Welcome to our online store Portal

Template Information

Wednesday, February 27, 2013

MADUDU YALIYOMFANYA PAPA AJIUZULU HAYA HAPA





*Makachero waibua kashfa nzito
*Papa akabidhiwa ripoti ya usaliti, ufisadi
*Keith Kardinali O'Brien aachia ngazi

SIKU moja kabla ya kung’atuka kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedicto XVI, kwenye wadhifa wake, imeripotiwa kuwa uamuzi wa kuachia ngazi aliufikia baada ya kubaini vitendo vya usaliti, ufisadi na ushoga ndani ya kanisa ambavyo kutokana na umri wake mkubwa hakuwa na uwezo na nguvu za kukabiliana navyo.
Gazeti la Italia, La Repubblica, limekariri taarifa za kiintelijensia za ndani ya kanisa hilo, zilizokuwa zikieleza kuwa makachero wa Vatican, walimfikishia Papa Benedicto ripoti yao ya uchunguzi ya mwenendo wa mlolongo wa matukio ya usaliti, ulaji rushwa na kashfa ya chini kwa chini ya uwepo wa vitendo vya ushoga katika Vatican.

Katika taarifa yake hiyo, gazeti hilo liliripoti kuwa, Papa Benedicto baada ya kuichambua ripoti hiyo na kubaini uwezekano wa kuibuka mgogoro wa kikanisa iwapo hatua za kushughulikia kashfa hizo hazitachukuliwa huku yeye mwenyewe akijitathimini afya yake na kubaini hataweza kuhimili vishindo vya kukabiliana na kashfa hizo, Februari 11 mwaka huu, alitangaza kujiuzulu.

Katika tangazo lake hilo, Papa Benedicto alieleza kuwa anakusudia kujiuzulu rasmi nafasi yake itakapofika Februari 28 kwa sababu hawezi tena kutekeleza majukumu yake kutokana na umri wake.

Wakati hatua ya kujiuzulu kwa Papa ikisubiriwa kwa shauku kubwa na mamilioni ya watu duniani sambamba na uchaguzi wa Papa mpya, ripoti ya kikachero kutoka ndani ya Vatican iliyoripotiwa na gazeti La Repubblica, ilieleza kuwa makardinali watatu, akiwemo mkuu wa zamani wa masuala ya ulinzi wa Vatican, walitakiwa ufanyike uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, ushoga na ufisadi ulioibuliwa na uchapishwaji wa nyaraka za siri za papa katika kashfa iliyopewa jina la ‘Vatileaks.’

Ripoti hiyo inaeleza zaidi kuwa makardinali hao watatu waliwasilisha ripoti ya uchunguzi wao kwa papa Desemba 17 mwaka jana, katika vitabu vikubwa viwili vyenye majalada ya rangi nyekundu vyenye takriban kurasa 300 vilivyokuwa na ramani halisi ya uovu na ufisadi ndani ya kile walichokiita ‘Holy See.’

Kwamba Papa baada ya kupokea ripoti hizo na kuzipitia, akiwa hata hajazitoa mezani kwake alipochukua uamuzi aliokuwa ameuficha kwa muda mrefu pale alipopokea ripoti nyingine iliyokuwa ikielezea kashfa za aina hiyo ya makachero wa Vatican.

Kashfa ya Vatileaks ilitokea Januari mwaka jana, baada ya mlolongo wa nyaraka za ndani za kinachoitwa Holy see, zilipovuja kwenye vyombo vya habari vya Italia na kusababisha sintofahamu kwa taifa zima.

Hata hivyo, wakati tukio hilo likizidi kufukuta ndani ya Vatican, Mwanahabari wa Kiitaliano, Gianluigi Nuzzi, aliongeza mafuta kwenye moto baada ya kutoa kitabu chake kiitwacho ‘His Holiness.’

Kitabu hicho kinaangazia vita vya madaraka ndani ya Vatican kwa kutoa nyaraka na barua za siri kutoka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa kanisa kwenda kwa Papa na kwa katibu wake muhtasi.

Mei mwaka jana, mamlaka za Vatican zilimkamata Paolo Gabriele, msaidizi wa papa kwa tuhuma za kuhusika na uvujishaji wa nyaraka hizo za siri na kumuhukumu kifungo cha miezi 18 jela, hata hivyo baadaye alisamehewa.

Wakati huo huo, Kardinali Keith O'Brien wa Uingereza, amejiuzulu wadhifa wake kutokana na tuhuma za kwenda kinyume na matakwa ya kikasisi mapema miaka ya 1980.

Kardinali Keith O'Brien ambaye alikuwa astaafu uongozi wa kanisa hilo mwezi ujao, akiwa na umri wa miaka 75, ameachia madaraka kama Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo nchini Scotland.

Kutokana na uamuzi huo, hatarajii kusafiri kwenda Vatican kushiriki kumchagua Papa ajaye baada ya Papa Benedict XVI kutangaza kuwa ifikapo kesho ataachia madaraka ya kuliongoza kanisa hilo.

Imeripotiwa kuwa, Askofu huyo mkuu wa zamani wa Kanisa la Andrews na Edinburg, ameshutumiwa na mapadre watatu ambao waliwasilisha malalamiko yao wiki mbili zilizopita kwa mwakilishi wa Papa nchini Uingereza, kuwa aliwavunjia heshima makasisi hao miongo mitatu iliyopita.

Wafuatiliaji wa mambo wanaeleza kuwa, kujiuzulu kwa kardinali huyo kunaongeza shinikizo kwa makardinali wengine wanaokabiliwa na tuhuma juu ya namna walivyoshughulikia kashfa za ngono zilizowakabili watumishi wa kanisa hilo kuachia ngazi. View detail

TCRA YAVIFUNGIA VITUO VIWILI VYA REDIO NA KUVITOZA FAINI

 

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA kupitia kitengo cha maudhui imevifungia matangazo kwa muda wa miezi sita vituo vya radio viwili nchini kwa kukiuka maadili ya
utangazaji.

Vituo hivyo ni pamoja na Kwa Neema FM ya Mwanza iliyofungiwa kwa kuendesha mjadala uliokuwa ukihusiana na watu wa dini gani wenye haki ya kuchinja wanyama kati ya waislam na wakristu hali iliyosababisha mgongano wa waumini wa dini hizo.

Kingine ni Imani Radio FM ya mjini Morogoro ambayo imefungiwa kwa kosa la kupinga zoezi la sensa mwaka jana na kuwashawishi waumini wa dini ya kiislam wasijiandikishe.
Nayo Clouds FM imepigwa faini kwa kuendesha mjadala kuhusiana na ushoga pamoja na kuwa na kipengele kwenye kipindi cha Power Breakfast kiitwacho ‘Jicho la Ng’ombe’ ambacho wametakiwa wakifute kutokana na kuendeshwa kinyume na maadili.
View detail

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akagua Ukumbi mpya Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam Unaojengwa na Serikali yake


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi mkubwa wa mikutano wa Julius Nyerere multi-purpose International conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete bali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali.
Sehemu ya jukwaa kuu
Nafasi za wajumbe wa mikutano
Viti
Upande wa juu
View detail

Tuesday, February 26, 2013

Mdahalo wa mwisho wa wagombea Kenya

Uhuru Kenyatta alisemekana kufanya vyema katika mjadala wa kwanza

Mdahalo wa mwisho wa wagombea wa uchaguzi nchini Kwenya unafanyika jioni ya leo.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa mgombea wa Urais Uhuru Kenyatta alikuwa amesusia mdahalo huo akidai kuwa mdahalo wa kwanza waliokuwa wanauendesha mjadala wenyewe waliangazia sana swala la ICC na kuwafanya wagombea wengine kumlemea.
Uhuru pamoja na mgombea mwenza William Ruto, wanakabiliwa na kosa la kuwa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/2008 katika mahakama ya ICC.
Duru zilisema kuwa Uhuru alisitisha kampeini zake leo ili kuweza kujiandaa vilivyo kwa mjadala huo.
Wagombea wengine akiwemo waziri mkuu Raila Odinga wanajiandaa kwa mjadala huo ambaop hii leo utalipa kipao mbele mbele swala la ardhi, sera za kigeni, na uchumi.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa asilimia tisini ya wapiga kura wanaona mjadala huu una manufaa kwa wakenya. Asilimia themanini na tano walisema wako trayari kutazama mjadala huo.
Asilimia robaini ya wapiga kura waliohojiwa punde baada ya mjadala wa kwanza walisema wangempigia kura Uhuru Kenyatta wakati asilimia 33 walisema wangempigia kura Raila Odinga.Wawili hao ndio wagombea wakuu katika uchaguzi huu.
View detail

Monday, February 25, 2013

WAKENYA WAIOMBEA NCHI YAO AMANI KTK UCHAGUZI MKUU

Mamia ya Wakenya wamehudhuria mkusanyiko wa mwisho wa sala mjini Nairobi, kuomba uchaguzi mkuu wa juma lijalo uwe wa salama.
Mhadhara huo wa ibada umefanywa baada ya polisi kusema kuwa vipeperushi vinavochochea fujo vilisambazwa katika baadhi ya maeneo.
Wagombea kadha wa urais walihudhuria mhadhara wa leo, pamoja na Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta.
Anakabiliwa na  mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu kuhusu ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa Kenya miaka minne iliyopita ambazo ziliuwa watu zaidi ya elfu moja.
View detail

Friday, February 22, 2013

Watu 7 wauawa wakitoka msikitini Kenya

 
Eneo la Kaskazini mwa Kenya limekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na Al Shabaab

Watu saba wameuawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi karibu na msikiti Kaskazini Mashariki mwa Kenya, karibu na mpaka na Somalia.
Wanakijiji waliambia azizicompdoc.blogspot.com kuwa watu kumi waliokuwa wamejihami waliwashambulia kwa bunduki watu hao wakati walipokuwa wanaondoka msikitini mapema asubuhi.
Mwanzo wanaume watano waliuawa na kisha wanawake wawili waliosikia milio ya risasi walipofika kuchunguza, nao pia wakauawa.
Shambulio linafanyika chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika katika eneo mojawapo ambapo usalama ni tatizo kubwa.
Wenyeji wa kijiji cha Malaley wanasema kuwa hakuna kilichoibiwa kwani washambuliaji walitoroka punde baada ya shambulizi.

Kijiji hicho kiko umbali wa kilomita 45 kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo ni makao kwa wakimbizi zaidi ya laki tano, waliotoroka vita nchini Somalia.
Katika mwaka mmoja uliopita, eneo hilo limekumbwa na mashambulizi ambayo yamelaumiwa kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu Al Shabaab.
Al-Shabab iliahidi kulipiza kisasi wakati wanajeshi wa Kenya walipokwenda Somalia kupambana nao, mwezi Oktoba mwaka 2011 kama juhudi za kusaidia wanajeshi wa muungano wa Afrika.
View detail

Thursday, February 21, 2013

NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA MILION MIAMBILI ZAKAMATWA NAMTUMBO NA KAMPUNI YA GAME FRONTIERS OF TANZANIA



Gari la Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA likirejea katika Ofisi ya Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la SELOU likitokea ndani ya Pori

Hawa ni wafanyakazi wa Game frontiers of Tanzania wakiwa wamebeba pembe za ndovu
Pembe za ndovu, Risasi na Silaha zilizokamatwa

Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori wa Selou na Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .


Doria hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika pori hilo.


Akizungumza na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na risasi.


 Akiendelea kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na kundi la doria.



Ameongezea kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.


Nae Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE 458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA.
View detail

Tuesday, February 19, 2013

Rais wa Kenya Mh: Mwai Kibaki kuwasili nchini kesho kwa ya Ziara ya kitaifa ya siku mbili


Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mwai Kibaki anatarajia kuwasili nchini tarehe 20 Februari, 2013 kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili. Ziara hiyo ya Mhe. Rais Kibaki inafuatia mwaliko wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, ziara ya Mhe. Rais Kibaki inafanyika kufuatia ziara ya Mhe. Rais Kikwete nchini Kenya mwezi Septemba, 2012.

Mhe. Rais Kibaki ambaye anatarajiwa kuwasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 20 Februari, 2013 saa 9.00 alasiri, atapokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Akiwa hapa nchini, Mhe. Rais Kibaki atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete tarehe 20 Februari 2013 kabla ya kushiriki katika Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.

Mhe. Rais Kibaki anatarajiwa pia kukutana na  Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 21 Februari, 2013, kuzindua Barabara ya Mwai Kibaki na kutembelea Gereza Kuu la Ukonga Jijini Dar es Salaam ili kujionea shughuli mbalimbali zinazolenga kuwarekebisha Wafungwa kuwa Raia wema na kuwapa mafunzo ya kiufundi kuwawezesha kujitegemea wanapomaliza vifungo vyao. Shughuli hizo ni pamoja na ushonaji, useremala na kilimo cha kisasa.
Mhe. Rais Kibaki ataondoka nchini tarehe 21 Februari, 2013 kurejea nchini kwake.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
19 FEBRUARI, 2013
View detail

Monday, February 18, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATOKA RASMI



MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 BOFTA HAPA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.
Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na walio feli ni 24903.
Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys Dar es Salaam, Marian Girls Bagamoyo na Simini,hizo ndizo zilizopo kwenye tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.






View detail

Sunday, February 17, 2013

GHOROFA LAPOROMOKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA MAENEO YA SINZA JIONI HII

Jengo kuukuu la Ghorofa 5 ambalo lilikuwa halijamalizika ujenzi wake lililopo eneo la Sinza Mori karibu kabisa na Masjid Qubah,limeporomoka jioni hii na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa na wenzake wawili jirani na jengo hilo,ambapo mmoja alivyoona hatari hiyo alikimbia na kuwaacha wenzie wawili ambao walinasa ndani Kati ya walionasa mmoja amefanikiwa kutolewa huku akiwa ameumia vibaya na mwingine ndio huyo aliepoteza maisha.
Inasemekana chanzo cha kuanguka kwa jengo hilo la Ghorofa ni hali yake ya kukaa kwa muda mrefu bila kumalizika kwa ujenzi waka ambapo inadaiwa kuwa lina umri wa zaidi ya miaka 10.
View detail

UN yawaonya wakenya wasifanye ghasia


Ghasia za Kenya za mwaka wa 2008

Jumuia ya kimataifa itaingilia kati nchini Kenya iwapo ghasia zitazuka kabla au baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 4 March, endapo serikali haiwezi kudhibti hali.
Gazeti la Kenya la The East African limemnukuu mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kuzuwia mauaji ya kimbari, Adama Dieng, akisema mjini Nairobi kwamba ni wajibu wa serikali ya Kenya kuhakikisha usalama wa wananchi wake kwa kuzuwia ghasia.
Bwana Dieng alisema baada ya ghasia za miaka ya '90 na baada ya uchaguzi mwaka wa 2008, jumuia ya kimataifa itafanya iwezalo kuzuwia hayo yasitokee tena.
Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa alisema wanaweza kuingilia kati kwa vikwazo na kuzidisha uwezo wa serikali kupambana na ghasia.
Hatua ya tatu ni kuingilia kijeshi.
View detail

Friday, February 15, 2013

Washukiwa wa ICC Watagombea Kenya?



Uamuzi kuafikiwa ikiwa wawili hawa watawania nyadhifa za rais na makamu wake
Mahakama kuu nchini Kenya imeeleza kwamba haiwezi kuamua iwapo Uhuru Kenyatta na William Ruto wanapaswa kugombea nyadhifa katika uchaguzi mkuu ujao.
Wawili hao wanakabiliwa na tuhuma za kuchochea ghasia nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata na kusababisha mapigano ya kikabila.
Ikiwa zimesalia wiki mbili tu kwa uchaguzi mkuu kufanyika Kenya, inaonekana kuwa wananchi ndiyo watakaoamua kupitia kura, iwapo Uhuru Kenyatta na William Ruto wanafaa au hawafai kuwa viongozi nchini.
Uhuru Kenyatta anawania urais katika uchaguzi mkuu utakaokuja katika muda wa wiki mbili zijazo na makamu wake ni William Ruto.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mashirika yasiyo ya serikali yaliyotaka kubainishiwa iwapo viongozi hao wawili wa muungano wa kisiasa, Jubilee, wana uwezo wa kuhudumu katika ofisi ya serikali wakati wanatuhumiwa kwa kesi za uhalifu.
Hali ambayo mashirika hayo yanaona ni kwenda kinyume na katiba ya nchi.
Mahakama ilikuwa iangalie iwapo Uhuru na Ruto wangechaguliwa, wataweza kutimiza jukumu la kuiongoza nchi, wakati wanatuhumiwa kwa kuhusika na ghasia zilizoshuhudiwa Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, katika mahakama ya uhalifu ICC, mjini Hague Uholanzi.
Uamuzi huu umetolewa baada ya hapo jana kuwepo kikao cha mahakama hiyo ya uhalifu ICC, kukagua hali ya kesi hiyo inayowakabili wawili hao.
Kesi hiyo iliyowasilishwa na mashirika yasiyo ya kiserikali inaendelea katika mahakama kuu mjini Nairobi na inatarajiwa kutoa uamuzi iwapo mahakama ina uwezo wa kutoa uamuzi juu ya wawili hao au iwapo itahitaji usaidizi wa mahakama ya juu nchini kufikia uamuzi kuhusu hilo.
Zimesalia wiki mbili tu kwa uchaguzi mkuu kufanyika Kenya na uamuzi huu huenda ukawa na athari kubwa kwa uchaguzi ujao.
Mahakama inajaribu kuona iwapo Uhuru na Ruto ikiwa watachaguliwa wataweza kutimiza jukumu la kuiongoza nchi, na wakati huo huo kukabiliana na kesi inayowaandama katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC mjini Hague Uholanzi, ambapo wanatuhumiwa kuhusika na ghasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
View detail

Thursday, February 14, 2013

UMATI WA WATU WALIOHUDHURIA MAZISHI YA MWANAZUONI SHEIKH NASSOR ABDALLAH BACHU



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Masheikh mbali mbali
na mamia ya wananchi wa Zanzibar, akiwa katika mazishi ya Mwanazuoni na mhadhiri
maalum Zanzibar na eneo la Afrika Mshariki, Sheikh Nassor Abdallah Bachu huko katika
viwanja vya Mnazimmoja mjini Zanzibar jana. Alizikwa jana kijijini kwao Donge,
Wilaya ya Kaskazini 'B', Mkoa wa Kaskazi
View detail

Tuesday, February 12, 2013

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Watambulishwa na Rais kikwete mjini Dodoma leo

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kuwatambulisha wajumbe wapya wa Kamati kuu ya CCM ilkiyofanyika katika viwanja vya Makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCm Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM nje ya ukumbi wa White House,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na waliokuwa viongozi waandamizi wa CHADEMA.Kushoto anayevaa kofia ya CCM ni aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Mbozi Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA Bwana Mtela Mwampamba na kulia ni Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana CHADEMA Bi Juliana Shonza.Weninge katika picha ni Katibu mkuu wa CCMNdugu Abdulrahman Kinana(kulia) na kushoto ni Makamu Mweyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula. View detail

Monday, February 11, 2013

WAZIRI MEMBE AKAGUA UJENZI WA KIWANDA CHA SARUJI LINDI

Mkuu wa wilaya ya lindi Dr Hamidi Nassoro wa kwanza kushoto akiwa Waziri wa 
Mambo ya nje Bernard Membe (wapili kushoto akikagua maendeleo ya ujenzi wa 
Kiwanda Cha Cement Mkoani Lindi leo, ambako Kiwanda hicho kinajengwa 
na kutarajiwa kutoa ajira kwa zaidi ya watu 600.



Akipewa maelekezo na wasimamizi wa mradi huo na kampuni inayojenga

 
Waziri Membe Akiangalia vifaa vitakavyotumika kwenye ujenzi.


Magari na vifaa mbalimbali vikiendelea na kazi ya maandalizi ya ujenziwa kiwanda.
  
Vifaa vya kutosha kwenye eneo hilo vinaonekana huku kukiwa na vijana zaidi ya 280 wakiwa wamepata ajira za muda.

Baadhi ya vifaa kazi kwenye eneo hilo linalotarajiwa kuwa kiwanda  kikubwa cha cement.  
Takriban Wakazi 600 wa Manispaa ya Lindi watanufaika na Ajira mara  utakapokamilika Ujenzi wa Kiwanda cha Simenti kilichoanza hatua za awali za Ujenzi wake huku Tayari zaidi watu 260 wakiwa wamepata ajira katika hatua za awali baada ya kuanza kwa kazi hiyo hivi karibuni Akizungumza na Wakazi wa Manispaa ya Lindi mara baada ya kukagua kazi za Ujenzi wa kiwanda hicho kilichoanza ujenzi kufuatia Upatikanaji wa Gesikatika Mikoa ya Lindi na Mtwara,
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe alitoa wito kwa Wazazi na walezi kuongeza jitihada za kusomesha watoto wao ili wanufaikena ajira zitakazopatikana kutokana Uwepo wa Viwanda na shughuli mbalimbali zinazotokana na Gesi ikiwemo Upanuzi wa Bandari ya mji wa Lindi. Waziri Membe alitembelea kukagua kazi za ujenzi wa Kiwanda hichoMaeneo ya Machole Manispaa ya Lindi ambapo alielezwa kazi inavyoendelea na ajira zilizopo kwa sasa Sambamba na Gesi ya Mtwara,Waziri Membe alibainisha kuwa Kampuni ya Satoil ya Norway tayari imegundua uwepo wa Gesi nyingi umbali wa Km 85 baharini kutoka manispaa ya Lindi na kupatikana kwa gesi hiyo,Serikali tayari Imeshaingia mikataba ya Uchimbaji wake Gesi hiyo iliyogunduliwa na kampuni ya Satoil itasaidia maendeleo ya Lindi kwa kuwa kutajengwa kiwanda cha Mbolea,Kiwanda cha vifaa vya plastiki aina zote pamoja na Upatikanaji wa uhakika wa nishati ya Umeme alimalizia Membe kwa kusema Lindi Kucheleeeee!!!! 

Awali akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake,Meneja Mradi wa Lindi Cement kiwanda ambacho kinajengwa na Kampuni ya Meis Industries,Bw Valerian Magembe alibainisha kuwa kazi ya Ujenzi wa kiwanda hicho itakamilika na kuanza Uzalishaji June 2014 ambapo zaidi ya wananchi 600 watanufaika na Ajira na kueleza kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 500 kwa siku Ndg Waandishi mipango yetu iko vema kama mnavyoona kazi inavyoendelea na tayari Maji na Umeme ndio tunakamilisha,,Wana Lindi wakae mkao wakula kwa kupata ajira na ongezeko la pato la kila mdau kwa sekta yake Na pia nawahakikishia kiwanda hiki ni cha kisasa na hakutokuwa na uharibifu wa Mazingira kutakuwa na mtambo wa kudhibiti Vumbi Tumejipanga vilivyo Alimalizia Bw Magembe Kazi za Ujenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Kampuni ya Wazawa ya Meis Industries kinatarajiwa kuzalisha tani 500 kwa siku kitakapokamilika huku tayari ajira zaidi ya 280 zimetolewa kwa wakazi wa mji huo kwa awamu ya kwanza ya kazi za Ujenzi

View detail

Papa Benedict alazimika kujiuzulu

Huko Ujerumani, msemaji wa serikali amesema kuwa anaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Papa huyu aliyezaliwa katika Jimbo la Bavaria la nchini humo.
Papa Benedict
Baba Mtakatifu ameelezea kwamba matatizo ya kiafya yamemfanya kutangaza kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, amemsifu Papa kwa jitihada zake za kuimarisha mahusiano baina ya Vatican na Uingereza.
Askofu mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake.
Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa, waislamu na wayahudi.
Alikumbusha hotuba ya Papa alipozuru bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.
Uwamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.
Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, na sherehe za Pasaka.
Tabia ya kujiuzulu kwa Papa si ngeni, ingawa ni tukio jipya katika karne za hivi karibuni.
Mwandishi wa azizicompdoc.blogspot.com mjini Roma anasema habari hizi zimetokea kama radi, na kwamba hakukua natetesi yoyote juu ya uwezekano kama huu.
Msemaji wa Vatikani Father Federico Lombardi, amesema kuwa hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa na fununu juu ya tukio hili.
Kakake Papa huyu mzaliwa wa Ujerumani alipewa ushauri na Daktari wake asifanye ziara nyingine yoyote ya Marekani na kwamba kwa miezi kadhaa Mtakatifu Papa amekuwa akitafakari kujiuzulu.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake huko Regensburg, Ujerumani, Georg Ratzinger amesema kuwa Kaka yake alikuwa ameanza kupata shida ya kutembea na kwamba kujiuzulu kwake ni hatua ya kimaumbile.
Wakati wa kutawazwa kama Papa, Kadinali Joseph Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa akiwa mwenye umri mkubwa wa miaka 78.
Alitangazwa Papa mnamo mwezi Aprili 2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.
Uongozi wake ulitokea wakati wa wimbi kali la ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha miongo mingi, ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana.
Katika taarifa yake, Mtakatifu Papa amesema: "baada ya kujichunguza binafsi na nafsi yangu mbele ya Mola wangu, nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya, ukiambatana na umri mkubwa, ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Kuna kipengele katika sheria ya Kanisa kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki.
View detail

GEITA KWAZUKA VURUGU ZA KIDINI, HALI NI TETE


Habari zilizopo ni kuwa leo Geita mapigano yametokea kati ya Waislamu na Wakristo (particular Protestants wa AIC). Na hii ni baada ya Wachungaji wa AIC kutenga eneo la Buselesele kwa ajili ya machinjio ya Wakristo wao,maeneo ya Katoro na jirani ni vurugu na mtifuano!
Mapambano yanaendelea kwa silaha za jadi, mpaka sasa majeruhi kadhaa wana hali mbaya!
Hali imejitokeza baada ya Wachungaji wa AIC jana kuwatangazia waumini wao kuwa hawawezi kula nyama iliyochinjwa na Waislamu kama sehemu ya ibada,hivyo Wachungaji wakaamua kutenga eneo la Kanisa hapo

Buselesele kama machinjio...leo asubuhi wakachinja nyama na kuanza kuwauzia Wakristo, hali hiyo ikawafanya Waislamu kwenda kuvamia eneo hilo lenye "nyama haramu." Hali hiyo mpaka sasa imeleta mapigano makali, pikipiki zinachomwa, maduka yanafungwa na shughuli zimesimama.
Hali inazidi kuwa mbaya, misikiti inachomwa, mtu mmoja aripotiwa kuuwawa mpaka sasa, mchungaji mmoja kala kichapo na pikipiki yake kupigwa kiberiti...
Polisi wa Geita wamezidiwa wanakuja wengine toka Mwanza na Chato! Unaulizwa jina ukitaja la kinyume na waliokukamata unaanza kupewa doze!

View detail

Friday, February 8, 2013

WATOA HUDUMA ZA CHANJO WAUAWA NIGERIA




Ripoti kutoka nchini Nigeria zinsema kuwa watu 12 wakiwemo wafanyakazi waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio kwa watoto, wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Maafisa wa afya wameambia azizicompdoc.blogspot.com kuwa wafanyakazi wanane waliokuwa wanatoa chanjo waliuawa mjini Kano,na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Walioshuhudia mauaji hayo wanasema kuwa, watu wengine 8 waliuawa katika kituo cha afya maeneo ya Hotoro, karibu na mji wa Kano.
Miongoni mwa waliouawa ni wanawake waliokuwa wanawasubiri watoto wao, waliokuwa wanachanjwa.
Baadhi ya viongozi wa kiisilamu, Kaskazini mwa Nigeria wamekuwa wakipinga chanjo ya Polio, wakisema inasababisha watu kukosa uwezo wa kuzaa.
View detail

Thursday, February 7, 2013

UJENZI WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA MTWARA WAPAMBA MOTO KUENDANA NA KASI YA MAENDELEO

Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania (OUT) chanunua eneo Mtwara na chaanza ujenzi mara moja ili kuhakikisha kinaendana na kasi ya maendeleo kwa mikoa ya kusini na kuhakikisha watu wa maeneo hayo wanapata huduma hiyo kwa ukaribu na kwa hadhi inayostahili kama watanzania wengine.
Makamu mkuu wa chuo Hicho Prof  Tolly Salvatory A. Mbwete amesema atahakikisha ujenzi huo unakamilika mara moja ili alete  matumaini makubwa kwa wanamtwara na watanzania kwa ujumla na kuhakikisha kua elimu ya vyuo vikuu inakua ni haki kwa kila mtanzania mwenye sifa bila kuhangaika ktk kuipata elimu hiyo
Kwa kuhakikisha hayo kweli yanawezekana, Prof Mbwete amekwenda mwenyewe ktk eneo la ujenzi na kuhakikisha ujenzi unakwenda kwa kasi anayoitaka, jambo hilo limekua rahisi kwake kwa kua yeye ni mtaalamu aliyebobea ktk fani hiyo na kuhakikisha mambo yote yanakwenda bila wasiwasi. 
 
View detail

SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA 36 YA KUZALIWA KWA CCM MKOA WA LINDI ZATIKISA MJI



Viongozi wa CCM Wakiongozwa na Mama Salma Kikwete  wakikata keki kuashiria kuzaliwa kwa chama hicho

Mjumbe wa Halmashauri kuu wilaya ya Lindi ambae pia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewahimiza Wazazi mkoani Lindi kusimamia elimu ya watoto wao kwa kuhakikisha kuwa wanaenda shule ili kusaidia kuondokana na tatizo la watumishi waendeshaji na wanataaluma  katika mkoa huo ulio na rasilimali nyingi kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika kimkoa katika kata ya Chiponda -Rondo wilaya ya Lindi vijijini.
Mama Kikwete alipokua Lindi alieleza kuwa kutokana mikoa hiyo kuwa nyuma kimaendeleo sasa ifike wakati Wazazi na walezi kusaidia na kuakikisha watoto wao wanapata elimu kufuatia matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha pili hivyo basi kina baba washirikiane na wake zao kuhakikisha kuwa watoto wanahudhuria shule na kufanya vizuri katika masomo yao. 


Aidha Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM taifa aliwataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kutosubiri nafasi za upendeleo(viti maalum)
‘Wanawake wenzangu mjitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani na nje chama ili muingie katika ngazi ya maamuzi na kuachana na mawazo kuwa hamuwezi kuingia katika chaguzi za wananchi'alisema.
Sambamba na sherehe hizo Mama Kikwete aliwataka Wananchi wa Mkoa huo kuendelea kudumisha amani, upendo na utulivu, kufanya kazi kwa bidiii, maarifa na kujituma, wakulima walime kilimo cha kisasa ambacho kitawafanya wavune mazao mengi.

Awali Mama Kikwete pia alifungua jengo la ofisi ya CCM lenye thamani ya shilingi milioni 35 ambalo limejengwa na Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe.
Waziri Membe alisema kuwa jengo hilo lina vyumba sita ambavyo ni ofisi za jumuia zote za chama hicho ambazo ni Vijana, Wanawake, Wazazi, pia kuna ofisi za Mbunge, Mjumbe wa NEC na chumba cha mikutano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Ally Mtupa aliwataka wanachama wa chama hicho kuwa na mahusiano mazuri baina yao na viongozi wanaowaongoza. Wakisikia jambo wasiwe na papara ya kukimbilia kuandamana bali wafanye upelelezi kwanza na wakishabaini ukweli ndipo wachukue hatua. 

Mtupa alisema, “Hivi sasa kuna watu wanapita mitaani na kupotosha ukweli kuwa Serikaliyetu haijaleta maendeleo, wamesahau kuwa wanatembea katika barabara na kutibiwa katika Hospitali zilizojenga na CCM, tunawaomba watu hawa wawaheshimu viongozi wanaotawala kwani hata vitabu vya dini vinasisitiza umuhimu wa kuwatii viongozi waliopewa mamlaka ya kutawala”.
Sherehe hizo zilienda sambamba na mchango wa matembezi ya mshikamono ambapo zaidi ya shilingi milioni mbili zilipatikana, ufunguzi wa ofisi za CCM Kata ya Chiponda, ufanyaji wa usafi wa mazingira , kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, utoaji wa kadi kwa wanachama wapya ambapo wanachama wapya wa CCM 286 walijiunga,Jumuia ya wazazi 63 na kutoka vyama vya upinzani 23 walipewa kadi katika sherehe hizo.

Wanachama wa ccm wakisikiliza hotuba ya Mjumbe wa Nec,Mama salma kikwete

Mjumbe wa Nec,Mama Salma Kikwete akifurahia burdan iliyokuwa inatolewa na Wasanii katika sherehe za ccm


View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop