dar es Salaam tarehe 22 Novemba 2013. Aidha, tarehe 6 Desemba 2013, EWURA iliitisha mkutano wa mwisho wa wadau wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini(MEM), TANESCO, Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania, Baraza la Watumiaji na Baraza la Ushauri la Serikali, Umoja wa Wazalishaji wa Saruji wa Afrika Mashariki, na kiwanda cha ALAF. Katika mkutano huo EWURA iliwasilisha mwelekeo wa maamuzi kuhusu maombi ya TANESCO na namna zilivyokokotolewa. Wadau walipewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu mwelekeo wa bei na maoni yao yamezingatiwa katika kufikia maamuzi ya mwisho.

UCHAMBUZI NA UAMUZI

Kwa kufuata sheria na kanuni zinazoelekeza kuhusu uchambuzi wa bei ya umeme, EWURA ilifanya uchambuzi wa kifedha na kiufundi ili kubaini uwezo wa TANESCO katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Uchambuzi uliangalia utendaji wa Shirika la TANESCO katika miaka iliyopita na pia iliangalia majukumu yanayoikabili TANESCO katika miaka mitatu ijayo. EWURA imebaini kwamba hali ya kifedha ya Shirika la Umeme sio nzuri. Shirika limeendelea kupata hasara, ambayo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 47.3 katika mwaka 2010 na kufikia shilingi bilioni 223.4 mwishoni mwa mwaka 2012. Pamoja na mapungufu ya kiufanisi, sababu kubwa ya ongezeko la hasara ni kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa umeme ambao TANESCO inanunua kutoka kwa wazalishaji binafsi. Hali hii imelifanya shirika kushindwa kulipa madeni yake ya muda mfupi na ya muda mrefu, ambayo yamelibikizwa na kufikia TZS 456.8 bilioni tarehe 22 Novemba 2013, hali ambayo inatishia uendelevu wa huduma ya umeme hapa nchini.

Mamlaka imetumia Kanuni ya Ukokotoaji wa Bei kama ilivyopendekezwa na AF-MERCADOS wakati wa kukokotoa mahitaji ya mapato ya TANESCO. Kanuni hiyo inawezesha kukokotoa bei zinazolandana na gharama halisi kwenye mfumo wa umeme na kuzigawa kwenye makundi ya watumiaji umeme, kadiri kila kundi linavyosababisha gharama kwenye mfumo wa umeme kwa mujibu wa mahitaji ya Sheria ya Umeme ya 2008 Kifungu cha 23(2)(f).

EWURA imejiridhisha kwamba, ufumbuzi wa matatizo ya kifedha ya TANESCO, unahitaji njia/mikakati miwili itekelezwe kwa pamoja:
kuongeza bei ya umeme ili kufikia bei inayokidhi gharama halisi (Cost Reflective Tariff); na
TANESCO kupata mkopo wa gharama nafuu ama ruzuku kutoka Serikalini ili kulipa limbikizo la madeni ya Shirika.

Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, katika kikao chake cha tarehe 10 Desemba 2013 pamoja na mambo mengine, ilitoa maamuzi ya ongezeko la bei za umeme kwa viwango mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya wateja, kama ifuatavyo:

Kundi D1: Hili ni kundi la wateja wadogo wa majumbani, hasa vijijini, ambao hutumia wastani usiozidi wa Uniti 75 kwa mwezi. EWURA imeongeza wigo wa mahitaji ya umeme na kufikia uniti 75 kwa mwezi, lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wateja wa TANESCO wanaoweza kulipa kidogo kwa matumizi ya umeme kwa kiwango hicho, na pia kuwahamasisha kutumie zaidi umeme. Awali kundi hili lilikuwa linatunia wastani wa matumizi ya uniti 50 kwa mwezi. Bei mpya ni shilingi 100 kwa uniti moja, kutoka shilingi 60 za sasa, sawa na ongezeko la shilingi 40.

Kundi T1: Hili ni kundi la watumiaji wakubwa wa umeme majumbani, biashara ndogondogo, mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani, mabango n.k. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 306 kwa uniti moja, ikiwa ni ongezeko la Shilingi 85 ya bei ya sasa. TANESCO ilipendekeza ongezeko la shilingi 131.

Kundi T2: Hili ni kundi la watumiaji umeme wa kawaida ambao hupimwa katika msongo wa volti 400, na ambao matumizi yao ya wastani kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500 wateja wafanyabiashara kubwa, viwanda vya kati. Bei ya nishati iliyoridhiwa ni shilingi 205 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 73 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 145 ya bei ya sasa.

Kundi T3-MV: Hili ni kundi la wateja wakubwa kama viwanda vikubwa waliounganishwa katika msongo wa kati (Medium Voltage). EWURA imeidhinisha bei ya nishati kwa kiwango cha shilingi 166 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 45 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 148 kwa uniti moja.

Kundi T3-HV: Hili ni kundi la wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa juu (High Voltage – Voti 66,000 na zaidi) ikiwa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 159 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 53 la bei ya sasa. TANESCO waliomba ongezeko la shilingi 80 kwa uniti moja.

Bei ya umeme itakuwa inarekebishwa kila baada ya miezi mitatu kulingana na mabadiliko ya kiwango na bei za mafuta; mfumuko wa bei, mabadiliko ya thamani ya fedha, na upatikanaji wa ruzuku toka Serikalini.

Vilevile, TANESCO inatakiwa kutekeleza miradi ya uwekezaji iliyoainishwa kwa kutumia fedha zitakazokusanywa kutokana na bei zilizoidhinishwa. EWURA inaweza kurekebisha bei ya umeme ya TANESCO kila mwisho wa mwaka 2014 na/au mwaka 2015 endapo TANESCO itashindwa kutekeleza miradi iliyotajwa katika Jedwali husika. Marekebisho hayo yatatokana na makadirio ya gharama za miradi ambayo haikutekelezwa.

Kutokana na matazamio ya kuwa na mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa umeme (generation mix) katika mwaka 2015 na kuendelea, kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa kwa upatikanaji wa gesi asilia, EWURA itafanya utafiti kubaini gharama halisi (Cost of Service Study) ya huduma ya umeme kwa wakati huo. Hivyo, bei zilizoidhinishwa zitatumika mpaka mwaka 2016, kama utafiti unaotazamiwa kufanywa hautakamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015.

EWURA ililinganisha bei za umeme kwa kila Uniti, katika nchi za Afrika ya Mashariki, na kuona kuwa bado bei za umeme za Tanzania zipo chini ukilinganisha na bei za katika nchi jirani kama inavyoonyeshwa hapa chini, kwa makundi mbalimbali ya watumiaji umeme.

Pamoja na maamuzi hayo, Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, pia iliagiza TANESCO kutekeleza yafuatayo:

  • kuzalisha umeme kwa kutumia mitambo yenye gharama nafuu ("least cost merit order") na kuwasilisha ripoti kwa Mamlaka katika kila mwezi ikionyesha uzalishaji halisi na mpango wa uzalishaji kama ilivyoidhinishwa na EWURA;

  • kuhakikisha kuwa zabuni za miradi ya uzalishaji umeme zinatolewa kulingana na mahitaji kama ilivyoidhinishwa kwenye Mpango wa Umeme wa Taifa (Power System Master Plan). Miradi yote mipya lazima ipatikane kwa njia ya ushindani kwa kufuata Sheria ya Umeme, "Public Private Partnership Act", Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni husika;

  • kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu viashiria vya takwimu za ubora na uhakika wa umeme (supply and reliability) katika misongo ya 11kV, 33 kV, 66 kV, 132 kV, na 220 kV kwa kila mkoa kwa ajili ya uhakiki. Takwimu husika zinatakiwa kuonyesha jumla ya masaa mteja aliyokosa umeme kwa kila njia ya umeme ("feeder"), kukosekana kwa umeme kulikopangwa (planned outages), na ambao haukupangwa (unplanned outages), idadi ya matukio ya kukosa umeme katika kila "feeder", idadi ya wateja wanaohudumiwa na kila "feeder", idadi ya wateja walioathirika na katizo la umeme katika kila "feeder" na kiasi cha umeme kilichokosekana kutokana na katizo hilo (total unserved energy in kWh);

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, katika kipindi cha miezi mitatu baada kuanza kwa Agizo hilo la Mamlaka, mpango wa utekelezaji wa "Demand Side Management Programme" ili uidhinishwe;

  • kupunguza kiwango cha upotevu wa umeme (technical and non-technical losses) katika mtandao wa usambazaji kutoka asilimia 19 ya mwaka 2012 hadi asilimia 15.1 ifikapo mwisho wa mwaka 2015;

  • kubuni mikakati ya kupambana wizi wa umeme utokanao na uunganishaji umeme usio halali, na kuondoa ucheleweshaji usio wa lazima katika kutunganisha wateja wapya;

  • kuhamisha wateja walio katika kundi la D1 kwenda T1 endapo matumizi yao ya mwezi yatazidi uniti 75 kwa miezi mitatu mfululizo;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi, 2014, Mpango wa kuwawekea wateja wake mita za LUKU na AMR ili kupunguza wateja wanaotumia mita za zamani (conventional meters);

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kila baada ya miezi mitatu, taarifa/ripoti ya ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wateja wake ili kuongeza mapato ya Shirika;

  • kutoa elimu kwa wateja wake kuhusu haki na wajibu wa wateja kwa mujibu wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja na kushughulikia kero za wateja kama inavyoelekezwa katika Mkataba husika na Kanuni za Umeme;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, maombi ya marekebisho ya bei yatokanayo na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na ubadilikaji wa thamani ya fedha; Ukokotoaji wa marekebisho hayo utakuwa kama ulivyoainishwa katika Kanuni za Kupanga Bei za Umeme za mwaka 2013 (Electricity (Tariff Setting) Rules, 2013);

  • kuendelea kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu hali ya kifedha na kiundeshaji. Taarifa hizi zitatumiwa na Mamlaka katika kutathmini utendaji wa TANESCO ikilinganishwa na mashirika mengine ya umeme katika nchi jirani ili kuboresha utendaji wake. Tathmini hii pia itatumiwa na Mamlaka katika kubaini uhalali wa maombi ya baadae ya kurekebisha bei;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi 2014, mpango wa utekelezaji wa kila sharti katika Agizo la EWURA.

Bei mpya za umeme zitaanza kutumika tarehe 1 Januari 2014. Ni matarajio ya EWURA kwamba TANESCO watatumia fursa hii kutoa huduma bora zaidi za umeme na kuhakikisha kuwa wanashughulikia malalamiko ya wateja kila yanapojitokeza ili kurejesha imani kwa Shirika la Umeme la TANESCO.
View detail

Monday, December 23, 2013

YANGA WAOMBWA KUA WATULIVU

yusufsanga
Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga.
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
“Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea” alisema Manji.
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.

Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi  majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.
Habari kwa hisani ya Youngafricans.co.tz
View detail

ALICHOKISEMA ZITTO AKIWA KIGOMA HIKI HAPA

DSC_0018
Mh. Zitto Kabwe baada ya kutua Uwanja wa Ndege mjini Kigoma akilakiwa na baadhi ya viongozi wa Chadema mjini Kigoma.
Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji. Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.
DSC_0008
Umati wa wafuasi wa Chadema waliojitokeza kwenye uwanja mdogo wa Ndege Kigoma kumpoke Mbunge wao. 
Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini Ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa Ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa Ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na Jimbo la Kigoma Mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995. Kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994. Wakati Watanzania wengine wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyoanzishwa, watu wa Ujiji, watu wa Kigoma hamkusita kupokea mabadiliko. Wengi wamepoteza maisha yao, wengine kazi zao na wengine hata ndoa zao katika kupata mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu. Nawataka msichoke. Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha demokrasia katika nchi yetu haijaisha na inahitaji uvumilivu, kusameheana na kuaminiana.
DSC_0032
Pichani juu na chini ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh. Zitto Kabwe akiwapungia na kusalimiana na wapiga kura wake waliojitokeza kumlaki kwenye uwanja wa ndege mara baada kuwasili mjini Kigoma leo.
DSC_0033
Na nchi yetu Tanzania ni nchi inayoonyesha uwezo mkubwa katika kupendana, kuaminiana, kuvumiliana na hata kusameheana. Na haya si maneno tu ambayo ninayazungumza kama mwanasiasa. Hii ni hali halisi na maisha niliyoyaishi kwa mifano nilipokuwa ninakua na kusoma katika shule ya Msingi Kigoma na baadaye Shule ya Sekondari Kigoma. Malezi yangu yalikuwa yanaongozwa na jamii nzima ya Kigoma. Nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu niliokutana nao kwenye masomo na kwenye siasa kwamba nimeanza kuvaa viatu kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la tatu. Viatu hivyo viliitwa ‘asante Salim’ vilivyokuwa vinatengenezwa na Kampuni ya Bora Shoes. Vililinunuliwa na mama Coretha Furugunya ambaye tulikuwa tunakaa mtaa mmoja wa Kisangani Mwanga. Mama Coretha hakuninunulia viatu kwa sababu alikuwa ana uwezo mkubwa, la hasha! Alifurahishwa na matokeo yangu ya mitihani ya darasa la pili kwenda la tatu. Ninaamini kitendo cha mama huyu ni ushahidi wa uungwana, upendo na hata uwajibikaji ambao tunao sisi watanzania. Uwajibikaji kwani alichukua jukumu kunilea ingawa hakuwa mzazi wangu, lakini aliona kuwa kama mwanajamii ana nafasi kubwa katika kuwaendeleza watoto wote. Jamii hii ya watu wa Kigoma ilinifunza kuwa nikijitahidi na kukazana kwa bidii kwenye masomo na majukumu, nitafanikiwa. Siwezi kusahau somo hili katika maisha yangu na ni somo hili ndilo limenifanya nijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuwatumikia kwa uadilifu na mafanikio ya hali ya juu sana.
DSC_0048
Wanakigoma wakiusindikiza msafara wa Mh. Zitto Kabwe  kutokea Uwanja wa ndege.
Nikiwa nimejaa matumaini haya kuhusu wananchi wenzangu, leo nataka niwakumbushe kwa nini kama jamii tulichagua kufuata njia ya demokrasia. Demokrasia ina maana pale ambapo inatumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wananchi. Maisha yanayotakiwa ni yale yanayomwezesha mwananchi kupata huduma zake stahili kama Elimu, Afya, Maji na miundombinu. Demokrasia haina maana pale wananchi wanakufa njaa kwa kukosa ajira na kukuza umasikini. Demokrasia inahusu maendeleo. Tumejitahidi kwa upande wetu kuondoa mkoa wa Kigoma kutoka mikoa isiyo na miundombinu kabisa ya maendeleo mpaka kuwa mkoa unaotumika kama mfano kwa miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo Daraja la Malagarasi, Uwanja wa ndege wa Gombe-Mahale, barabara za lami na upanuzi wa Bandari, ujenzi wa bandari ndogo mpya na ujenzi wa kituo cha Usafirishaji Mwandiga. Asije mtu akasema yeye ndio kafanya haya. Haya ni matunda ya nyinyi watu wa Kigoma kupokea demokrasia na bila woga kuchagua viongozi wenu bila kujali vyama bali kwa kuangalia uwezo. Haya ni matunda ya viongozi wenu kupaza sauti yenu kwenye baraza la Taifa, Bunge. Haya ni matunda ya uvumilivu wenu na uamuzi wenu wa kutaka maendeleo. Juhudi hizi lazima ziendelezwe kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa nafasi ya mkoa wa Kigoma katika uchumi wa Tanzania inaonekana dhahiri na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa kituo cha biashara katika nchi za maziwa makuu.
DSC_0067
Maandamano yakitokea uwanja wa ndege huku wengine wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali.
DSC_0059
Lakini tukumbuke pia kuwa Demokrasia ni Uwajibikaji. Katika kipindi cha utumishi wangu kwenu,kutokana na malezi niliyoyapata kutoka kwenu,nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Serikali inawajibika kwa Wananchi. Nakumbuka wakati napambana kuhusu sheria mbovu ya madini kuna watu hapa nyumbani walisema ‘sasa huyu kawa mbunge wa Taifa’ lakini watu wengi zaidi wakasema tumemtuma Dodoma kusemea Watanzania wote na sio Kigoma tu. Tuliweza ndani ya miaka mitano kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye sera ya Madini na sheria ya madini ambapo baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayafikiriki sasa yametungiwa sheria ikiwemo Serikali kuwa na hisa kwenye migodi, Tanzanite kumilikiwa na Watanzania sio chini ya asilimia 50 na kuzuia kabisa wageni kuchimba vito vya thamani. Uwajibikaji ulipelekea kumshinikiza Rais kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri kwa kuwafukuza mawaziri wanane mwaka jana. Hii ilitokana sio tu na hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bali pia ushiriki mkubwa wa wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii ambapo wabunge walishinikizwa kuweka saini kwenye karatasi za kumtoa Waziri Mkuu. Toka wakati huo kumekuwa na utaratibu sasa ambapo wabunge hawaoni taabu kutaka uwajibikaji waziwazi ili kuzuia ubadhirifu wa fedha za Umma. Ni hivi jana tumeshuhudia mawaziri wanne wamejiuzulu na kufukuzwa kazi kutokana na kashfa ya operesheni Tokomeza ujangili iliyoibuliwa na ripoti ya kamati ya bunge. Mabadiliko haya ni hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia yetu.
Pamoja na matunda haya mengi mazuri lakini bado kuna changamoto katika juhudi zetu.
DSC_0119
Changamoto kubwa tuliyonayo wananchi ni kukosekana kwa imani katika demokrasia yetu.
Kutoaminiana. Ni dhahiri kuwa kutoaminiana katika nchi yetu kumekuwa kwa kiasi kikubwa. Taarifa za kitafiti zinaonyesha kuwa katika kila Watanzania kumi, wanane hawaaminiani. Ni changamoto kubwa sana. Wananchi wameacha kutuamini wanasiasa na wanasiasa wameacha kuaminiana wenyewe kwa wenyewe. Hivi sasa uongo umegeuzwa kuwa ukweli na ukweli umekuwa ni uongo. Hivi sasa ukitaka kuwa mwanasiasa maarufu inabidi ujue kudanganya na ukitaka kuitwa mwanasiasa msaliti inabidi uwe msema kweli. Kukosekana kwa uaminifu na kuaminiana imekuwa ni kansa katika siasa zetu. Itachukua muda mrefu sana kujenga demokrasia imara katika nchi yetu kama hatutapata jibu la changamoto hii ya kutoaminiana na kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Hivi sasa ukweli umekuwa unatengenezwa badala ya kutafutwa. Ni majanga! Juzi bungeni Mwanasheria Mkuu wa Serikali alielekeza shutuma kwangu kwamba sikushirikiana na kamati maalum iliyoundwa na Bunge kufuatilia mabilioni ya uswisi na kwamba chini ya kiapo nilisema sina majina ya watu wenye akaunti huko Uswisi. Huu ulikuwa ni uongo. Ni uongo kwa sababu niliitika wito wa kamati hata nilipokuwa katika mafunzo ya mgambo huko Tanga na nilikutana nao mara nne. Ni uongo kwa sababu niliwapa wajumbe wa Kamati Maalaum maelezo na taarifa nyingi sana kuhusu utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na umiliki wa mali nje ya nchi kinyumecha sheria. Ni uongo kwa sababu mimi kutotaja majina haya haina maana sina majina, bali ni kwamba ninaheshimu utaratibu na nimeachia vyombo husika vikamilishe uchunguzi. Kwani mimi kama mtu binafsi nikianza kuchukua majukumu ya taasisi ninaweza kutia dosari harakati hizi muhimu na hata kupelekea mchakato mzima kuvurugika. Sitaingia mtego huu! Lakini hatua hii ya Mwanasheria Mkuu imenipelekea kujiuliza maswali mengi kwa mfano uongo kama huu ulifanywa kwa malengo gani? Na ninajikuta hata mimi ninaingia katika hali ninayoilalamikia ya KUTOAMINIANA.
DSC_0067
Lakini mtambue pia kuwa kutoaminiana kunaleta kutovumiliana. Hivi sasa kuwa na mawazo tofauti katika vyama vya siasa au hata asasi za kijamii ni uhaini. Lakini bila kuenzi tofauti za mawazo hatuwezi kujenga vyama imara wala Taifa imara. Demokrasia imara ni zao la tofauti za mawazo na uhuru wa mawazo. Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyorutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo, tutajenga Taifa lenye watu wenye kuogopa na waliojaa woga. Wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta, lakini uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia. Bila demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa Taifa la kidikteta. Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo Taifa litaongozwa.
DSC_0178
Demokrasia bila kuaminiana, demokrasia bila kuvumiliana sio demokrasia ya kweli.
Juzi nilipoingia Bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanayoendelea ndani ya chama chetu nilikaa pamoja na mbunge Tundu Lissu. Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo. Hii ni kwa sababu sina chuki na mtu yeyote yule. Mmenifunza kutojenga chuki na watu na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha. Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti na hatimaye kutafuta suluhu ya pamoja. Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tunasahau kwa maksudi. Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha ya wananchi na sio malumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa. Siasa si kuwekeana chuki na kuonyeshana ubabe.
DSC_0585
Na hapo ni muhimu muelewa wanaKigoma mnapoambiwa kuwa eti ninapofuatilia mabilioni ya Uswisi ninatafuta umaarufu, ni uongo! Mnaposikia eti kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki na kujitafutia umaarufu, ni uongo! Kinachonisukuma kufanya vyote hivi ni ninyi. Ninasukuwa kila ninapowaona watoto bado wanatembea bila viatu;kila ninapoona akina mama wanapoteza maisha yao katika uzazi;kila ninapoona vijana ambao hawana uhakika wa kupata hata mlo moja kwa siku kwa kukosa kazi; ninapoona wazee wa Kigoma kukosa hata shilingi mia moja kununua chai asubuhi. Ninawaona si wanaKigoma bali mamilioni ya watanzania wakiishi katika hali hii. Alafu nalinganisha na taarifa tunazozipata kuhusu ufujaji na utoroshwaji wa pesa zetu. Hebu sasa linganisheni na ukweli kuwa ripoti ya kimataifa iliyotolewa hivi karibuni imeonyesha kuwa mwaka 2010 pekee, jumla ya dola za kimarekani milioni 1315 (bilioni 1.3), yaani shilingi trilioni  2,113,930,000,000 (sh trilioni 2.1) zilitoroshwa kutoka nchini Tanzania. Mwaka 2011 kiasi cha dola za kimarekani milioni 817 yani shilingi za kitanzania zipatazo trilioni 1,315,370,000,000 (trilioni 1.3) zilitoroshwa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa jumla ya fedha za Watanzania zilizotoroshwa nje ya nchi katika miaka kumi iliyopita zilifikia dola za kimarekani milioni 4526 (bilioni 4.5) sawa na shilingi za kitanzania trilioni 7,286,860,000,000 (trilioni 7.3).  Nimewatajia hapa namba chungu nzima na matrilioni na mabilioni hayaleti maana. Lakini hii ina maana kwamba kiasi cha pesa zilizotoroshwa katika miaka 10 pesa – robo yake tuingeweza kujenga barabara ya lami ya kiwango cha juu kabisa kutoka Kigoma mpaka Dar-es-salaam! Pesa hizi zingeweza kuajiri na kuwalipa vizuri walimu, madaktari na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha tunapata huduma bora na kutengeneza ajira bora kwa vijana wetu. Pesa hizi zingeweza kununua madawa muhimu na kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama tunaowapoteza kila mwaka wakati wa uzazi. Pesa hizi zingeweza kuwanunulia watanzania wote si watoto tu angalau pea 10 ya viatu. Sasa nikitafakari haya siwezi kuchapa usingizi mnono na kufumbia macho utoroshwaji wa fedha au matumizi mabaya ya fedha za umma kwa njia ya sisi wabunge kujilipia posho! Hapana! Nafsi yangu hainiruhusu kukaa kimya kwa kuogopa kuitwa mbinafsi au msaliti!
z
Lakini naomba niwasihi kuwa katika nyakati kama hizi za changamoto za kisiasa jambo la msingi kuliko yote ni kutulia maana hakuna linalotokea bila sababu. Licha ya kwamba kuna watu wengi wanapaza sauti zao katika mambo haya lakini pia kuna wengi zaidi ambao wapo kimya lakini wana mawazo yao, ndani na nje ya chama chetu;ndani na nje ya Serikali na ndani nanje ya nchi yetu. Ndio maana lazima kuibadili nchi yetu ili kuweza kuhakikisha kila raia anakuwa na fursa ya kutoa mawazo na fikra zake zinakuwa huru.
zitto
Maisha ni mabadiliko; mabadiliko hayana ukomo; mabadiliko hayazuiliki kwa sababu bila mabadiliko hakuna ukuaji, bila mabadiliko hakuna maendeleo. Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop