Welcome to our online store Portal

Template Information

Saturday, November 30, 2013

WARAKA WA CHADEMA WAGUBIKWA NA UTATA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Utata mkubwa umeibuka kuhusu waraka halisi wa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ uliosababisha Zitto Kabwe kuvuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Novemba 20 - 22, mwaka huu.
Baada ya juzi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika kuwaeleza wanahabari kuwa waraka uliochapishwa katika magazeti na mitandao ya kijamii, siyo halisi, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba amejitokeza na kuutetea huku akidai kwamba huo unaodaiwa na uongozi kuwa ndiyo halisi umeghushiwa.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alivuliwa uongozi pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na Mwigamba kutokana na madai ya kuandaa waraka huo ambao Chadema kimesema ulikuwa unaeleza mbinu za uasi za viongozi hao ambazo zingetumika wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho jambo ambalo ni kinyume na katiba, sheria na itifaki zake.
kuna njama zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa Chadema ili kuubadili waraka halisi wa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ kwa lengo la kupoteza maana yake, huku akisisitiza kuwa waraka halisi hauna tatizo lolote.
Katika madai yake, Mnyika alisema waraka huo unaosambazwa na kuchapishwa, si ule uliowasilishwa na kujadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu na kuahidi kuutoa waraka halisi ambao una mambo makubwa na mengi zaidi.
“Waraka utakaotumika katika mashtaka yao siyo huo. Sisi tutautumia ule ambao uliwasilishwa katika Kamati Kuu ambao una mambo makubwa na mengi zaidi kuliko huo unaochapishwa sehemu mbalimbali, ikibidi tutautoa huo waraka halisi,” alisema.
Hata hivyo, jana Mwigamba alisema waraka halisi ni ule ambao upo katika kompyuta mpakato (Laptop) aliyonyang’anywa na wanachama wa Chadema, Oktoba 25, mwaka huu, katika mkutano mjini Arusha.
“Waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika magazeti ya jana (juzi), pamoja na nakala iliyopo katika mtandao wa kijamii wa Jamii Forums.”
Aliongeza: “Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndiyo wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye kompyuta yangu kwani waraka huo uliibwa kutoka katika kompyuta hiyo ambayo nilirudishiwa baada ya wao kuikagua na kukuta waraka huo halisi.”
Mwigamba alisema waraka wake unatofautiana kwa kiasi kikubwa na ule ambao Chadema kinasema kuwa ndiyo halisi: “Lissu na wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu, lakini wamekwama.”
Alisema kuandaa waraka huo siyo uhaini kama ambavyo imekuwa ikielezwa na viongozi wa Chadema na kusisitiza kuwa ni waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama hicho uliopangwa kufanyika Desemba mwaka huu na baadaye kusogezwa hadi Juni mwakani.

“Wakati wa uchaguzi si ajabu kuwepo kwa wanachama wanaounga mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa miaka mingi, najua hata yeye ana mikakati na wanaoshiriki mkakati wake ni Lissu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema,” alisema.
Alisema anashangazwa kwa kitendo cha Chadema kuusambaza waraka huo, wakati ulikuwa ni mpango wa siri kati yake, Dk Kitila pamoja na mtu mwingine anayetajwa kwa jina la M2.
“Baada ya kugundua madhara ya kusambaza ovyo waraka huo, sasa wameamua kuukana, waraka wangu ni sahihi na unaeleza ukweli. Binafsi nimefanya kazi ofisi ya makao makuu ya chama kama Mhasibu Mkuu ningeweza kuanika mengi lakini sijafanya hivyo kwa masilahi ya chama,” alisema na kuongeza:
“Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Zitto na tangu siku nyingi walipanga kumfukuza. Nawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama. Zitto hahusiki na mkakati huu pamoja na kwamba alikuwa ndiye mhusika mkuu, alikuwa hajui lolote.”
Jumamosi iliyopita, mama yake mzazi Zitto, Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema waraka huo ulikuwa umeongezwa maneno.
“Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya baadhi ya wanachama kumpora Mwigamba `laptop’ yake alipokuwa mkoani Arusha katika kikao cha Chadema,” alisema bila kutaka kufafanua ulibadilishwa vipi, licha ya kuwataja kwa majina waliohusika kuubadili wakiwamo wabunge wawili wa chama hicho na viongozi wa ngazi za juu.

Kuhusu hatima yake ndani ya Chadema, Mwigamba alisema hana mpango wa kuondoka hata baada ya kuvuliwa uongozi, huku akisisitiza kuwa hakusudii kuomba radhi kutokana na kuandaa waraka huo.
Alisema hakusudii kuhama kwa kuwa ana historia ndefu na Chadema na anaamini kuwa ndicho mkombozi wa Watanzania.
“Nimekuwa kiongozi wa kata, wilaya, mkoa hadi taifa. Nimetumia muda wangu mwingi na hata kuhatarisha maisha yangu kwa ajili ya chama hiki, siwezi kuondoka kutokana na tofauti za kimitazamo na viongozi wangu,” alisema.
Mwigamba, ambaye alikuwa mfanyakazi katika Mahakama ya Kimataifa inayosikiliza Kesi za Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (ICTR) na baadaye kujiondoa ili ajikite kwenye siasa, alisema ana imani yanayotokea sasa katika chama hicho yatapita salama.
View detail

CHADEMA WAPEWA ONYO NA PROF. BAREGU

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.
“Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani  viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama,” Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.
Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.
Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.
“Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.”
Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.
Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.
“Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao  ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho,” alisema na kuongeza:
“Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.”
Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.
“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.”

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare alisema chama hicho kipo imara na hakiwezi kuyumba kwa sababu ya uamuzi huo.
Lwakatale ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alisema: “Mfumo wa ulinzi ndani ya chama upo imara, yakitolewa maelezo na ngazi za juu kinachofuata baada ya hapo ni utekelezaji.”
Alisema kilichotokea ni kitu cha kawaida na ni mwanzo wa chama kujiimarisha.

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu na Baraza Kuu la Chadema hicho Wilaya ya Temeke wamepinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu ya kuwavua nyadhifa viongozi hao.
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Temeke, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, Joseph Patrick aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mgogoro huo haulengi kujenga chama, bali unakibomoa.
“Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia uchaguzi wa ndani. Hii inasababisha kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika kwa lengo la kuwadhoofisha mbele ya wanachama,” alisema na kuongheza:
“Tumeona mifano mingi ya namna hii. Wakati Chacha Wangwe akiwa hai alipotangaza kuwania uenyekiti, mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote na hakuwahi kusemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama, bali viongozi wenzake waliotofautiana kimsimamo.”
Alisema hali hiyo ilijitokeza pia kwa Zitto alipotangaza kuwania uenyekiti kama ilivyokuwa wakati wa chaguzi za viti maalumu na mabaraza ya chama.
Alisema ni vyema viongozi wakaitisha mkutano mkuu wa dharura na kuwaeleza wanachama mambo mbalimbali ikiwamo ni kwa nini wameamua kusambaza waraka ambao alisema unakidhalilisha chama badala ya waliouandika.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Herry Kilewo amehojiwa na Polisi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na madai ya Zitto kutishiwa kuuawa.
Katika mahojiano hayo, Kilewo aliongozwa na Mwanasheria wake, Mussa Mfinanga, Mwanasheria wa Chadema John Malya na pia alikuwapo Diwani wa Ubungo, Boniface Jacob. Mfinanga alisema Novemba 11 mwaka huu, chombo kimoja cha habari kiliripoti kuwa Zitto ametishiwa kuuawa na mteja wake Kilewo.
Mfinanga alisema baada ya madai hayo, Jeshi hilo lilimwita Zitto kutoa maelezo yake na kisha kuona haja ya kumhoji Kilewo shutuma hizo. Alisema mteja wake amejidhanini mwenyewe na yupo nje kwa dhamana bila ya masharti yeyote.
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alikiri kuhojiwa kwa Kilewo akisema ni kawaida kwa jeshi hilo kumuita mtu na kumhoji kwa mujibu wa taratibu na sheria zake.
View detail

Friday, November 29, 2013

WATU WAWILI WAFARIKI SINGIDA KTK MATOKEO TOFAUTI

DSC04171 (1)
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP. Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya matukio ya kuuawa watu wawili mkoani Singida, likiwemo la Egila Petro kumpiga kwa fimbo mama mkwe wake mwenye umri wa miaka 80 na kusababisha kifo chake. Mmoja ampiga fimbo kichwani mkwewe, kisa amechoka kumlea

Watu wawili mkoani Singida wamefariki dunia kwenye matukio tofauti likiwemo la kikongwe mmoja mwenye umri wa miaka 80, kupigwa fimbo kichwani na mkwewe kwa kile kilichodaiwa kuwa mkwewe huyo, amechoka kumlea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP,Geofrey Kamwela, amesema Egila Petro (42) mkazi wa kijiji cha Mpora kata ya Iseke tarafa ya Nkoko wilayani Manyoni amempiga fimbo kichwani mama mkwe wake Doris Chiwiche na kumsababishia kifo chake siku tisa baadaye.
Amesema kikongwe huyo Doris alipigwa fimbo kichwani na Egila Novemba 18 mwaka huu saa nane mchana na alifariki Novemba 27 mwaka huu saa 12 asubuhi.

Kamwela amesema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa chini kwa chini kati ya Egila na mama mkwe wake Doris huku ikidaiwa kuwa Egila amekuwa akimshinikiza mumewe Benard Mdemu amwondoe mama yake huyo na kumpeleka kwa ndugu zake wengine kwa vile yeye amechoka kumlea.
Katika tukio jingine Kamanda Kamwela amesema John Liongo (37) mkazi wa Misuna Singida mjini amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kichwani na tumboni na watu wasiojulikana.

Amesema tukio hilo limetokea Novemba 27 mwaka huu saa 6.10 mchana huko katika kijiji cha Mnang’ana kata na tarafa ya Sepuka wilayani Ikungi.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu akiwa na watu wasiojulikana siku ya tukio aliondoka Singida mjini kwa gari ambalo bado halijajulikana namba zake za usajili Walipofika katika kijiji cha Mnang’ana waliingia porini na huko ndiko walipomuulia John”,alifafanua Kamwela. 

Kamanda huyo amesema katika eneo hilo la mauaji waliokota maganda watatu ya SAR na SMG ambayo risasi zake zilitumika kumuulia John.
“Niseme tu kwamba uchunguzi zaidi bado unaendelea kwa lengo la kuwabaini wauaji hao waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria”,amesema.
 
View detail

Dk. Nchimbi atoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo (SUA)

PIX 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpa cheti mwanafunzi Nuru Ally aliyefanya vizuri kuliko wanafunzi wote katika somo la Development Studies katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kilichopo mjini Morogoro. Mwanafunzi huyo pia alikabidhiwa zawadi ya Shilingi 50,000. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma SUA, Profesa Peter Gillah. (Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
PIX 2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri karika msomo mbalimbali wanaotarajiwa kufanya mahafali yao leo tarehe 29, Novemba 2013 katika chuo hicho.  Waziri Nchimbi alitoa vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika msomo mbalimbali chuoni hapo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Gerald Monela. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP) John Minja na Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Profesa Peter Gillah. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wapili kushoto aliyevaa tai) wakiwa katika picha ya pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri karika msomo mbalimbali wanaotarajiwa kufanya mahafali yao leo tarehe 29, Novemba 2013 katika chuo hicho.  Waziri Nchimbi alitoa vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika msomo mbalimbali chuoni hapo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
View detail

Mkutano wa Kitaifa wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi nchini wafunguliwa na Mulugo

001 NACTE
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo,akifafanuliwa jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)Dkt.Primus Nkwera(kulia)kabla ya kufungua mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi,Mkutano huo wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Arusha (AICC) jijini Arusha.
003 NACTE
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo,akiongea na wadau wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi,alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano  wa kwanza Kitaifa wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha wenye lengo la kujadili ubora wa mafunzo ya ufundi nchini.
004 NACTE
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi,wakijadiliana jambo  baada ya Naibu Waziri Philipo Mulugo kuzindua rasmi mkutano huo wa kwanza Kitaifa wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
005 NACTE
Washiriki wakiwa wamesimama ikiwa ni ishara ya kumkaribisha ya Naibu Waziri,Bw. Philipo Mulugo ambaye alikuwa mgeni rasmi kuzindua  mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi utakaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
005 NACTE 006 NACTE
Baadhi ya washiriki wanaoshiriki katika mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi unaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
007 NACTE
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo(katikati)akimshuhudia Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Ufundi(NACTE)Prof.B.L.M.Mwamila,akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani) cheti pamoja na Tuzo mara baada ya kukabidhiwa na Naibu waziri,wakati wa mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi  kwa utendaji bora kwa miaka mitatu mfululizo,Mkutano huo wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa  arusha (AICC) jijini Arusha.
008 NACTE
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo(kulia)akifurahia pamoja na  Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Ufundi(NACTE)Prof.B.L.M.Mwamila na ,mara baada ya kumkabidhi cheti pamoja na Tuzo ya heshima,wakati wa mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi  kwa utendaji bora kwa miaka mitatu mfululizo,Mkutano huo wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa  arusha (AICC )jijini Arusha.
009 NACTE
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo(katikati)akifurahia pamoja na  Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Ufundi(NACTE)Prof.B.L.M.Mwamila na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)Dkt.Primus Nkwera(kulia)mara baada ya kumkabidhi cheti pamoja na Tuzo,kwenye mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi  kwa utendaji bora kwa miaka mitatu mfululizo,Mkutano huo wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Arusha( AICC) jijini Arusha.
View detail

KINANA ASEMA VIONGOZI WA VYAMA TUACHE UMANGIMEZA KTK VYAMA KAMA KWELI TUNAHITAJI DEMOKRASIA YA KWELI NCHINI (TUKUBALI KUKOSOLEWA)

 
170
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana jioni ya jana, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini Tunduma, ambao umehudhuriwa na maelfu ya wananchi. Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, Kinana aliambatana na majenbe ya Chama cha Mapinduzi , Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro, Katika mkutano huo Kinana amesema wananchi kuikosoa CCM sio kosa kwani Chama hicho kimeingia mkataba na wananchi pale kilipopewa ridhaa ya kuongoza nchi ili kutekeleza ilani yake ya uchaguzi na ni haki ya mtu yeyote wakiwemo wapinzani ili kujua maendeleo yao, Amesema CCM haitakubali kuona ukiritimba na umangimeza wa baadhi ya watendaji Serikalini na unakwamisha maendeleo ya wananchi, ameongeza kuwa kazi ya CCM ni kutenda tu na kazi ya wapinzani ni kusema maneno tu.
2
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma.
3
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia maelefu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.
4
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amebebwa juujuu na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo.
5
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisakata muziki na wakina mama wana CCM kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
6
Wananchi wakisakata muziki kabla ya kuanza kwa mkutano.
7
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisakata muziki na wananchi.
9
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake akilekea katika eneo la mkutano.
10a
Msafara ukiwasili mjini Tunduma ukitokea wilayani Ileje.
11
Maelfu ya wananchi wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kianana hayupo pichani alipokuwa akiwahutubia.
12
Hapa akisisitiza jambo kwa wananchi hao wakati akitoa hutuba yake.
13
Mzee wa kimila wa kabila la wanamwanga wilayani Momba Jubeki Chipansia akimpa silaha za kijadi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kumsimika kuwa miongoni mwa wazee wa kabila hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tunduma jana jioni.
View detail

Thursday, November 28, 2013

GHARIB BILALI AMUHANI PHILIP MANGULA

  01.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam,jana jioni kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Peter Mangula, aliyefariki juzi asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili. Peter anatarajia kuzikwa kesho Ijumaa jijini Dar es Salaam.
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, marehemu Peter Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole.
03
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phili Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole. 
04
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji nyumbani kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phil Mangula,aliyefiwa na mtoto wake, Peter Mangula.
05
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam,jana jioni kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Peter Mangula, aliyefariki juzi asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili. Peter anatarajia kuzikwa kesho Ijumaa jijini Dar es Salaam.
06
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, marehemu Peter Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa ajili ya kumpa pole.
View detail

ZANZIBAR WAHIMIZWA FURSA ZA KIWANDA CHA SUKARI

 

000
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu kwenye mkutano wa hadhara wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika kwenye kiwanja cha michezo cha Mkaratini kilichopo ndani ya Jimbo lake la Kitope.
010
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia matukio yaliyokuwepo kwenye Mkutano wa Hadhara wa Wana CCM wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Hapo Kitope ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Haji Juma Haji.
992
Wana CCM walijikuta wakinengua wakati Kikundi cha burudani cha CCM Big Star kikifanya vitu vyake kwenye mkutano wa hadhara wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika kwenye kiwanja cha michezo cha Mkaratini kilichopo ndani ya Jimbo lake la Kitope.
(Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ). 

Wananchi wa Majimbo ya Donge, Kitope na Bumbwini yaliyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B” wameombwa kuitumia fursa na bahati waliyoipata ya uwepo wa kiwanda cha Sukari Mahonda ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nafasi za  ajira wakati kitakapoanza rasmi kazi zake za uzalishaji wa sukari.
Ombi hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa salamu maalum kwenye Mkutano wa hadhara wa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika katika uwanja wa michezo wa  Mkaratini ndani ya Jimbo lake la Kitope.

Balozi Seif amesema tabia ya baadhi ya watu kujaribu kufanya hujuma kwa kuchoma moto mashamba yaliyooteshwa miwa ya kiwanda hicho inaweza kuwafukuzisha wawekezaji ambao tayari wameshaonyesha nia ya kutaka kuwekeza vitega uchumi vyao hapa Nchini.
Alieleza kwamba wananchi wa Majimbo hayo wanapaswa kuwa makini pamoja na kukemea vitendo hivyo viovu ambavyo endapo vitaachiliwa kuendelea kufanyika katika maeneo hayo vitachangia kurejesha nyuma juhudi za Serikali kuu za kukaribisha wawekezaji wanaopewa nafasi ya kuwekeza ili kusaidia uchumi wa taifa pamoja na ustawi wa jamii.
“ Vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya wenzetu tunapaswa kuelewa kwamba hatuwatendei haki wawekezaji wetu waliojitolea kuweka vitega uchumi vyao hapa Nchini “. Alifafanua Balozi Seif.

Inasikitisha kuona kuwa zaidi ya ekari kumi na nane zilizooteshwa miwa kwa ajili ya usagaji wa sukari wakati utakapoanza uzalishaji tunaarifiwa kwamba zimeteketea kwa moto unaosadikiwa kuwa ni hujuma za makusudi “. Alionyesha Masikitiko yake Balozi Seif.
Aliwashauri wananchi hao kuwa walinzi wa miradi ya uwekezaji ambayo mingi kati yao huwanufaisha wananchi walioziunguukwa na miradi hiyo.

Akizungumzia suala la siasa Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mbunge wa Kitope aliwatahadharisha wana CCM na wanachi wote Nchini kutokubali kudanganywa na baadhi ya wanasiasa wenye sera zisizotekelezeka.
Amesema wanachokihitaji wananchi walio wengi nchini ni sera pamoja na kile wanachokihitaji kitekelezwe na Viongozi waliowachagua katika maeneo yao na si vyenginevyo.
Alifahamisha kwamba baadhi ya wanasiasa hivi sasa wamekuwa kero mitaani kwa tabia yao ya kuendeleza matusi na lawama kiasi kwamba zinakwenda kinyume na mfumo wa vyama vingi vya siasa lakini hata na maadili ya dini.
Aliwataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali yao yenye lengo la kuwaletea maendeleo kwa kujenga miundo mbinu itayotoa fursa ya kutanuka kwa huduma za Kiuchumi samba mba na kupunguza umaskini.

“ Tunapaswa tuangalie kwa makini tokea mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hadi leo Bara bara ngapi zilizojengwa  katika maeneo yetu. Sasa lazima tuelewe kwamba Zanzibar ni ya Wazanzibari  wenyewe na wao ndio watakaohusika katika kuijenga “. Alisisitiza Balozi Seif.
Aidha Balozi Seif alieleza kwamba lengo la Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha Muungao kwa faida ya watu wake wote.
Alifahamisha kwamba cheche ya ubaguzi inayoendelezwa na baadhi ya watu kwa kutaka kuvunja muungano haiwatendei haki Wazanzibari walio wengi wanaoishi upande wa Bara wa Muungano.

Amesema choko choko hizo zinaendelea kuchochewa wakati tayari wazanzibari hao wameshawekeza miradi kadhaa ya kiuchumi inayoweza kusambaratika kama fitina hiyo ikiachiliwa kuchomoza zaidi.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi alisisitiza na kuweka wazi kwamba msimamo wa Chama cha Mapinduzi uko wazi wa mfumo wa Serikali mbili ambazo ndio muhimili wa kuendelea kuwepo kwa Muungano uliopo hivi sasa.
View detail

NIDHAMU YA MATUMIZI YA FEDHA YAHIMIZWA KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI


DSC04577
Rais wa shirikisho la wachimbaji madini Tanzania (FEMATA), John Bina akifungua kikao cha kwanza cha kamati ya dhahabu ya FEMATA Taifa, kilichofanyikia mjini Singida.Wa kwanza kulia na mwenyekiti wa FEMATA Ahmed Adamu na kushoto ni Golden Hainga, katibu wa FEMATA.
DSC04568
Katibu wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Singida,Farijala Kiunsi akitoa taarifa yake ya utekelezaji katika kikao cha FEMATA.
DSC04583
Baadhi wa wajumbe wa mkutano wa FEMATA wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye kikao cha wachimbaji Dhahabu mkoani Singida.
DSC04593
Rais wa FEMATA Taifa, John Bina (wa pili kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pomoja na viongozi wa kitaifa wa FEMATA taifa waliohudhuria kikao mjini Singida.Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa FEMATA, Ahmed Adamu na kushoto ni katibu wa FEMATA,Golden Hainga.(Picha zote na Nathaniel Limu).

RAIS wa Shirikisho la wachimbaji madini Tanzania (FEMATA), John Bina, amewataka wachimbaji madini kujenga utamaduni wa kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ili fedha wanazozipata ziweze kuwaletea maendeleo endelevu.
 Bina amesema hayo wakati akifungua kikao cha kamati ya dhahabu ya FEMATA taifa, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya madini kanda ya kati mjini hapa.
 Amesema wachimbaji madini wamekuwa na sifa mbaya kwa madai kwamba, wengi hutumia fedha vibaya na kupelekea shughuli ya madini kutokuwanufaisha kimaisha.
 Bina amesema matumizi  hayo mabaya ya fedha, yana madhara mengi ikiwemo mhusika kufilisika mapema.
 “Uzoefu unaonyesha kwamba mchimbaji akipata kwa mfano shilingi milioni 10,kipaumbele chake kinakuwa ni  kuoga mwili kwa  pombe (bia), ataacha kuchimba madini na kutumbukia kwenye anasa hadi hapo fedha zitakapomwishia”,alifafanua Rais huyo.
 Kwa hali hiyo,Bina aliwataka wabadilike na kuwa na nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha, ili fedha wanazozipata ziwasaidie kujiletea maendeleo wao binafsi,familia zao,mkoa wao na taifa kwa ujumla.
 Katika hatua nyingine, Rais Bina aliwataka wachimbaji madini kujiepusha na uchimbaji haramu na pia wajenge utamaduni wa kulipa kodi, ili kujijengea mazingira ya kukopesheka na taasisi za kifedha.
 Wakti huo huo, kikao hicho kilimteua Farijala Kiunsi kuwa katibu wa FEMATA Taifa.
View detail

KINANA AELEKEA MOMBA BAADA YA KUTOKA ILEJE


1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akiongozana na Balozi Katiti wa shina namba moja la Kata ya Sange wilayani Ileje Mkoani Mbeya ambapo katibu mkuu huyo alizungumza na wanachama wa shina hilo na kumpongeza balozi kwa kazi nzuri ya kujitolea na kukijenga chama cha Mapinduzi, amewataka viongozi wote wa mikoa, wilaya na kata kuwatembelea mabalozi .Ili kuwapa moyo na kutambua umuhimu wa kazi zoa kwani hao ndiyo wenye wanachama lakini viongozi wa juu hawana wanachama kazi yao ni kuongoza na kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi inatekelezwa kwa mafanikio ili kuwapa maendeleo wananchi, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa..
238
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kushoto akipata maelezo ya Mkuu wa wilaya ya Ileje Rosemary Sinyamule wakati alipokagua daraja la mto Songwe katika mpaka wa Tanzania na Malawi mahali ambapo kunatakiwa kujengwa ofisi ya uhamiaji ili kurahisisha kazi za tasisi hiyo muhimu nchini, Wilaya ya Ilenje kata ya Isongole inapakana na kata na kijiji cha Mbilima wilaya ya Chitipa kwa upande wa Malawi 3 
Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kalembo kutokana na kushindwa kutembelea na kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Steven Kibona ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na kutumikia nchi kwa uadilifu mkubwa, Kinana amesema yeye na marehemu Steven Kibona waliwahi kufanya kazi wakiwa manaibu waziri wa Ulinzi na akasifu uadilifu wa marehemu Steven Kibona kushoto ni Mke wa marehemu Mama Kibona 4 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya 
 Kalembo
 5 
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kyela Bw. Mohamed Mwala wakati alipokuwa akitoa kero ya mbolea inayotengenezwa na kiwanda cha Minjingu ambayo inadaiwa na wakulima wa Ileje kuwa haina viwango na inasababisha mazao kuharibika. 6 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mke wa Marehemu Steven Kibona Mama Kibona kwenda kupata chakula cha mchana katika kata ya Kalembo leo mchana. 9 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakivuka daraja wakivuka daraja la mto Songwe wakati alipokagua daraja hilo hapo wanaingia upande wa
 Malawi.
 10 
Kikundi cha ngoma ya asili ya watu wa Ileje kikitumbuiza kabla ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuzungumza na wananchi katika kata ya Kalembo leo. 11 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ileje Rosemary Sinyamule wakati akitoa maelezo zaidi kuhusu uimarishaji wa miundimbinu ya Wilaya ya Ileje ili kurahisisha shughuliza kibiashara katika mpaka wa Tanzania na Malawi wakati alipokagua daraja la mto Songwe katika mpaka huo leo kulia ni Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifana kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh. Godfrey Zambi. 13 
Kutoka kulia ni wapiganaji Richard Mwaikenda wa Jambo Leo, John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa www.fullshangweblog.com na Laude Mwambona kutoka gazeti la Mwananchi wakivinjari katika mpaka wa Malawi na Tanzania wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua daraja hilo wapiganaji hao ni miongozi mwa wanahabari waliopo katika msafara huo. 14 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakirejea upande wa Tanzania.

  15 
Maofisa wa Idara ya Uhamiaji wakiwa katika ofisi yao iliyopo Isongole inadaiwa jengo hilo ni la kupanga

 16 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mkuu wa kituo hicho cha idara ya uhamiaji Isongole Bw. Fredrick Luhanga wakati alipotembelea katika ofisi hiyo. 17 
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwa amekaa na wanachama wa CCM katika shina namba moja Kata ya Sange. 18 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea nyumbani kwa balozi 19 
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kmataifana akishiriki ujenzi wa msingi wa jengo la kituo cha afya cha Lubanda 20 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa msingi wa jengo la kituo cha afya cha Lubanda leo 22 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Bi Sylivia Siriwa
 
 
 
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop