Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, March 31, 2014

MAREKANI NA URUSI UTATA MTUPU

http://azizicompdoc.blogspot.com/
John Kerry akutana na Serguei Lavrov kuhusiana na taharuki kuhusu Ukraine
Waziri wa mashauri ya Nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, amesema kuwa hakuna makubaliano yaliyoafikiwa baina yake na mwenzake kutoka Urusi Sergei Lavrov, katika mkutano wa
Marekani inasisitiza kuwa hatua ya urusi kutwaa eneo la Crimea baada ya kura ya maoni sihalali.
Bwana Lavrov ametoa masharti makali yasiyoegemea upande wowote huku akitaka uhuru wa Ukraine kama taifa utambuliwe.

Waziri wa Urusi amesema kuwa ni jukumu la Kiev kuandaa katiba mpya ili kuwezesha hilo lifanyike, mbali na kulinda maisha ya waukraine wachache wanaozungumza kirusi dhidi ya uvamizi kutoka kwa
waukraine wanaounga mkono kujiunga na jumuiya ya Ulaya.
Marekani imetaka hatua ya kuongeza wanajeshi zaidi wa Urusi katika mpaka mashariki ya Ukraine kukomeshwa mara moja.
Mazungumzo ya Paris siku ya ijumaa yalifuatwa na mazungumzo ya simu kati ya Rais Vladimir Putin wa Urusi na Rais Obama wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Washington siku ya
Jumamosi, Bwana Kerry alibadilisha mkondo na kuelekea Paris.

Ukraine inasisitiza kuwa Urusi ina njama ya kuigawanya Ukraine na kulisambaratisha kama taifa.
Waandishi wanasema kuwa Maafisa wa Marekani wamegawanyika iwapo mazungumzo hayo yaliyopangwa yametokana na nia halisi ya Urusi ya kujaribu kupunguza taharuki iliyopo au ni mipango ya
hatua zaidi ya kijeshi.
Pentagon inaamini kuwa maelfu ya wanajeshi wa Urusi wamekita kambi karibu na mpaka na Ukraine kwa niya ya kuwatishia viongozi wa Ukraine .
View detail

Internship Web 2.0 and Social Media for Development

http://azizicompdoc.blogspot.com/
The Technical Centre for Agricultural and Rural Cooperation (CTA) is a joint international institution of the African, Caribbean and Pacific (ACP) Group of States and the European Union (EU). Its mission is to advance food and nutritional security, increase prosperity and encourage sound natural resource management in ACP countries. It facilitates access to information and knowledge; supports evidence-based, multi-stakeholder development of agricultural policies and strategies; promotes inclusive value chain development and use of ICTs and strengthens the capacities of agricultural and rural development institutions and communities.
CTA has an opening for an intern within the Policies, Markets and ICTs Programme.
For more information follow the link below  View detail

Friday, March 28, 2014

RIDHIWAN KIKWETE AENDELEA KUSAKA KURA ZA JIMBO LA CHALINZE


CH 1

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipandisha bendera kwenye shina la wakereketwa wa CCM la Zinduka katika Kijiji cha Chahua,Kata ya Bwilingu Machi 27, 2014.
CH 2
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwasalimia wakina Mama wa jamii ya watu Wafugaji (Wamasai) wakati alipowasili kwenye Kijiji cha Matuli kwa ajili ya kuendelea na Mikutano ya Kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze.
CH 3
CH 4
34
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akishiriki kucheza muziki na wananchi wa Kijiji cha Matuli,Kata ya Bwilingu Machi 27, 2014,wakati wa moja ya Mikutano ya Kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze.
View detail

TUHUMA NZITO DHIDI YA WAZIRI MKUU BUNGENI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Hali ya hewa jana ilichafuka kwenye Bunge la Katiba baada ya mjumbe Ezekiel Wenje kuwatuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziri kuwa waliwahonga baadhi ya wajumbe wa kundi la 201.
Katika tuhuma hizo, Wenje alimtaja Waziri Profesa Jumanne Maghembe, Dk. Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka akisema kuwa walitoa rushwa ya vyakula, maji na vinywaji kwa wajumbe hao ili waunge mkono msimamo wa serikali mbili.
Kauli hiyo, iliyotolewa katika mjadala wa mabadiliko ya kanuni, ilisababisha mawaziri hao kunyanyuka kujibu tuhuma hizo, huku Wenje akisisitiza kuwa aliyoyasema ni kweli tupu.
Vilevile baadhi ya wajumbe wanaotoka katika kundi hilo walicharuka na kujaribu kujitetea huku mmojawapo akitishia kuwa iwapo Wenje asingeomba radhi, asingetoka ndani ya Bunge hilo.

Wenje, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana (Chadema), alianza kwa kueleza kwamba wapinzani “walilia” sana kuwa Bunge la Katiba lisingekuwa na usawa kutokana na Chama cha Mapinduzi kuwa na wajumbe wengi, ndipo ikaonekana wapatikane wajumbe wengine 201, lakini jambo la ajabu ni kwamba walioteuliwa katika kundi hilo asilimia 80 ni makada wa CCM akiwamo mzee maarufu ambaye ameingizwa kama mganga wa jadi.
Ingawa hakumtaja jina, Wenje alikuwa anamaanisha kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyeteuliwa kupitia kundi la waganga wa jadi.
Kuhusu rushwa, Wenje alisema:“…Sasa kuna wajumbe wa kundi la 201 walipelekwa kwa Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamepeana rushwa, vikao vingi vilifanyika usiku. Hii haikubaliki.”
Baada ya kauli hiyo ya Wenje, Profesa Maghembe alisimama ghafla huku akionekana kutaharuki, ambapo Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan alimpa nafasi ya kujieleza.
Profesa Maghembe alikiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe wa kundi hilo, akieleza kwamba ilikuwa ni katika hali ya ukarimu uliozoeleka miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
“Kuna kundi lipo hapa ambalo linafanya kazi ya kudhalilisha wenzao. Ni kweli niliwaalika kwa chakula wajumbe hao kwa taratibu za kawaida, lakini hakuna mbunge hapa anayeshindwa kujinunulia chakula, hakuna anayeweza kupewa rushwa.
“Kwa sababu hiyo ninaomba kiti chako kimtake mjumbe aliyewasilisha hoja hiyo aniombe radhi. Wenje aniombe radhi,” alisema Profesa Maghembe akiwa katika hali ya hasira, huku kukiwa na sauti za kuzomea na kushangilia kutoka kwa wajumbe.
Makamu mwenyekiti pia alifanya jitihada za kuwataka wajumbe kuwa wavumilivu, huku akitoa nafasi kwa Dk. Kawambwa kujieleza akisisitiza kwamba ni tuhuma nzito. 
Kawambwa alisema: “Ni kweli nilikutana nao; ni wajumbe ambao wanatoka kwenye taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu, lakini mbona wameshafanya mikutano yao mingine mingi ambayo mimi hawakuniita. Kama mtu akiwa hana hoja bora akae chini.”
Makamu Mwenyekiti alimtaka Wenje aombe radhi kutokana na kauli yake, lakini katika hali ya kushangaza mjumbe huyo alisisitiza kwamba Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamekiri.
“Maghembe amekiri aliwaita wafugaji na wavuvi ndiyo waliokula chakula cha rushwa, pia wapo wengine walienda kwa Waziri Gaudensia Kabaka, kuna ushahidi mama mmoja siwezi kumtaja jina hapa alikwenda huko akafukuzwa, nitakupa jina lake mwenyekiti baadaye. Aliambiwa kwamba anatoa siri… hoja iliyojadiliwa huko ilikuwa ni kwamba msimamo ni wa serikali mbili… rushwa ya chakula, maji na bahasha walipewa,” alisema Wenje na kusababisha kulipuka kwa kelele zaidi.
Wenje aliongeza kuwa kuna wajumbe wengine walikwenda hadi kwa waziri mkuu ambako walikula, walikunywa hadi saa 7:00 usiku.
Alisema wengine walikwenda kwa Gaudensia Kabaka (Waziri wa Kazi na Ajira) na walikula na kunywa na kupewa bahasha.
Baada ya Wenje kukaa, baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 walichachamaa wakitaka kutetea hadhi yao, akiwamo mjumbe kutoka kundi la wafugaji, Esther Juma aliyesema hawatendewi haki kama kundi kusema kwamba walihongwa.
Alisema yeye ana ng’ombe 3,000 na asingeweza kwenda kupokea rushwa ya chakula na kumtaka mbunge huyo kuwaomba radhi la sivyo asingetoka mlangoni.
Wakati mjadala huo ukiendelea, mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta aliyekuwa ametoka kwa udhuru, alirejea kimya kimya, na kumtaka Wenje kueleza iwapo anadhani kauli yake haikuwaudhi baadhi ya wajumbe.
Wenje alikiri kuwa ni kweli baadhi ya wajumbe wameudhika kutokana na ukweli aliosema dhidi yao na kuwaomba radhi kwa ukweli huo.
Kauli hiyo ilimfanya Sitta kutangaza kuwa anapeleka suala hilo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge na uamuzi utakaotolewa atautangaza bungeni.
View detail

Thursday, March 27, 2014

HALI HALISI BUNGE LA KATIBA

http://azizicompdoc.blogspot.com/  “Uvumilivu una mwisho wake, ukifika wakati huo tutawaambia Watanzania nini kinachoendelea na sisi tunakusudia kufanya kitu gani.”PICHA|MAKTABA
Kuna njama. Maneno haya mawili ndiyo yametumiwa na pande mbili zinazopingana ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, kuelezea hali iliyojitokeza jana wakati wa kikao cha Bunge hilo kuhusu mvutano wa mabadiliko ya kanuni.
Njama zinazoelezwa na pande hizo ni za kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya, zikirejea yaliyotokea jana jioni ikiwamo zomeazomea hali iliyomlazimu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kuliahirisha Bunge hadi leo jioni.
Baada ya kuahirisha Bunge hilo, Sitta alikutana na waandishi wa habari na kusema kwamba kuna njama za baadhi ya wanasiasa kutumia vurugu kuhujumu mchakato wa upatikanaji wa Katiba, badala ya kujenga hoja.
Bila kuwataja wanasiasa hao, Sitta alisema ikiwa hawataki kuendelea na mchakato huo, basi waondoke na kuwaacha wenye nia njema.
“Wanasiasa hawa wamedhamiria kuvuruga mchakato wa Katiba, tuhuma ambazo tumetuhumiwa leo na Lissu (Tundu) ni uongo na uzushi, mimi sihusiki na kupeleka marekebisho ya kanuni kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge,” alisema Sitta.
Sitta alikuwa anajibu mchango wa mjumbe wa Bunge, Tundu Lissu alioutoa mapema kwenye kikao cha jioni, akipinga kilichoelezwa ni njama za kutaka kubadili kanuni kinyemela ili kumsaidia mwenyekiti kulidhibiti Bunge.
Sitta alisema kwa kuzingatia kanuni ya 59 (1), Kamati ya Uongozi ina mamlaka ya kupeleka marekebisho ya kanuni ili kuliwezesha Bunge kufanya kazi vizuri.
Alisema hoja kwamba haiwezekani kufanyika mabadiliko hata kabla ya kuanza kutumika kanuni, siyo ya msingi kwani kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira yake.
“Kamati ya Uongozi ndiyo ilipeleka waraka wa mabadiliko ya kanuni kwa Kamati ya Kanuni na Haki kwa kuzingatia kanuni, lakini hata kabla ya kujadiliwa na kamati husika inaonekana kuna wajumbe ndiyo wameichukua na kuifikisha bungeni,” alisema Sitta.
Alisema kwa kiasi kikubwa marekebisho ambayo yangesomwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pandu Ameir Kificho, yalilenga kutoa ufumbuzi wa kanuni ya 37 na 38 juu ya upigaji kura ama uwe wa wazi au siri.
Sitta alisema pamoja na hilo, kulikuwa na marekebisho ya msingi kama kuweka utaratibu mzuri wa majadiliano katika kamati pia kuweka utaratibu wa vikao vya Bunge kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.
“Mengi ambayo alikuwa anayasema Lissu kama ni takataka hayakuwapo katika taarifa ya Kificho,” alisema Sitta.

Kauli ya Lissu
Lissu katika mchango wake alibainisha kile alichoeleza kama ‘njama’ za kuchakachua kanuni, akihoji inawezekanaje kasoro zikaanza kuonekana wakati kanuni hazijaanza kutumika.
Alisema kanuni zilipitishwa mapema mwezi huu na kiporo pekee kilikuwa ni ile ya 37 na 38 kuhusu upigaji kura.
“Tumeletewa jedwali la marekebisho ambalo linaonyesha kuna marekebisho katika kanuni ya 14 (1), 32, 33, 35 na zile za 37 na 38 pamoja na 58(1) (d) zingine ni 63 (1) na 64 na kufutwa kwa kanuni ya 85, jambo ambalo ni kinyume kabisa na kanuni zetu,” alisema Lissu.
Mbunge huyo wa Singida Mashariki, alisema utaratibu wa kurekebisha kanuni umeelezwa katika kifungu cha 87 (2) kwamba, mjumbe akiona kuna hitaji la kurekebisha kanuni awasilishe pendekezo kwa mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Kanuni na iwapo Mwenyekiti akiona inafaa atawasilisha mapendekezo hayo bungeni.
“Kanuni hazina hata wiki tatu, hazijaanza kutumika tayari mmeanza kuzichakachua hivi, kasoro mmezipataje wakati bado hazijaanza kutumika,” alihoji.
Huku akionyesha marekebisho hayo, Lissu alisema: “Hizi ni takataka ambazo hatutakubali ziingizwe ndani ya mabadiliko.” Alisema Kamati ya Uongozi haina mamlaka yoyote juu ya kanuni za Bunge.
Lissu kushtakiwa
Sitta alisema kutokana na lugha alizotumia Lissu juu yake, anakusudia kumfikisha kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge. Alisema atatoa utetezi na wale ambao wanamtuhumu wataeleza ili ukweli ujulikane.
Alisema vurugu za jana jioni, zilipangwa hata kabla ya kuanza Bunge hilo, kwani hata wajumbe wanaotokana na Ukawa walisusia kutoa maoni katika Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge.
“Wajumbe wao hata kwenye kamati walikuwa hawazungumzi na wakati wanatoka walisikika wakisema wataendelea na mkakati wao wa kufanya vurugu,” alisema Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dalili za kuvunjika kikao hicho zilionekana mapema baada ya wajumbe kuingia ukumbi kwani baadhi walikuwa kwenye makundi yaliyoashiria kujipanga kwa jambo lililokuwa mbele yao.
Kwa muda kidogo ukimya ulitawala bungeni baada ya Sitta kuzungumza, kisha ilisikika sauti ikiomba mwongozo.
Mwenyekiti alitoa nafasi kwa Lissu akitimiza ahadi yake aliyokuwa ameitoa asubuhi kabla ya kuahirisha Bunge hilo.
Mapema jana asubuhi, Sitta alikuwa ameahidi kuwa angetoa nafasi kwa miongozo hata kama ingekuwa 20 au 30 ili kila mtu aweze kupata kile alichokuwa akikihitaji.
Baada ya Lissu kueleza tuhuma zake, zomea zomea ilianza bungeni kiasi cha kuvuruga na kuondoa utulivu.
Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakary baada ya kuruhusiwa alisema Bunge linaendeshwa na kanuni “haiwezekani huko aliko aandike mambo yake na kuyapeleka kwenye kamati halafu yaletwe bungeni, jambo hili haliwezi kukubalika.”
Alisema Bunge hilo ni lenye hadhi na heshima kubwa lakini kanuni kukiukwa kwa kanuni na sheria husika kunapunguza hadhi yake.
Kauli za wajumbe hao ziliungwa mkono na mjumbe mwenzao Ismail Jussa ambaye alisema waliopendekeza mabadiliko ya kanuni walikaa mafichoni kutekeleza azma hayo.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, akizungumza huku akikatishwa na makofi yaliyochanganyika na zomeazomea na yeye akielekeza maneno yake kwa kelele hizo alisikika akisema, “sijazoea kuzomewa” na wakati mwingine akisema “sijazoea kupigiwa makofi.”
Baada ya utulivu kukosekana, Sitta aliahirisha Bunge hilo ili kwanza wajadiliane kabla ya kuendelea.

Wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamesema wataendelea kupambana ndani ya Bunge Maalumu hadi ipatikane Katiba nzuri na watakuwa wa mwisho kujitoa katika mchakato huo.
Pia wamebainisha kuwa kukimbia au kujitoa katika mjadala huo ni sawa na kuwaachia CCM walio wengi kwenye Bunge Maalumu watunge Katiba wanayoitaka wenyewe na hivyo kuzima mawazo ya wananchi.
Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe alitoa msimamo huo jana katika mkutano na waandishi wa habari huku akiweka tahadhari kuwa “Uvumilivu una mwisho wake, ukifika wakati huo tutawaambia Watanzania nini kinachoendelea na sisi tunakusudia kufanya kitu gani.”
Imeandikwa na Mussa Juma, Habel Chidawali na Editha Majura
Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuna dalili zinavyoonyesha kuwa CCM hakina nia njema ya kuwafanya wananchi wapate Katiba nzuri.
“Hakuna mwendawazimu ambaye anaweza kufanikiwa kutugombanisha na kutusambaratisha, lazima katika jambo hili tutashinda na matakwa ya wananchi yatachukua nafasi ndani ya Katiba.”
Kwa upande wake James Mbatia alisema Ukawa haiwezi kwenda kinyume na wala haitakuwa tayari kuwasaliti wananchi katika yale ambayo waliyapendekeza kwenye rasimu.
Hotuba za JK, Warioba kutojadiliwa
Matarajio ya wajumbe wa Bunge Maalumu kujadili hotuba ya Rais Jakaya Kikwete na ile ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba yameyeyuka.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alisema amechukua uamuzi huo baada ya majadiliano ya kina na kuonekana ni kama kutanguliza mjadala wa Rasimu ya Katiba kabla ya wakati wake.
“Kumbukeni waheshimiwa Rasimu ya Katiba tutaijadili kwa mpangilio wa sura mbili kama haitafanyika marekebisho ya kanuni hivyo, tukijadili hotuba hizi, wabunge watajadili mahala popote panapowahusu na hivyo itaharibu kabisa utaratibu wa kanuni,” alisema Sitta.
Awali, ilipangwa hotuba hizo kujadiliwa hasa kutokana na hoja mbalimbali za wajumbe kutaka kujadiliwa hutuba hiyo.
Miongoni mwa wajumbe walioomba kujadiliwa kwa hotuba hizo ni Julius Mtatiro ambaye pia aliomba kurejeshwa kwa Jaji Warioba kutoa ufafanuzi kuhusu masuala yaliyoibuliwa na Rais Kikwete.

Mjumbe mwingine Tundu Lissu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa alikuwa anakusudia kumjibu neno kwa neno Rais Kikwete katika kila hoja kwani hotuba yake ilikuwa na upungufu.
View detail

Monday, March 24, 2014

Egyptian court condemns 529 people to death


 An Egyptian court has today sentenced to death 529 members of the Muslim Brotherhood on charges which include murder as the authorities tighten their squeeze on the movement.
As the verdict was called out family members of the condemned stood outside the courthouse screaming. Defence lawyers stated that this was the largest mass death sentence ever handed out in Egypt’s modern history.
Turmoil has continued to plague the country ever since Egypt’s first ever freely elected president, Mohamed Morsi, of the Muslim Brotherhood, was overthrown by the military in July. 
State television reported the sentences without comment and a government spokesman or other government officials did not immediately respond to calls.
The majority of the defendants at today’s hearing were detained and charged with carrying out attacks during the violence which erupted in the southern province of Minya after the authorities heavy handedly forced the dispersal of two Muslim Brotherhood protest camps in Cairo on August 14 last year.
“The court has decided to sentence to death 529 defendants, and 16 were acquitted,” defence lawyer Ahmed al-Sharif said.
The Muslim Brotherhood, who call for the downfall of military rule in Egypt, have now largely been driven underground.
Mohamed Mahsoub, who served as minister of legal affairs under Morsi, described the court’s decision “a ruling calling for the execution of justice” on his Facebook page.
The charges against the group, include violence, inciting murder, storming a police station, attacking persons and damaging public and private property. The men can appeal against the ruling.
“This is the quickest case and the number sentenced to death is the largest in the history of the judiciary,” said lawyer Nabil Abdel Salam, who defends some Brotherhood leaders, including Morsi.
“There are a lot of flaws in this verdict. I think maybe an appeal could be successful but nothing is predictable,” said Mohamed Zaree, program manager, Cairo Institute for Human Rights Studies.
It is doubtful at this moment that the sentences will be carried out as stated by experts, the very issuing of the sentences themselves are very significant. It has also thrown into light the justice system of Egypt,
“When the trial starts on Saturday and it is just a procedural hearing, and the judge doesn’t listen to any lawyers or witnesses and doesn’t even call the defendants, you are before a group of thugs and not the judiciary,” said Walid, a relative of one of the defendants.
Egypt is also currently detaining three Al Jazeera England journalists and they continue to fight the courts on the charges of portraying false news and inciting terrorism. The journalists all deny the allegations.
View detail

WALIOCHAGULIWA KUINGIA KIJIJI CHA MAISHA PLUS HAWA HAPA


Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania.
Wageni waalikwa waliofika kijijini cha Maisha Plus kuangalia uzinduzi…
Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao.
Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya).
Mkuu wa Kijiji… Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe.
Wageni waalikwa.
Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea… ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48.
Kila mmoja anawajibika kuhakikisha kazi ya kujenga nyumba inafanikiwa.
Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini.
6
Safari ya kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi… washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5
Safari ikiendelea huku washiriki wakiwa wameshachoka… wengine walitamani kughairi kuendelea na safari.
Wengine ilibidi wasaidiane kupeba mizigo.
Hakuna kuchoka, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe…
Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo. 

 
 
 
View detail

MAKAMU WA RAIS ZNZ ATEMBELEA SHAMBA LA MTOTO WA MKULIMA

PG4A3916
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd kukagua zao la zabibu  katika shamba lake  lililopo Zuzu , Dodoma.
PG4A3882
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanachuo wa Chuo cha Nyuki cha Tabora waliotembelea shamba lake lililopo Zuzu, Dodoma kujifunza ufugaji bora wa Nyuki  Machi 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PG4A3920
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu  zao la migomba kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd ambaye alitembelea shamba lake lililopo Zuzu mjini Dodoma Machi 22, 2014. Wapli kulia ni Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka na kulia ni Majasiliamali wa Dar es salaam, Alphonce Buhatwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
View detail

Thursday, March 20, 2014

KCB YAZINDUA TAWI LA SHARIAH DAR

_DSC4373
Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Katikati)akizindua tawi jipya la Benki ya KCB Shariah Lililopo barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam, litakalotoa  huduma kwa kuzingatia maadili ya kiislamu,ambapo watapata mikoipo isiyokuwa na riba .Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania  Moezz Mir, wapili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa benki hiyo Dr.Edmund Mndolwa na wakwanza Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Shariah wa benki hiyo Uzairu Athuman.
_DSC4392
Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la Benki ya KCB Shariah Lililopo barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam.
_DSC4428
Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiteta jambo na Mwenyekiti wa benki hiyo Dr.Edmund Mndolwa mara baada ya kuzindua tawi jipya la Benki ya KCB Shariah Lililopo barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam.
_DSC4464
Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Katikati)akimkabdhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni kumi,Mwenyekiti wa yatima Group Trust Fund Winfrida Lubanza kwaajili ya kuendeleza kilimo cha kisasa wakati wa uzinduzi tawi jipya la Benki ya KCB Shariah Lililopo barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam.kushoto ni ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Dr.Edmund Mndolwa na  watatu toka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania  Moezz Mir. 
View detail

AMUUA MAMA YAKE MZAZI KWA PANGA

uzee

Jehi la polisi wilaya ya Makete mkoani Njombe linamshikilia Bw. Sadick Sanga (28) mkazi wa kijiji cha Unyangogo kata ya Iniho wilayani hapa, kwa tuhuma za kumuua kikatili Bibi Meluti Mbwilo (70) ambaye ni mama yake wa kambo
Tukio hilo limetokea Machi 14 mwaka huu ambapo mtuhumiwa alitenda mauaji hayo kwa kumkatakata na panga kichwani na miguuni wakati marehemu akiwa jikoni kwake
Akizungumzia tukio hilo Afisa upelelezi wilaya ya Makete ambaye pia ni kaimu OCD, Bw. Gosbert Komba amesema kuwa baada ya wananchi kugundua mauaji hayo, walimkamata mtuhumiwa na kisha wakatoa taarifa kwa jeshi hilo ambapo walifika mara moja na kumtia mbaroni mtuhumiwa
Amesema mtuhumiwa alikamatwa na kielelezo ambacho ni panga analodaiwa kulitumia kutekeleza mauaji hayo na kwa sasa anashikiliwa na jeshi hilo na atapandishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kujibu mashitaka yanayomkabili

Bw. Komba amekiri vitendo vya mauaji ya kikatili kuendelea kushamiri wilayani Makete ambapo ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume na sheria za nchi
Amesema mauaji hayo yanahusishwa na imani za kishirikina hivyo, kutokana na wazee wengi kuonekana wana macho mekundu hivyo watu kuwadhania kuwa ni wachawi hivyo kuwataka wananchi kuondokana na dhana hiyo potofu
“Unajua maeneo mengi hapa wilayani watu wanapikia kuni, na kuni zinatoa moshi, hawatumii gesi ama umeme huko vijijini, hivyo uwezekano wa watu kuwa na macho mekundu ni mkubwa kutokana na moshi unaotokana na kuni wakati wa kupika, haimaanishi macho mekundu yao eti ni wachawi” alisema Komba.
View detail

KAMPUNI MPYA YA SIMU ZA MKONONI YAANZISHWA TANZANIA

unnamed (2)
 Afisa Mtendaji MKuu wa Smart Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena,jijini Dar,kulia kwake ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham.
unnamed (3)
Pazia likishushwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kampuni hiyo ya simu za mikononi-Smart.”lets talk. 
unnamed (4)
Afisa Mtendaji MKuu wa Smart Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar.
unnamed (1)
Pichani kati ni Balozi wa Kampuni hiyo ya simu iliyozinduliwa  jijini Dar,Msanii wa maigizo ya vichekesho atambulikae kwa jina la Hemed Maliyaga a.k.a Mkwere Orijini akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani (shoto) na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham wakiwa katika picha ya pamoja.
unnamed
Viongozi wakuu wa kampuni ya Smart Telecom, Afrika Masharikii wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi waliojipatia zawadi kupitia mtandao huo,baada ya kushiriki kwenye kampeni ya GIVE US A NAME iliofanyika hivi karibuni.
IPS kukuza ujasiliamali wa jamii katika mawasiliano ya simu Burundi, Uganda na Tanzania
Shirika la kuhamasisha viwanda (IPS), chombo na silaha ya maendeleo ya viwanda chini ya mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Aga Khan (AKFED),jana wametangaza kuingia katika soko la mawasiliano la Afrika Mashariki chini ya kampuni iitwayo SMART.
Jina la kampuni ni matokeo ya kura zilizopigwa Afrika Mashariki katika kampeni ya Uvumbuzi. Kuzinduliwa kwa kampuni hiyo kutaisaidia AKFED kukuza huduma zake za kibiashara kwa jamii katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda, lengo kuu likiwa kuwekeza na kuwahudumia wateja

Mtandao wa IPS una uwanda/uelewa mpana katika sekta ya mawasiliano. Ni washirika wakubwa wa Roshan shirika linaloongoza katika utoaji wa huduma za mawasiliano nchini Afghanistan na pia washirika muhimu katika shirika la Tcell linaloongoza katika kutoa huduma Tajikistan.
IPS pia ni wawekezaji wakubwa na wa pekee waliowekeza SEACOM submarine cable venture in East Africa. Wakati umefika ambao ushirika wa IPS ndani ya SMART utaleta ushirikiano na kuweka record ya ushirikiano wa makampuni ya simu Nepal na Cambodia  na kuwafanya wawe waongozaji katika soko hili.
Kuzinduliwa kwa SMART kutashirikisha uzoefu wa AKDEF katika kuwekeza kwa lengo la kuhamasisha ujasiliamali na ujenzi wa uchumi wa sauti ambao utatoa fursa nyingi za ajira na kuboresha maisha ya watu. Afrika Mashariki. AKFED imewekeza Serena Hotels, Diamond Trust Bank, Jubilee Insurance Group, National Media Group na katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji na miundombinu kama vituo vya nguvu ya umeme vya Bujagali na Tsavo.

“Kazi zetu katika mawasiliano kwa njia ya simu hasa Roshan-Asia ya kati ni kuboresha uwekezaji wa jamii katika miundombinu ya jamii, huduma za afya na elimu. Pia kutengeneza biashara yenye mafanikio katika soko ili tuweze kujitofautisha na washindani wengine, Tunatazamia kuwa uwekezaji katika kampuni dada ya AKDN utakua umeenea katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda kwa zaidi ya miaka 100” alisema Lutaf Kassam Meneja wa IPS
SMART itaingia katika masoko haya ikiwa na dhamira ya embrance tamaduni za ndani ili kuboresha jamii wanakofanyia kazi.mfano mzuri wa dhamiri hii ni njia ambayo jina la kampuni lilivyochaguliwa. Kampeni ya Tupe Jina ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka 2013 ikiwahamasisha watu wa Afrika Mashariki kupendekeza na kulipigia kura jina la kampuni.
 Kampeni hiyo iliwavutia zaidi ya watu 70,000 na majina tofautitofauti yalipendekezwa na kupigiwa kura. Mwisho kampeni ililipata jina la SMART ikikusudia kuangalia uvumbuzi wa mawazo katika soko la Afrika Mashariki.
View detail

Wednesday, March 19, 2014

WALIOPOTELEWA NA JAMAA ZAO KTK NDEGE YA MALAYSIA WATISHIA KUSUSIA KULA


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Jamaa na ndugu wa abiria wa China waliokuwa kwenye ndege ya Malaysia iliyopotea,wametisha kususia chakula ikiwa maafisa wa utawala wa Malaysia watakosa kutoa taarifa kamili kuhusu ndege hiyo siku 11 zilizopita.
Jamaa hao wameelezea kukerwa mno baada ya mkutano na maafisa wa shirika la ndege hiyo mjini Beijing.
Maafisa wa Malaysia nao wanasema kuwa wanafanya kila wawezalo katika kuisaka ndege hiyo.
Ndege hiyo MH370 ilitoweka tarehe nane mwezi Machi ikiwa imewabeba watu 239.
Nchi 25 zinahusika na juhudi za kuisaka ndege hiyo huku China ikianza kuitafuta katika ardhi yake.
Watu 153 raia wa China walikuwa kwenye ndege hiyo iliyokuwa inatoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.
Vyombo vya habari nchini China vimekuwa vikikosoa juhudi za Malaysia katika kuitafuta ndege hiyo.
Baadhi ya jamaa za wachina wanasema kuwa wanaamnini serikali ya Malaysia imebana taarifa kuhusu ndege hiyo na wanataka maelezo zaidi kuihusu.
Baada ya kukutana na maafisa wa shirika la ndege siku ya Jumanne, familia za waliokuwa kwenye ndege hiyo walitishia kususia chakula
"Tunachokitaka ni ukweli,'' alisema mwanamke mmoja.
Wakati huohuo, nchi jirani ya Malaysia, Thailand imesema kuwa jeshi lake limetambua kile linachosema ni Data za mtambo wa Rader ambazo huenda zilitoka kwenye ndege hiyo.
Inasema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea Magharibi baada ya kupoteza mwelekeo. Hii inathibitisha madai ya hapo ya awali ya jeshi la Malaysia.
View detail

ANGALIA JAJI WARIOBA ALIPOFAFANUA MUUNDO WA SERIKALI 3

Tuesday, March 18, 2014

TURKEY SCHOLARSHIPS

http://azizicompdoc.blogspot.com/

FULL TUITION FEE + MONTHLY STIPEND. You can now run your postgraduate course without paying a kobo. INTERESTED? Then apply for Turkiye Postgraduate Scholarship. Deadline is March 31, 2014 Follow the link below! View detail

SERIKALI TATU KUONGOZA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Jaji Sinde Warioba leo aweka wazi kwanini tume yake ilipendekeza serikali tatu kwa nia ya kudumisha muungano pamoja na changamoto kutokosekana ila kuna uwezo mkubwa wa kuondoa kero nyingi za muungano na kudumisha muungano wetu, suala la ukubwa na uzito wa serikali hizo amesema ni suala la kawaida na sio zito kama linavyofikiriwa na wengi ktk nchi, uthubutu lazima uwepo tukitaka kuishi bila migongano ktk muungano wetu.
Katika kuielezea Zanzibar kuhusu changamoto za muungano amesema kiuhalisia huwezi kuikataza leo znz isiitwe nchi na wakati katiba ya nchi hiyo inatambua kama nzn ni nchi kamili ktk muungano wa nchi mbili yaani Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya watu wa Tanganyika. Mamlaka ya viongozi wa nchi ya znz yalionekana kuchukuliwa na Rais wa muungano na baadae kurudishwa kupitia katiba mpya ya Zanzibar, kitu ambacho kwa sasa ni kigumu kutokana na sheria zinazotungwa na bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuonekana hazitatumika znz mpaka baraza la wawakilishi znz litakapozipitia na kuzipitisha sheria hizo.

Mgawanyo wa mapato ya muungano umekua mgumu na kusababisha mapato ya muungano kutumika zaidi ktk upande mmoja wa muungano ambako ni Tanzania bara. Akaunti ya pamoja ni miongozi mwa mambo ya makubaliano ktk muungano lakini limekua gumu mpaka sasa kufanyiwa kazi, Mamlaka ya waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano ni mpaka zanzibar, lakini haonekani waziri mkuu kukagua miradi ya maendeleo zanzibar, halikadhalika kwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania haonekani kufanya hivyo kwa zanzibar.
Suala la Tanganyika kujificha ktk koti la muungano limedhihirishwa dhahir leo bungeni na Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Sinde Warioba na kuwaasa wajumbe wa bunge hilo kua makini na maamuzi yao ili kufikia mafanikio mazuri ya kudumisha muungano wetu na kusema ye na wajumbe wenzake wametoa pendekeze la kua na serikali tatu badala ya mbili za sasa kama inavyotambua katiba yetu.

Rasimu hiyo imeonyesha kuvuta hisia za wajumbe wengi wa bunge maalum na kutoa ahadi za kufanya vizuri zaidi ktk maamuzi yao kama alivyotoa shukrani zake makamu mwenyekiti wa bunge maalum Mh Samia Suluhu. Mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki Afrika

View detail

Monday, March 17, 2014

SILAHA ZA AL SHABAAB ZAZIDI KUA NZITO WANAZITOA WAPI?

Ripoti ya umoja wa mataifa imeonya kuwa silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa vikosi vya serikali ya Somali zimeingia katika mikono ya kundi la Al-shabaab kutokana na ukiukwaji wa utaratibu katika serikali.
Uchunguzi huo uliofanywa na wataalam walio huru umesema kuwa silaha za kudungua ndege,mabomu na risasi zilizotoka nchini Uganda na Djibout haziwezi kuwajibikiwa.
Ripoti hiyo sasa inataka taifa la Somali kuwekewa vikwazo vya silaha ambavyo viliondolewa mwaka uliopita.
Wataalam hao wamesema kuwa wana ushahidi kwamba mshauri mkuu wa rais nchini Somali amekuwa akihusika na mpango wa kuwapelekea silaha wapiganaji wa Alshabaab. View detail

BUNGE LASITISHWA GHAFLA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Hali hiyo imetokea ghafla saa 11 jioni baada ya mwenyekiti wa mabadiliko ya katiba Jaji Warioba kuingia ktk bunge na wabunge wa bunge maalum  kuamua kupiga meza kama kumpongeza mwenyekiti kwa kuja na kutoacha kupiga meza kwa zaidi ya robo saa, na walipotakiwa kuacha wakawa wanaendelea mpaka pale mwenyekiti wa kudumu Mh Samwel Sitta alipoamua kuliahirisha bunge hilo mpaka itakapotangazwa tena. Je watanzania ni mabadiliko ya kidemokrasia au utovu wa nidhamu na utumiaji mbovu wa rasilimali za watanzania? jibu na maamuzi tunayo sisi wenyewe na kuamua watu hawa kuwarudisha tena bungeni msimu ujao au kuwaondoa wakajifunze tabia. Mali na muda wa watanzania unapotea bila sababu kwa umbumbumbu wa watu wachache, kuna haja ya mabadiliko nchini kwetu View detail

KALENGA KUMEKUCHA CCM YAIZIDI CHADEMA ZAIDI YA MARA 3 KURA ILIZOVUNA

1 (7)
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Ndg. Godfrey Mgimwa akibebwa juu juu na wanachama na wapenzi wa CCM baada ya matokeo kuonyesha ameshinda kwa kishindo Kalenga.
Matokeo Kalenga CCM 16861, Chadema 4273, Chausta 78, Umoja wetu ndio Ushindi Wetu!
View detail

CCM WAENDELEA KUSHINDA KTK MATOKEO YA VITUO KALENGA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Chama cha Mapinduzi CCM kimezidi kuwakosha wanachama wake baade ya kuibuka na ushindi ktk baadhi ya vituo vya uchaguzi Kalenga, na sasa wanachama hao wanangojea matokeo ya mwisho yatakayomuweka Mbunge wao madarakani na huku wapinzani wao CHADEMA wakiwa ktk sintofahamu baada ya mbunge wa viti maalum  Rose Kamili ambaye pia ni mke wa Dr Slaa kukamatwa akiwa anatoa rushwa kwa wapiga kura wa vituo mbalimbali

1. Rose Kamili
  Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Rose Kamili, ambaye pia ni mke wa Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa, akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa madai ya kukutwa akigawa rushwa kwa wapigakura

Endelea kutufuatilia uhabarike zaidi
View detail

Thursday, March 13, 2014

HONGERA MWL MNYENGEMA KWA KUSTAAFU SALAMA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Huyu ni Mwl Myengema akiwa ktk maulid ya shukran kwa Allah kumjaalia kumaliza kazi yake ya ualimu salama ingawa alikutana na mambo kadhaa kazini


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Huyu ni Mwl Myengema akiwa na mama yake mzazi Bi Aikama nyumbani kwake Ng'apa Lindi


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Huyu ni Mwl Myengema akiwa na mama yake mzazi Bi Aikama na mumewe kipenzi Alhaj Said Ahmad Mnyengema nyumbani kwa mama yake Ng'apa Lindi

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Huyu ni Mwl Myengema akiwa na Mumewe Kipenzi akimpa hongera ya kustaafu salama na kumkumbuka allah kwa wema aliomtendea 

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Huyu ni Mwl Myengema akiwa na mwanawe wa kwanza wa kiume Mr. Abdulazizi Mnyengema (Computer Doctor) 

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Kaka ndugu na shemeji wa Mwl Mnyengema wakimuunga mkono Mwl kwa maulid ya shukran aliyofanya

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Mwanafunzi wa Madrasa akitoa daaawah kama ilivyokua kazi ya Mwl Mnyengema

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Shekh mkuu wa Lindi ambaye pia ni khadh wa mkoa akiwa pamoja na Ummat muhamad kumpongeza Mwl Mnyengema kwa kustaafu salama na kumkumbuka allah kwa yote

View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop